sw_ulb/10-2SA.usfm

1142 lines
105 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id 2SA
\ide UTF-8
\h 2 Samweli
\toc1 2 Samweli
\toc2 2 Samweli
\toc3 2sa
\mt 2 Samweli
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alirudi kutoka kuwashambulia Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.
\v 2 Siku ya tatu, mtu mmoja alikuja kutoka kambi ya Sauli nguo zake zikiwa zimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake. Alipofika kwa Daudi akaanguka chini na akamsujudia.
\p
\v 3 Daudi akamuuliza, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Nimeponyoka kutoka kambi ya Israeli.”
\p
\v 4 Daudi akamwambia, “Tafadhali nieleze jinsi mambo yalivyokuwa.” Akajibu, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wameanguka, na wengi wao wameuawa. Sauli na Yonathani mwanawe pia wameuawa.”
\p
\v 5 Daudi akamwuliza kijana, “Unajuaje kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wameuawa?”
\p
\v 6 Yule kijana akajibu, “Kwa bahati nilikuwa juu ya Mlima Gilboa, na pale alikuwepo Sauli ameegemea mkuki wake, na magari ya farasi na waongozaji walikuwa karibu kumkamata.
\v 7 Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, Mimi hapa.
\p
\v 8 Akaniuliza, Wewe ni nani? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki,
\p
\v 9 Akaniambia, Tafadhali simama juu yangu uniue, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.
\p
\v 10 Hivyo nilisimama juu yake nikamuua, kwa maana nilijua kwamba asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka. Ndipo nikachukua taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, na nimevileta hapa kwako, bwana wangu.”
\p
\v 11 Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.
\v 12 Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.
\p
\v 13 Daudi akamwambia yule kijana, “Unatokea wapi?” Akajibu, “Mimi ni kijana wa mgeni Mwamaleki.”
\p
\v 14 Daudi akamwambia, “Kwa nini haukuogopa kumuua mfalme, mtiwa mafuta wa Yahwe kwa mkono wako?”
\v 15 Daudi akamwita mmojawapo wa vijana na akamwambia, “Nenda ukamuue.” Hivyo kijana huyo akaenda na kumpiga hata chini, Mwamaleki akafa.
\v 16 Ndipo Daudi akamwambia Mwamaleki aliyekufa, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako kwa kuwa kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako kusema, Nimemuua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe.’”
\p
\v 17 Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe.
\v 18 Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Upinde kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari.
\q1
\v 19 “Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
\q1
\v 20 Msiiseme katika Gathi, msiitangaze katika mitaa ya Ashikeloni, ili binti za wafilisti wasifurahi, ili binti za wasiotailiwa wasisherehekee.
\q1
\v 21 Enyi Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu, wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haikupakwa mafuta.
\q1
\v 22 Kutoka katika damu ya waliouawa, kutoka katika miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu.
\q1
\v 23 Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
\q1
\v 24 Enyi binti wa Israeli lieni juu ya Sauli, aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
\q1
\v 25 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka vitani! Yonathani ameuawa juu ya mahali pako pa juu.
\q1
\v 26 Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
\q1
\v 27 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka na silaha za vita zimeteketea!”
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Ikawa baada ya haya Daudi akamuuliza Yahwe, “Je naweza kuupandia mmojawapo wa miji ya Yuda?” Yahweh akamjibu, “Panda.” Daudi akauliza, “Niuendee mji upi? Yahwe akajibu, “Hebroni”
\p
\v 2 Hivyo Daudi akakwea pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, mjane wa Nabali.
\v 3 Daudi akawaleta watu waliokuwa pamoja naye, na kila mmoja akaleta familia yake katika mji wa Hebroni walipoanza kuishi.
\v 4 Kisha watu wa Yuda wakaja na kumtia Daudi mafuta kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi, “Watu wa Yabeshi Gileadi wamemzika Sauli.”
\v 5 Hivyo Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi Gileadi akawaambia, “Mbarikiwe na Yahwe, kwa kuwa mmeonyesha utiifu huu kwa bwana wenu Sauli mliyemzika.
\v 6 Sasa Yahwe awadhihirishie utiifu na uaminifu wa kiagano. Nami pia nitawaonyesha wema kwa sababu ya yale mliyoyafanya.
\v 7 Sasa basi, mikono yenu itiwe nguvu; mwe jasiri kwa maana Sauli bwana wenu amekufa, na nyumba yote ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme wao.”
\p
\v 8 Lakini Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi la Sauli, akamchukuwa Ishboshethi mwana wa Sauli akamleta Mahanaimu.
\v 9 Akamfanya Ishboshethi mfalme juu ya Gileadi, Asheri, Yezreeli, Efraimu, Benjamini na juu ya Israeli yote.
\p
\v 10 Ishiboshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili. Lakini nyumba ya Yuda ikaambatana na Daudi.
\v 11 Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ni miaka saba na miezi sita.
\p
\v 12 Abneri mwana wa Neri na watumishi wa Ishboshethi mwana wa Sauli walitoka Mahanaimu kwenda Gibeoni.
\v 13 Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi wakatoka na kukutana nao katika bwawa la Gibeoni. Wakakaa pale, kundi moja upande huu wa bwawa na kundi lingine upande wa pili.
\p
\v 14 Abneri akamwambia Yoabu, “Haya, vijana na wainuke na kushindana mbele yetu.” Yoabu akajibu, “Haya na wainuke.”
\p
\v 15 Ndipo vijana walipoinuka na kukutana, kumi na wawili kwa ajili ya Banjamini na Ishboshethi mwana wa Sauli, na kumi na wawili kutoka kwa watumishi wa Daudi.
\v 16 Kila mtu akakamata kichwa cha adui yake na kupiga upanga wake katika ubavu wa adui yake, wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa kwa Kiebrania, “Helkath-Hasurimu,” yaani “konde la upanga,” lililopo Gibeoni.
\p
\v 17 Vita vikawa vikali sana siku ile na Abneri na watu wa Israeli wakashindwa mbele ya watumishi wa Daudi.
\p
\v 18 Wana watatu wa Seruya walikuwepo pale: Yoabu, Abishai na Asaheli.
