sw_ulb/53-1TH.usfm

127 lines
10 KiB
Plaintext

\id 1TH
\ide UTF-8
\h 1 Wathesalonike
\toc1 1 Wathesalonike
\toc2 1 Wathesalonike
\toc3 1th
\mt 1 Wathesalonike
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Paulo, Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani iwe nanyi
\p
\v 2 Tunatoa shukrani kwa Mungu kila mara kwa ajili yenu nyote, wakati tunapowataja katika maombi yetu.
\v 3 Tunaikumbuka bila kukoma mbele ya Mungu na baba yetu kazi yenu ya imani, juhudi ya upendo, na uvumilivu wenye ujasiri kwa ajili ya baadaye katika Bwana Yesu Kristo.
\v 4 Ndugu Mnaopendwa na Mungu, tunajua wito wenu.
\v 5 Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu.
\v 6 Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.
\v 7 Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini.
\v 8 Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote.
\v 9 Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli.
\v 10 Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure.
\v 2 Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi.
\v 3 Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila.
\v 4 Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu.
\v 5 Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote, kama mjuavyo, wala hatukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu.
\v 6 Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo.
\v 7 Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe.
\v 8 Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mlikuwa wapendwa wetu.
\v 9 Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu.
\v 10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini.
\v 11 Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia
\v 12 kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake.
\p
\v 13 Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini.
\v 14 Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.
\v 15 Walikuwa ni Wayahudi ndiyo waliomuua Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni Wayahudi ambao walitufukuza tutoke nje. Hawampendezi Mungu na ni maadui kwa watu wote.
\v 16 Walituzuia tusiseme na Mataifa ili wapate kuokolewa. Matokeo yake ni kwamba wanaendelea na dhambi zao. Mwisho ghadhabu imekuja juu yao.
\p
\v 17 Sisi, ndugu, tulikuwa tumetengana nanyi kwa muda mfupi, kimwili, si katika roho. Tulifanya kwa uwezo wetu na kwa shauku kuu kuona nyuso zenu.
\v 18 Kwa kuwa tulitaka kuja kwenu, mimi Paulo, kwa mara moja na mara nyingine, lakini shetani alituzuia.
\v 19 Kwa kuwa kujiamini kwetu ni nini, au furaha, au taji ya kujivunia mbele za Bwana wetu Yesu wakati wa kuja kwake? Je si ninyi zaidi kama walivyo wengine?
\v 20 Kwa kuwa ninyi ni utukufu na furaha yetu.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Kwa hiyo, tulipo kuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuwa vema kubaki kule Athene peke yetu.
\v 2 Tulimtuma Timotheo, ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika injili ya Kristo, kuwaimalisha na kuwafariji kuhusiana na imani yenu.
\v 3 Tulifanya haya ili kusudi asiwepo yeyote wa kuteteleka kutokana na mateso haya, kwa kuwa wenyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili.
\v 4 Kwa kweli, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitangulia kuwaeleza ya kuwa tulikuwa karibu kupata mateso, na hayo yalitokea kama mjuavyo.
\v 5 Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ilikusudi nipate kujua juu ya imani yenu. Huenda mjaribu alikuwa angalau amewajaribu, na kazi yetu ikawa ni bure.
\p
\v 6 Lakini Timotheo alikuja kwetu kutokea kwenu na akatuletea habari njema juu ya imani na upendo wenu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu yetu, na kuwa mnatamani kutuona kama ambavyo nasi twatamani kuwaona ninyi.
\v 7 Kwa sababu hii, ndugu tulifarijika sana na ninyi kwa sababu ya imani yenu, katika taabu na mateso yetu yote.
\v 8 Kwa sasa tunaishi, kama mkisimama imara kwa Bwana,
\v 9 Kwani ni shukurani zipi tumpe Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tuliyonayo mbele za Mungu juu yenu?
\v 10 Tunaomba sana usiku na mchana ili tuweze kuziona nyuso zenu na kuwaongezea kinachopungua katika imani yenu.
\p
\v 11 Mungu wetu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia yetu tufike kwenu.
\v 12 Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi katika pendo, mkipendana na kuwapenda watu wote, kama tunavyowafanyia ninyi.
\v 13 Na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu na Baba yetu katika ujio wa Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Hatimaye, ndugu, twawatia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maelekezo toka kwetu namna iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kwa njia hiyo pia muenende na kutenda zaidi.
