\v 9 Uheri huu si kwa watu wanaotahiriwa tu, lakini ni kwa watu wasiotahiriwa vilevile. Kwa maana tumekwisha kusema kwamba Abrahamu alihesabiwa kuwa mwenye haki kwa njia ya imani yake. \v 10 Yeye alihesabiwa vile alipokuwa katika hali gani? Alipokuwa amekwisha kutahiriwa au alipokuwa hajatahiriwa bado? Halikutendeka nyuma ya kutahiriwa kwa Abrahamu lakini mbele ya kutahiriwa kwake!