\v 19 Asaheli alikuwa mwepesi miguuni kama paa. Akamfuatilia Abneri kwa karibu bila kugeuka upande wowote.
\v 20 Abneri akaangalia nyuma yake na kusema, “Ni wewe Asaheli?” Akajibu, “Ni mimi.”
\p
\v 21 Abneri akamwambia, “Geuka upande wako wa kulia au kushoto umshike mmojawapo wa vijana na kuchukua silaha yake.” Lakini Asaheli hakugeuka.
\p
\v 22 Ndipo Abneri alipomwambia tena Asaheli, “Simama usinifuate. Kwa nini nikupige hata chini? Nitautazamaje uso wa Yoabu ndugu yako?”
\p
\v 23 Lakini Asaheli hakukubali kugeuka; na hivyo Abneri akamchoma kwa nchi ya mkuki wake, hata ukatokea upande wa pili. Asaheli akaanguka chini akafa. Hata ikawa kila mmoja aliyefika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa, alisimama hapo hapo.
\p
\v 24 Lakini Yoabu na Abishai wakamfuatilia Abneri. Wakati jua linazama walikuwa wamefika mlima wa Amma, uliopo karibu na Gia katika njia ielekeayo nyika ya Gibeoni.
\v 25 Wabenjamini wakajikusanya nyuma ya Abneri na kusimama juu ya kilima.
\p
\v 26 Kisha Abneri akamwita Yoabu na kusema, “Je! Ni lazima upanga uendelee kurarua daima? Je, haujui kwamba mwisho wake utakuwa mchungu? Hata lini ndipo uwaambie watu wako waache kuwafuatia ndugu zao?”
\p
\v 27 Yoabu akajibu, “Kama Mungu aishivyo, usingesema hivyo, askari wangu wangewafuatia ndugu zao hata asubuhi!”
\p
\v 28 Ndipo Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wake wote wakasimama na hawakuendelea kuwafuata Israeli tena wala hawakupigana tena.
\p
\v 29 Abneri na watu wake wakasafiri usiku wote kupitia Araba. Wakavuka Yordani, wakatembea asubuhi yote iliyofuata, na hata wakafika Mahanaimu.
\p
\v 30 Yoabu akarudi kutoka katika kumfuatia Abneri. Akawakusanya watu wake wote, ambopo Asahali na askari wengine kumi na tisa wa Daudi walipungua.
\v 31 Lakini watu wa Daudi walikuwa wameua watu 360 wa Benjamini na Abneri.
\v 32 Kisha wakamchukua Asahali na kumzika katika kaburi la baba yake, lililokuwapo Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakasafiri usiku wote, kukacha wakati wanafika Hebroni.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Kulikuwa na vita ya mda mrefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi. Daudi akaendelea kupata nguvu zaidi, lakini nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika na kudhoofika.
\q
\v 2 Wana wakazaliwa kwa Daudi huko Hebroni. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu wa Yezreeli.
\q2
\v 3 Mwanawe wa pili, Kileabu, alizaliwa kwa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Wa tatu, Absalomu, alikuwa mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
\q2
\v 4 Mwana wa nne wa Daudi, Adoniya, alikuwa mwana wa Hagithi. Mwanawe wa tano alikuwa Shefatia mwana wa Abitali,
\q2
\v 5 na wa sita, Ithreamu, alikuwa mwana wa Egla mkewe Daudi. Hawa wote walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni.
\p
\v 6 Ikawa wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi Abneri akajifanya mwenye nguvu katika nyumba ya Sauli.
\v 7 Sauli alikuwa na suria jina lake Rispa, binti Aiya. Ishboshethi akamuuliza Abneri, “Kwa nini umeingia kwa suria ya baba yangu?”
\p
\v 8 Hata ikawa Abneri akakasirika sana kutokana na maneno ya Ishboshethi naye akasema, “Je mimi ni kichwa cha mbwa wa Yuda? Ninaonyesha uaminifu kwa nyumba ya Sauli, baba yako, kwa jamaa yake, na rafiki zake, kwa kutokukuweka katika mkono wa Daudi. Na bado leo unanishtaki kwa uovu kuhusu huyu mwanamke.
\v 9 Mungu na anifanyie hivyo, Abneri, na kuzidi, ikiwa sitafanya kwa Daudi kama Yahwe alivyomwapia,
\v 10 kuuhamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kukisimamisha kiti cha enzi cha Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hadi Beersheba.”
\v 11 Ishboshethi hakuweza kumjibu Abneri neno tena, kwani alimuogopa.
\p
\v 12 Kisha Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi kusema, “Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, nawe utaona kwamba mkono wangu uko nawe, kuiIeta Israeli yote kwako.”
\v 13 Daudi akajibu, “Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami.”
\v 14 Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, “Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti.”
\p
\v 15 Hivyo Ishboshethi akatuma kwa Mikali na kumchukua kutoka kwa mme wake, Paltieli mwana wa Laishi.
\v 16 Mme wake akafuatana naye, huku akilia, akaendelea hadi Bahurimu. Kisha Abneri akamwambia, “Basi sasa rudi nyumbani.” Hivyo akarudi.
\p
\v 17 Abneri akaongea na wazee wa Israeli kusema, “Zamani mlitaka Daudi awe mfalme wenu.
\v 18 Basi sasa fanyeni hivyo. Kwa maana Yahwe alisema kuhusu Daudi kusema, “Kwa mkono wa Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka katika mkono wa Wafilisti na kutoka katika mkono wa adui zao wote.”
\v 19 Pia Abneri akasema na watu wa Benjamini ana kwa ana. Kisha Abneri akaenda kuongea na Daudi huko Hebroni akaeleza kila jambo ambalo Israeli na nyumba yote ya Benjamini walitamani kulitimiza.
\p
\v 20 Wakati Abneri na watu ishirini kati ya watu wake walifika Hebroni kumuona Daudi, Daudi akaandaa sherehe kwa ajili yao.
\v 21 Abneri akamueleza Daudi, “Nitainuka na kukukusanyia Israeli wote, bwana wangu mfalme, ili kwamba wafanye agano nawe, kwamba utawale juu ya yote unayotaka.” Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka, Abneri akaondoka kwa amani.