\v 2 Kwa kuwa mwajua ni maelekezo gani tuliyowapa kupitia Bwana Yesu.
\p
\v 3 Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wenu - kwamba muepuke zinaa,
\v 4 Kwamba kila mmoja wenu anajua namna ya kumiliki mke wake mwenyewe katika utakatifu na heshima.
\v 5 Usiwe na mke kwa ajili ya tamaa za mwili (kama Mataifa wasiomjua Mungu).
\v 6 Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia.
\v 7 Kwa kuwa Bwana hakutuita kwa uchafu, bali kwa utakatifu.
\v 8 Kwa hiyo anayelikataa hili hawakatai watu, bali anamkataa Mungu, anayewapa Roho wake Mtakatifu.
\p
\v 9 Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja ya mtu yeyote kuwaandikia, kwa kuwa mmefundishwa na Mungu kupendana ninyi kwa ninyi.
\v 10 Hakika, mlifanya haya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote, lakini twawasihi, ndugu, mfanye hata na zaidi.
\v 11 Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru.
\v 12 Fanya haya ili uweze kuenenda vizuri na kwa heshima kwa hao walio nje ya imani, ili msipungukiwe na hitaji lolote.
\p
\v 13 Hatutaki mkose kujua, enyi ndugu, juu ya hao waliolala, ili msije mkahuzunika kama wengine wasio na uhakika kuhusu wakati ujao.
\v 14 Iwapo tunaamini kuwa Yesu alikufa na akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti katika yeye.
\v 15 Kwa ajili ya hayo twawaambia ninyi kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaokuwepo wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti.
\v 16 Kwa kuwa Bwana mwenyewe atashuka toka mawinguni. Atakuja na sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza.
\v 17 Kisha sisi tulio hai, tuliobaki, tutaungana katika mawingu pamoja nao kumlaki Bwana hewani. Kwa njia hii tutakuwa na Bwana milele.
\v 18 Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Sasa, kwa habari ya muda na nyakati, ndugu, hamna haja kuwaandikia.
\v 2 Kwa kuwa ninyi wenyewe mwajua ya kuwa siku ya Bwana inakuja kama mwizi ajapo usiku.
\v 3 Pale wasemapo kuna “Amani na usalama,” ndipo uharibifu huwajia ghafla. Ni kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba. Hawataepuka kwa njia yeyote.
\v 4 Lakini ninyi, ndugu hampo kwenye giza hata ile siku iwajie kama mwizi.
\v 5 Kwa maana ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi siyo wana wa usiku au wa gizani.
\v 6 Hivyo basi, tusilale kama wengine walalavyo. Bali tukeshe na kuwa makini.
\v 7 Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku.
\v 8 Kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, tuwe makini. Tuvae ngao ya imani na upendo, na, kofia ya chuma, ambayo ni uhakika wa wokovu wa wakati ujao.
\p
\v 9 Kwa kuwa Mungu hakutuchagua mwanzo kwa ajili ya gadhabu, bali kwa kupata wokovu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo.
\v 10 Yeye ndiye aliyetufia ili kwamba, tukiwa macho au tumelala, tutaishi pamoja naye.
\v 11 Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.
\p
\v 12 Ndugu, twawaomba muwatambue wale wanaotumika miongoni mwenu na wale walio juu yenu katika Bwana na wale wanao washauri.
\v 13 Tunawaomba pia muwatambue na kuwapa heshima katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Muwe na amani miongoni mwenu ninyi wenyewe.
\p
\v 14 Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote.
\v 15 Angalieni asiwepo mtu yeyote anayelipa baya kwa baya kwa mtu yeyote. Badala yake, fanyeni yaliyo mema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
\p
\v 16 Furahini siku zote.
\v 17 Ombeni bila kukoma.
\v 18 Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.
\p
\v 19 Msimzimishe Roho.
\v 20 Msiudharau unabii.
\v 21 Yajaribuni mambo yote. Mlishike lililo jema.
\v 22 Epukeni kila mwonekano wa uovu.
\p
\v 23 Mungu wa amani awakamilishe katika utakatifu. Roho, nafsi na mwili vitunzwe pasipo mawaa katika kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
\v 24 Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda.
\p
\v 25 Ndugu, tuombeeni pia.
\v 26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.
\v 27 Nawasihi katika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu wote.
\v 28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.