swc_1co_text_reg/07/17.txt

1 line
458 B
Plaintext

\v 17 Kwa ngambo ingine, kila mtu aendelee kuishi kufuatana na zawadi aliyopewa na Bwana na kufuatana na vile alivyokuwa mbele ya kuitwa na Mungu. Hii ndiyo kanuni ninayofundisha katika makanisa yote. \v 18 Ikiwa mtu alitahiriwa mbele ya kuitwa na Mungu, asitafute kufuta kovu la kutahiriwa kwake. Ikiwa alikuwa hajatahiriwa wakati alipoitwa na Mungu, hapaswi kutahiriwa. \v 19 Kutahiriwa au kutotahiriwa hakufai kitu. Kitu kinachofaa ni kutii amri za Mungu.