\p
\v 22 Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani.
\v 23 Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, “Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani.”
\p
\v 24 Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, “Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye ameenda?
\v 25 Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?”
\p
\v 26 Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sira, lakini Daudi hakulijua hili.
\v 27 Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoma tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
\p
\v 28 Daudi alipolisikia jambo hili akasema, “Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri.
\v 29 Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kilema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula.”
\p
\v 30 Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamuua Abneri, kwa sababu alimuua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.
\p
\v 31 Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, “Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri.” Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi.
\v 32 Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.
\p
\v 33 Mfalme akamwomboleza Abneri naye akaimba, “Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?
\q2
\v 34 Mikono yako haikufungwa. Miguu yako haikuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.” Watu wote wakamlilia zaidi.
\p
\v 35 Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, “Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama.”
\v 36 Watu wote wakaiona huzuni ya Daudi, na ikawapendeza, hivyo kila alichokifanya mfalme kikawapendeza.
\p
\v 37 Hivyo watu wote na Israeli yote wakatambua siku hiyo kwamba haikuwa nia ya mfalme Abneri mwana wa Neri afe.
\v 38 Mfalme akawaambia watumishi wake, “Je hamjui kuwa mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?
\v 39 Nami leo nimedhoofika, japokuwa nimetiwa mafuta kuwa mfalme. Watu hawa, wana wa Seruya ni hatari sana kwangu. Yahwe na amrudishie muovu kwa kumlipa kwa ajili ya uovu wake kama anavyostahili.”
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Ikawa Ishboshethi, mwana wa Sauli, aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, mikono yake ikadhoofika, na Israeli yote ikataabika.
\v 2 Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi vya askari. Mmoja wao alikuwa Baana na mwingine alikuwa Rekabu, wana wa Rimoni Mbeerothi wa wana wa Benjamini (kwa maana Berothi ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini,
\v 3 na Waberothi walikimbilia Gitaimu na wamekuwa wakiishi pale hadi sasa).
\p
\v 4 Basi Yonathani, mwana wa Sauli, alikuwa na mwana mlemavu wa miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano habari kuhusu Sauli na Yonathani ilipofika Yezreeli. Yaya wake akamchukua ili akimbie. Lakini wakati anakimbia, mwana wa Yonathani alianguka na akawa kilema. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.
\p
\v 5 Hivyo wana wa Rimoni Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana.
\v 6 Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita.
\p
\v 7 Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.
\v 8 Wakaleta kichwa cha Ishboshethi kwa Daudi huko Hebroni, nao wakamwambia mfalme, “Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyekuwa akiutafuta uhai wako. Leo Yahwe amemlipia kisasi bwana wetu mfalme dhidi ya Sauli na uzao wake.”
\p
\v 9 Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni Mbeerothi, akawambia, “Kama Yahwe aishivyo, aliyeuokoa uhai wangu na kila shida,
\v 10 mtu mmoja aliponiambia, Tazama, Sauli amekufa, akifikiri alileta habari njema, nilimkamata na kumuua huko Siklagi. Huo ndio ujira niliompa kwa habari yake.
\v 11 Namna gani, watu waovu wamemuua mwenye haki kitandani mwake ndani ya nyumba, Je, nisiitake damu yake kutoka katika mikono yenu, na kuwaondoa duniani?”
\p
\v 12 Kisha Daudi akawaagiza vijana, nao wakawaua wakakata mikono na miguu yao na kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika katika kaburi la Abneri katika Hebroni.
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Kisha kabila zote za Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni nao wakasema, “Tazama, sisi ni nyama na mifupa yako.
\v 2 Kipindi kilichopita, Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliyeliongoza jeshi la Waisraeli. Yahwe akakwambia, Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli.’”
\p
\v 3 Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebroni na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli.
\v 4 Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.
\v 5 Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sita huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.
\p
\v 6 Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kupigana na Wayebusi, waliokuwa wenyeji wa nchi. Wakamwambia Daudi, “Hautaweza kuja hapa kwani hata vipofu na vilema waweza kukuzuia kuingia. Daudi hawezi kuja hapa.”
\v 7 Lakini, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, ambayo sasa ni mji wa Daudi.
\v 8 Wakati huo Daudi akasema, “Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie vilema na vipofu ambao ni adui wa Daudi.” Hii ndiyo maana watu husema, “Vipofu na vilema wasiingie katika kasri.”
\p
\v 9 Hivyo Daudi akaishi ngomeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani.
\v 10 Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.
\p
\v 11 Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.
\v 12 Daudi akatambua kuwa Yahwe alikuwa amemuweka ili awe mfalme juu ya Israeli, na kwamba alikuwa ameutukuza ufalme wake kwa ajili ya Israeli watu wake.
\p
\v 13 Baada ya Daudi kuondoka Hebroni na kwenda Yerusalemu, akajitwalia wake na masuria wengi huko Yerusalemu, na wana na binti wengi walizaliwa kwake.
\v 14 Haya ndiyo majina ya wanawe waliozaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Selemani,
\v 15 Ibhari, Elishua, Nefegi, Yafia,
\v 16 Elishama, Eliada na Elifeleti.
\p
\v 17 Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.
\v 18 Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.
\v 19 Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?” Yahwe akamwambia Daudi, “Washambulie, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya Wafilisti.”
\p
\v 20 Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.
\v 21 Wafilisti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.
\p
\v 22 Kisha Wafilisti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.
\v 23 Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.
\v 24 Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisti.”
\v 25 Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomuamuru. Akawauwa wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Basi kwa mara nyingine Daudi akawakusanya wateule wa Israeli, 30,000.
\v 2 Daudi akainuka na akaenda na watu wake wote waliokuwa pamoja naye kutoka Baala mji ulioko Yuda ili alilete sanduku la Mungu, liitwalo kwa jina la Yahwe wa majeshi, akaaye juu ya makerubi.
\v 3 Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wanawe, wakauongoza mkokoteni.
\v 4 Wakautoa mkokoteni na sanduku la Mungu juu yake nyumbani mwa Abinadabu juu ya kilima. Ahio alikuwa ametangulia mbele ya sanduku.
