swc_rom_text_reg/04/16.txt

1 line
520 B
Plaintext

\v 16 Kwa hiyo ahadi inafuatana na imani, kusudi ikuwe imetolewa kwa neema ya Mungu. Na zaidi kuwe uhakikisho kwamba ahadi hiyo ni kwa ajili ya wazao wote wa Abrahamu, si kwa wale wanaotii Sheria tu, lakini vilevile kwa wale wanaokuwa na imani kama Abrahamu, babu yetu sisi wote. \v 17 Ni sawa vile inavyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: «Nimekuweka kuwa babu wa mataifa mengi. Abrahamu alimwamini Mungu, kwa hiyo yeye ni baba yetu mbele yake. Ni yeye Mungu anayewafufua wafu na kuamuru vitu visivyokuwa vipate kuwa.