\v 3 Yule anayekula kila chakula asimuzarau yule asiyekula kila chakula. Vilevile yule asiyekula kila chakula asimuhukumu yule anayekikula, kwa maana Mungu amemupokea. \v 4 Wewe ni nani unayehukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama imara katika kazi yake au akianguka, hilo ni shauri la bwana wake. Naye atasimama imara maana Bwana yuko na uwezo wa kumusimamisha.