\v 5 Kisha Daudi na nyumba yote ya Israeli wakaanza kucheza mbele ya Yahwe, wakishangilia kwa vyombo vya mziki, vinubi, vinanda, matari, kayamba na matowazi.
\p
\v 6 Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia.
\v 7 Kisha hasira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.
\p
\v 8 Daudi akakasirika kwa kuwa Yahwe alimpiga Uza, naye akapaita mahali pale Peresi Uza. Eneo hilo linaitwa Peresi Uza hata leo.
\p
\v 9 Daudi akamuogopa Yahweh siku hiyo. Akasema, “Sanduku la Yahwe lawezaje kuja kwangu?”
\v 10 Hivyo Daudi hakuwa tayari tena kulichukua sanduku la Yahwe katika mji wa Daudi. Badala yake, akaliweka kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
\v 11 Sanduku la Yahwe likakaa katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti kwa miezi mitatu. Kwa hiyo Yahwe akambariki yeye na nyumba yake yote.
\p
\v 12 Kisha mfalme Daudi akaambiwa, “Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.” Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.
\v 13 Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.
\v 14 Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.
\v 15 Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.
\p
\v 16 Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamuona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.
\p
\v 17 Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.
\v 18 Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.
\v 19 Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.
\p
\v 20 Kisha Daudi akarudi ili aibariki familia yake. Mikali, binti Sauli, akatoka ili akutane na Daudi naye akasema, “Jinsi gani mtukufu mfalme wa Israeli alivyokuwa leo, aliyejiacha uchi mbele ya macho ya vijakazi miongoni mwa watumishi wake, kama mmoja wa wapumbavu ambaye bila aibu hujifunua yeye mwenyewe!”
\p
\v 21 Daudi akamjibu Mikali, “Nilifanya hivyo mbele ya Yahwe, aliyenichagua juu ya baba yako na juu ya familia yake yote, aliyeniweka kuwa kiongozi juu ya watu wa Yahwe, juu ya Israeli. Mbele ya Yahwe nitafurahi!
\v 22 Nitakuwa nisiye na heshima hata zaidi ya hapa, na nitajishusha mbele za macho yangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliowasema, nitaheshimiwa.”
\p
\v 23 Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watoto hata alipokufa.
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Ikawa mfalme alipokuwa amekwisha kukaa katika nyumba yake, na baada ya Yahwe kuwa amemstarehesha kutokana na adui zake wote waliomzunguka,
\v 2 mfalme akamwambia nabii Nathani, “Tazama, mimi ninaishi katika nyumba ya mierezi, lakini sanduku la Mungu lipo hemani.”
\p
\v 3 Basi Nathani akamwambia mfalme, “Nenda, fanya lililo moyoni mwako, kwa maana Yahwe yupo nawe.”
\p
\v 4 Lakini usiku uleule neno la Yahwe lilimjia Nathani kusema,
\pi
\v 5 “Nenda na umwambie mtumishi wangu Daudi, Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Je utanijengea nyumba ya kuishi?”
\v 6 Kwa maana sijawai kuishi katika nyumba tangu siku ile nilipowaleta wana wa Israeli kutoka Misri hata leo; badala yake nimekuwa nikitembea katika hema, hema la kukutania.
\v 7 Mahali pote ambapo nimekuwa nikihama miongoni mwa wana wote wa Israeli, Je niliwahi kusema lolote na viongozi wa Israeli niliowaweka kuwachunga watu wangu Israeli, kusema, Kwa nini hamjanijengea nyumba ya mierezi?
\pi
\v 8 Sasa basi, mwambie Daudi, mtumishi wangu, Hiki ndicho asemacho Yahwe wa majeshi: Nilikutwaa kutoka machungani, kutoka katika kuwafuata kondoo, ili uwe mtawala juu ya watu wangu Israeli.
\v 9 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda na nimewakatilia mbali adui zako wote mbele yako. Na nitakutengenezea jina kubwa, kama jina la mojawapo ya wakuu walio juu ya nchi.
\v 10 Nitatenga mahali kwa ajili ya watu wangu Israeli nami nitawapanda pale, ili kwamba waweze kuishi mahali pao wenyewe na wasisumbuliwe tena. Waovu hawatawatesa tena, kama walivyofanya mwanzo.
\v 11 Kama walivyofanya tangu siku ile nilipoamuru waamuzi juu ya watu wangu Israeli. Nami nitakustarehesha kutokana na adui zako wote. Zaidi ya hayo, Mimi, Yahwe, nakutamkia kwamba nitakutengenezea nyumba.
\v 12 Siku zako zitakapokwisha na ukalala pamoja na baba zako, nitainua mzao baada yako, atokaye katika mwili wako mwenyewe, nitauimarisha ufalme wake.
\v 13 Naye atajenga nyumba kwa jina langu, nami nitakiimarisha kiti chake cha enzi daima.
\v 14 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwanangu. Atakapotenda dhambi, nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu na kwa mapigo ya wana wa watu.
\v 15 Lakini uaminifu wa agano langu hautamwondokea, kama nilivyouondoa kutoka kwa Sauli, niliyemwondoa mbele yako.
\v 16 Nyumba yako na ufalme wako utathibitishwa mbele yako daima. Kiti chako cha enzi kitakuwa imara daima.’”
\p
\v 17 Nathani akamwambia Daudi na kumtaarifu maneno haya yote, na akamwambia kuhusu ono lote.
\p
\v 18 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani na kuketi mbele ya Yahwe; akasema, “Mimi ni nani, Yahwe Mungu, na familia yangu ni nini hata umenileta hapa nilipo?
\pi
\v 19 Na hili lilikuwa jambo dogo mbele yako, Bwana Yahwe. Hata ukasema kuhusu familia ya mtumishi wako wakati mkuu ujao, nawe umenionyesha vizazi vijavyo, Bwana Yahwe!
\pi
\v 20 Mimi Daudi, niseme nini zaidi kwako? Umemjua mtumishi wako, Bwana Yahwe.
\v 21 Kwa ajili ya neno lako, na kwa ajili ya kutimiza kusudi lako mwenyewe, umefanya jambo kubwa namna hii na kulidhihirisha kwa mtumishi wako.
\pi
\v 22 Kwa hiyo wewe ni mkuu, Bwana Yahwe. Kwa maana hakuna mwingine aliye kama wewe, na hakuna Mungu mwingine badala yako, kama jinsi ambayo tumesikia kwa masikio yetu wenyewe.
\v 23 Kwani kuna taifa lipi lililo kama watu wako Israeli, taifa moja juu ya nchi ambalo wewe, Mungu, ulikwenda na kuwakomboa kwa ajili yako wewe mwenyewe? Ulifanya hivi ili kwamba wawe watu kwa ajili yako mwenyewe, kujifanyia jina kwa ajili yako mwenyewe, na kufanya matendo makuu na ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako. Uliyaondoa mataifa na miungu yao kutoka mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri.
\v 24 Umeiimarisha Israel kama watu wako daima, na wewe, Yahwe, kuwa Mungu wao.
\pi
\v 25 Basi sasa, Yahwe Mungu, ahadi uliyofanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima. Ufanye kama ulivyo sema.
\v 26 Na jina lako liwe kuu daima, ili watu waseme, Yahwe wa majeshi ni Mungu wa Israeli, wakati nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako itakapokaa imara mbele zako daima.
\pi
\v 27 Kwa maana wewe, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, umedhihirisha kwa mtumishi wako kwamba utamjengea nyumba. Ndiyo maana mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri kuomba kwako.
\v 28 Sasa, Bwana Yahwe, wewe ni Mungu, na maneno yako ni amini, na umefanya ahadi hii njema kwa mtumishi wako.
\v 29 Sasa basi, na ikupendeze kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili iendelee mbele yako daima. Kwa maana wewe, Bwana Yahwe, umeyasema mambo haya, na kwa ahadi yako nyumba ya mtumishi wako itabarikiwa daima.
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.
\p
\v 2 Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.
\p
\v 3 Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.
\v 4 Daudi aliteka magari 1,700 ya farasi na askari 20,000 waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.
\p
\v 5 Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu 22,000.
\v 6 Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.
\p
\v 7 Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.
\v 8 Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.
\p
\v 9 Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,
\v 10 Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.
\p
\v 11 Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-
\v 12 kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilisti, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.
\p
\v 13 Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao 18,000.
\p
\v 14 Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.
\p
\v 15 Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote.
\v 16 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.
\v 17 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi.
\v 18 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Kisha Daudi akasema, “Je, kuna yeyote aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumuonyesha wema kwa ajili ya Yonathani?”
\p
\v 2 Alikuwepo mtumishi katika familia ya Sauli jina lake Siba, akaitwa kwa Daudi. Mfalme akamuuliza, “Je wewe ndiye Siba?” Akajibu, “Mimi ni mtumishi wako, ndiye.”
\p
\v 3 Hivyo mfalme akasema, “Je hakuna aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumuonyesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Yonathani ana mwana, ambaye ni mlemavu wa miguu.”
\p
\v 4 Mfalme akamwambia, “Yupo wapi?” Siba akamjibu mfalme, “Tazama, yupo katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.”
\p
\v 5 Ndipo mfalme Daudi akatuma watu na kumtoa katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.
\p
\v 6 Hivyo Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, akaja kwa Daudi naye akainama uso wake hadi katika sakafu kwa kumheshimu Daudi. Daudi akasema, “Mefiboshethi.” Naye akajibu, “Angalia, mimi ni mtumishi wako!”
\p
\v 7 Daudi akamwambia, “Usiogope, maana hakika nitakufadhili kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula katika meza yangu daima.”
\p
\v 8 Mefiboshethi akainama na kusema, “Mtumishi wako ni nani, hata ukamwangalia kwa fadhili mbwa mfu kama nilivyo?”
\p
\v 9 Kisha mfalme akamwita Siba, mtumishi wa Sauli, na kumwambia, “Yote yaliyo ya Sauli na familia yake nimempa mjukuu wa bwana wako.
\v 10 Wewe, wanao, na watumishi wako mtalima mashamba kwa ajili yake nanyi mtavuna mazao ili kwamba mjukuu wa bwana wako apate chakula. Kwa maana Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula katika meza yangu daima.” Basi Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.
\p
\v 11 Kisha Siba akamwambia mfalme, “Mtumishi wako atafanya yote ambayo bwana wangu mfalme amemwamuru mtumishi wake.” Mfalme akaongeza kusema, “Kwa Mefiboshethi yeye atakula katika meza yangu, kama mmojawapo ya wana wa mfalme.”
\p
\v 12 Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo jina lake Mika. Na wote waliokuwa wanaishi katika nyumba ya Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi.
\v 13 Hivyo Mefiboshethi akaishi Yerusalemu, naye akala chakula cha daima katika meza ya mfalme, japokuwa alikuwa mlemavu wa miguu yote.
\c 10
\cl Sura 10
\p
\v 1 Ikawa baadaye, mfalme wa watu wa Amoni akafa, na Hanuni mwanaye akawa mfalme mahali pake.
\v 2 Daudi akasema, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa kuwa baba yake alinitendea wema.” Hivyo Daudi akatuma watumishi wake kumfariji Hanuni kwa habari ya baba yake. Watumishi wake wakaingia katika nchi ya watu wa Amoni.
\v 3 Lakini viongozi wa watu wa Amoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “Je, unadhani kwa hakika Daudi anamheshimu baba yako hata ametuma watu kukutia moyo? Daudi hajawatuma watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, kuupeleleza, ili kuuangamiza?
\v 4 Hivyo Hanuni akawachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia mavazi yao hadi kwenye matako, naye akawaacha waende zao.
\p
\v 5 Daudi alipoelezwa kuhusu hili, akatuma watu kwenda kuwalaki, kwa kuwa walikuwa wamefedheheshwa sana. Mfalme akawaambia, “Kaeni Yeriko mpaka ndevu zenu zitakapoota, ndipo mrudi.”
\p
\v 6 Watu wa Amoni walipoona kwamba wamenuka kwa Daudi, wakatuma wajumbe na kuwaajiri Washami wa Bethi Rehobu na Soba, askari 20,000 waendao kwa mguu, na mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na watu wa Tobu 12,000.
\p
\v 7 Daudi aliposikia, akamtuma Yoabu na jeshi lote la askari.
\v 8 Waamoni wakatoka na wakafanya mistari ya vita katika maingilio ya lango la mji wao, wakati Washami wa Soba na wale wa Rehobu, na watu wa Tobu na Maaka, wakasimama peke yao uwandani.
\p
\v 9 Yoabu alipoona mistari ya vita ikimkabili pote mbele na nyuma, alichagua baadhi ya waisraeli wajuao kupigana vizuri na akawapanga dhidi ya Washami.
\v 10 Na sehemu iliyosalia ya jeshi, akawaweka chini ya Abishai nduguye, naye akawaweka katika mistari ya vita dhidi ya jeshi la Amoni.
\v 11 Yoabu akasema, “Ikiwa Washami watakuwa na nguvu zaidi juu yangu, kisha wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini ikiwa jeshi la Amoni litakuwa na nguvu zaidi juu yako, nitakuja kukuokoa.
\v 12 Iweni na nguvu, nasi tujionyeshe kuwa wenye nguvu kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu, kwa maana Yahwe atatenda yapendezayo kwa ajili ya kusudi lake.
\p
\v 13 Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasonga mbele katika vita dhidi ya Washami, waliolazimika kukimbia mbele ya jeshi la Israeli.
\v 14 Jeshi la Amoni lilipoona kwamba Washami wamekimbia, nao pia wakakimbia kutoka kwa Abishai wakarudi ndani ya mji. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na akarejea Yerusalemu.
\p
\v 15 Washami walipoona kwamba wameshindwa na Israeli, walijikusanya pamoja tena.
\v 16 Kisha Hadareza akatuma kuleta vikosi vya Washami ng'ambo ya Mto Frati. Wakaja Helamu pamoja na Shobaki, mkuu wa jeshi la Hadareza juu yao.
\p
\v 17 Daudi alipoambiwa, aliwakusanya Israeli wote pamoja, akavuka Yordani, na akafika Helamu. Washami wakajipanga katika mistari ya vita dhidi ya Daudi na wakapigana naye.
\v 18 Washami wakakimbia mbele ya Israeli. Daudi akaua askari mia saba wa magari na askari wa farasi elfu arobaini. Shobaki mkuu wa jeshi lao alijeruhiwa na akafa huko.
\v 19 Wafalme wote waliokuwa watumishi wa Hadareza walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Israeli na wakawa watumishi wao. Hivyo washami wakaogopa kuwasaidia watu wa Amoni tena.
\c 11
\cl Sura 11
\p
\v 1 Ikawa wakati wa majira ya kipupwe, wakati ambapo kwa kawaida wafalme huenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, mtumishi wake, na jeshi lote la Israeli. Wakaliaribu jeshi la Amoni na kuuhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu.
\p
\v 2 Hivyo ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi akaamka kutoka kitandani na akatembea katika dari la kasri. Akiwa pale akamwona mwanamke aliyekuwa akioga, mwanamke yule alikuwa mzuri sana wa kupendeza macho.
\v 3 Hivyo Daudi akatuma na kuuliza watu waliomfahamu yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, “Je huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, naye si mke wa Uria mhiti?
\p
\v 4 Daudi akatuma wajumbe nao wakamchukua; akaja kwake, na akalala naye (kwani ndio alikuwa amejitakasa kutoka uchafu wake). Kisha akarudi nyumbani kwake.
\v 5 Mwanamke akawa mjamzito, naye akatuma na kumwambia Daudi; akasema, “Mimi ni mjamzito.”
\p
\v 6 Kisha Daudi akatuma watu kwa Yoabu kusema, “Umtume kwangu Uria mhiti.” Hivyo Yoabu akamtuma Uria kwa Daudi.
\v 7 Uria alipofika, Daudi akamuuliza hali ya Yoabu. Jinsi jeshi lilivyokuwa likiendelea, na jinsi vita vilivyokuwa vinaendelea.
\v 8 Daudi akamwambia Uria, “Shuka nyumbani kwako, unawe miguu yako.” Hivyo Uria akaondoka katika kasri la mfalme, mfalme akamtumia zawadi kwa Uria alipoondoka.
\v 9 Lakini Uria akalala pamoja na watumishi wa bwana wake katika lango la kasri, wala hakushuka nyumbani kwake.
\p
\v 10 Daudi alipoambiwa, “Uria hakushuka nyumbani kwake,” akamwambia Uria, “Je haukutoka safarini? Kwa nini haukushuka nyumbani kwako?”
\p
\v 11 Uria akamjibu Daudi, “Sanduku, na Israeli na Yuda wamo kwenye mahema, na Yoabu na watumishi wa bwana wangu wamepiga hema uwandani. Jinsi gani basi mimi naweza kwenda nyumbani kwangu kula kunywa na kulala na mke wangu? Kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.”
\p
\v 12 Hivyo Daudi akamwambia Uria, “Ukae leo pia, kesho nitakuacha uende.” Kwa hiyo uria akakaa Yerusalemu siku hiyo na iliyofuata.
\v 13 Daudi alipomwita, alikula na kunywa pamoja naye, Daudi akamfanya alewe. Wakati wa jioni Uria akaenda kulala kitandani pake pamoja na watumishi wa bwana wake; hakushuka nyumbani kwake.
\p
\v 14 Hivyo asubuhi Daudi akamwandikia Yoabu barua, naye akaituma kwa mkono wa Uria.
\v 15 Ndani ya barua Daudi aliandika hivi, “Muweke Uria mbele ya vita vikali sana, na kisha, mmwache, ili apigwe na afe.”
\p
\v 16 Hivyo Yoabu alipoona mji ukizingirwa, alimuweka Uria katika sehemu aliyojua askari adui wenye nguvu wangekuwa wakipigana.
\v 17 Wakati watu wa mji walipotoka na kupigana dhidi ya jeshi la Yoabu, baadhi ya askari wa Daudi wakaanguka, na Uria Mhiti pia akauwawa.
\p
\v 18 Wakati Yoabu alipotuma neno kwa mfalme kuhusu hali ya vita,
\v 19 alimwagiza mjumbe, kusema, “Utakapomaliza kumwambia mfalme kuhusu hali ya vita,
\v 20 yawezekana mfalme akakasirika, naye akakwambia, Kwa nini mlipigana na mji kwa karibu hivyo, hamkujua kwamba wangeweza kushambulia kutokea ukutani?
\v 21 Ni nani aliyemuua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi? Siye mwanamke aliyerusha jiwe la kusagia juu yake kutoka ukutani, hata akafa huko Thebesi? Kwanini basi mliukaribia ukuta jinsi hiyo? Nawe umjibu, Uria mtumishi wako amekufa pia.’”
\p
\v 22 Hivyo mjumbe akaondoka na kwenda kwa Daudi akamwambia kila jambo ambalo Yoabu alimtuma kusema.
\v 23 Na mjumbe akamwambia Daudi, “Mwanzoni adui walikuwa na nguvu kuliko sisi; walitukabili uwandani, lakini tukawarudisha nyuma kwenye maingilio ya lango.
\v 24 Na wapiga mishale wao wakawarushia watumishi wako kutoka ukutani, na baadhi ya watumishi wa mfalme wameuawa, na mtumishi wako Uria mhiti pia ameuawa.”
\p
\v 25 Kisha Daudi akamwambia mjumbe, “Mwambie hivi Yoabu, Usiruhusu jambo hili likuhuzunishe, kwa maana upanga huangamiza huyu kama uangamizavyo na mwingine. Vifanye vita vyako kuwa vyenye nguvu zaidi dhidi ya mji, na uuteke. Mtie moyo Yoabu.”
\p
\v 26 Hivyo mke Uria aliposikia kwamba mme wake amekufa, akaomboleza sana kwa ajili yake.
\v 27 Huzuni yake ilipoisha, Daudi akatuma na kumchukua kwake katika kasri lake, naye akawa mkewe na akamzalia mwana. Lakini alichokifanya Daudi hakikumpendeza Yahwe.
\c 12
\cl Sura 12
\p
\v 1 Kisha Yahwe akamtuma Nathani kwa Daudi. Akaja kwake na kusema, “Kulikuwa na watu wawili katika mji. Mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini.
\v 2 Yule tajiri alikuwa na kundi la ng'ombe na kondoo wengi sana,
\v 3 lakini maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwanakondoo, aliyekuwa amemnunua na kumlisha na kumlea. Akakua pamoja naye na pamoja na watoto wake. Yule mwanakondoo hata alikula naye na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye akalala katika mikono yake na alikuwa kama binti kwake.
\p
\v 4 Siku moja mgeni akaja kwa tajiri, lakini tajiri hakuwa tayari kuchukua mnyama kutoka katika kundi lake la ng'ombe au kundi la kondoo ili kumuandalia chakula. Badala yake alichukua mwanakondoo wa maskini na akampika kwa ajili ya mgeni wake.”
\p
\v 5 Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, “Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa.
\v 6 Ni lazima alipe mwanakondoo mara nne zaidi kwa ajili ya kile alichokifanya, na kwa sababu hakuwa na huruma kwa mtu maskini.”
\p
\v 7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiye yule mtu! Yahweh, Mungu wa Israeli, asema, Nilikutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, na nilikuokoa kutoka katika mkono wa Sauli.
\v 8 Nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake zake mikononi mwako. Nilikupa pia nyumba ya Israeli na Yuda. Na ikiwa hayo yalikuwa kidogo zaidi kwako, ningeweza kukuongezea mengine zaidi.
\v 9 Hivyo basi kwa nini umedharau maagizo ya Yahwe, hata ukafanya yaliyo maovu mbele zake? Umeua Uria Mhiti kwa upanga na umechukua mkewe kuwa mke wako. Uliua kwa upanga wa jeshi la Amoni.
\v 10 Hivyo basi upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria mhiti kuwa mke wako.
\v 11 Yahwe asema, Tazama, nitaleta maafa dhidi yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe. Nitachukua wake zako, mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako wakati wa mchana.
\v 12 Kwa maana wewe ulitenda dhambi hii sirini, lakini mimi nitatenda jambo hili wakati wa mchana mbele za Israeli wote.’”
\p
\v 13 Ndipo Daudi alipomwambia Nathani, “Nimemtenda dhambi Yahwe.” Nathani akamjibu Daudi, “Yahwe naye ameiachilia dhambi yako. Hautauliwa.
\v 14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umemdharau Yahwe, mtoto aliyezaliwa kwako hakika atakufa.”
\p
\v 15 Kisha Nathani akaondoka na kwenda kwake. Yahwe akampiga mtoto ambaye mke wa Uria alimzaa kwa Daudi, naye akaugua sana.
\v 16 Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu.
\v 17 Wazee wa nyumba yake wakainuka na kusimama kando yake, ili wamwinue kutoka sakafuni. Lakini hakuinuka, na hakula pamoja nao.
\p
\v 18 Ikawa siku ya saba mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kwamba mtoto amekufa, kwa maana walisema, “Tazama, wakati mtoto alipokuwa hai tuliongea naye, lakini hakuisikiliza sauti yetu. Atakuwaje ikiwa tutamwambia kwamba kijana amekufa?!”
\p
\v 19 Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, “Je mtoto amekufa?” Wakajibu, “Amekufa.”
\p
\v 20 Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudi katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala.
\p
\v 21 Ndipo watumishi wake walipomwambia, “Kwa nini umefanya jambo hili? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto wakati alipokuwa hai, lakini mtoto alipokufa, ukainuka na kula.”
\p
\v 22 Daudi akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa hai nilifunga na kulia. Nilisema, “Ni nani ajuaye kwamba Yahwe angeweza kunihurumia mtoto akaishi au sivyo?
\v 23 Lakini sasa amekufa, hivyo nifungie nini? Je naweza kumrudisha tena? Nitakwenda kwake, lakini yeye hawezi kunirudia.”
\p
\v 24 Daudi akamfariji Bethsheba mkewe, akaingia kwake, na akalala naye. Baadaye akazaa mtoto wa kiume, naye akaitwa Selemani. Yahwe akampenda
\v 25 naye akatuma neno kupitia nabii Nathani kumwita Yedidia, kwa sababu Yahwe alimpenda.
\p
\v 26 Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake.
\v 27 Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, “Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji.
\v 28 Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu.”
\p
\v 29 Hivyo Daudi akalikusanya jeshi lote na kwenda Raba; akapigana nao na kuuteka.
\v 30 Daudi akachukua taji ya dhahabu kutoka katika kichwa cha mfalme wao iliyokuwa na uzito wa talanta, na ilikuwa na jiwe la thamani ndani yake. Taji ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Kisha akachukua nyara za mji kwa wingi.
\v 31 Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu.
\c 13
\cl Sura 13
\p
\v 1 Ikawa baada ya hayo kwamba Amnoni mwana wa Daudi, akamtamani sana Tamari dada yake wa kambo aliyekuwa mzuri, alikuwa tumbo moja na Absalomu, mwana mwingine wa Daudi.
\v 2 Amnoni akasononeka sana kiasi cha kuugua kwa ajili ya Tamari dada yake. Tamari alikuwa bikra, na hivyo ilionekana haiwezekani Amnoni kufanya neno lolote kwake.
\p
\v 3 Lakini Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi.
\p
\v 4 Yehonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. Akamwambia Amnoni, “Kwa nini, mwana wa mfalme, unadhoofika kila siku? Kwa nini huniambii?” Ndipo Amnoni akamjibu, “Nampenda Tamari, dada yake Absalomu ndugu yangu.”
\p
\v 5 Ndipo Yehonadabu akamwambia, “Lala kitandani mwako na ujifanye kuwa mgonjwa. Wakati baba yako atakapo kuja kukuona, mwambie, Tafadhali mtume dada yangu Tamari aandae chakula mbele yangu, ili kwamba nikione na kula kutoka mkononi mwake?’”
\p
\v 6 Hivyo Amnoni akalala na kujifanya kuwa mgonjwa. Mfalme alipokuja kumwona, Amnoni akamwambia mfalme, “Tafadhari mtume Tamari dada yangu aandae chakula kwa ajili ya ugonjwa wangu mbele yangu ili kwamba nikile kutoka mkononi mwake.”
\p
\v 7 Ndipo Daudi katika kasri lake akatuma neno kwa Tamari, kusema, “Nenda katika nyumba ya nduguyo Amnoni na umwandalie chakula.”
\v 8 Hivyo Tamari akaenda katika nyumba ya Amnoni nduguye alipokuwa amelala. Akachukua donge na kulifinyanga na kuandaa mkate mbele zake, kisha akauoka.
\v 9 Akachukua kikaangio na kumpa mkate, lakini akakataa kula. Kisha Amnoni akawaambia waliokuwepo, “Kila mtu na aondoke mbali nami.” Hivyo kila mmoja akaondoka.
\p
\v 10 Amnoni akamwambia Tamari, “Lete chakula chumbani kwangu nikile katika mkono wako.” Tamari akachukua mkate aliokuwa ameuandaa, na kuuleta katika chumba cha Amnoni kaka yake.
\v 11 Alipoleta chakula kwake, Amnoni akamshikilia na kumwambia, “Njoo, ulale nami, dada yangu.”
\p
\v 12 Yeye akamjibu, “Hapana, kaka yangu, usinilazimishe, kwani hakuna jambo kama hili linapaswa kufanyika katika Israeli. Usifanye jambo la aibu kiasi hiki!
\v 13 Nitakwenda wapi ili nijiepushe na aibu ambayo jambo hili litaileta juu ya maisha yangu? Na tendo hili litakuonyesha kuwa mpumbavu usiye na aibu katika Israeli yote. Tafadhali, ninakuomba uongee na mfalme. Yeye atakuruhusu unioe.”
\v 14 Lakini Amnoni hakuweza kumsikiliza. Kwa kuwa alikuwa zaidi akamkamata na akalala naye.
\p
\v 15 Kisha Amnoni akamchukia Tamari kwa chuki kuu. Akamchukia zaidi ya jinsi alivyokuwa amemtamani. Amnoni akamwambia, “Inuka na uondoke.”
\p
\v 16 Lakini yeye akamjibu, “Hapana! Kwa maana uovu wa kunifanya niondoke ni mmbaya zaidi ya kile ulichonitenda!” Lakini Amnoni hakumsikiliza.
\p
\v 17 Badala yake, akamwita mtumishi wake na akasema, “Mwondoe mwanamke huyu mbele yangu, na uufunge mlango nyuma yake.”
\v 18 Hivyo mtumishi wake akamtoa na kufunga mlango. Tamari alikuwa amevaa vazi lililopambwa kwa uzuri kwani ndivyo binti za wafalme waliobikra walikuwa wakivaa.
\v 19 Tamari akaweka majivu juu ya kichwa chake na akairarua vazi lake lililopambwa kwa uzuri. Akaweka mikono kichwani mwake na akaenda zake huku akilia kwa sauti.
\p
\v 20 Absalomu, kaka yake, akamwambia, “Amnoni, kaka yako, amekuwa nawe? Lakini sasa nyamaza, dada yangu. Yeye ni kaka yako. Usiliweke hili moyoni.” Hivyo Tamari akakaa peke yake katika nyumba ya Absalomu kaka yake.
\p
\v 21 Mfalme Daudi aliposikia haya yote, alikasirika sana.
\v 22 Absalomu hakusema chochote kwa Amnoni, kwa maana Absalomu alimchukia kwa kile alichokifanya, kumdhalilisha Tamari, dada yake.
\p
\v 23 Ikawa baada ya miaka miwili mizima Absalomu akawa na wakatao kondoo manyoya wakifanya kazi huko Baali Hazori, ulioko karibu na Efraim, naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme kufika huko.
\v 24 Absalomu akamwendea mfalme na kusema, “Tazama sasa, mtumishi wako anao wakatao kondoo manyoya. Tafadhali, naomba mfalme na watumishi wake waende nami, mtumishi wako.”
\p
\v 25 Mfalme akamjibu Absalomu, “Hapana mwanangu, tusiende sisi sote kwani tutakuwa mzigo kwako.” Absalomu akamsihi mfalme, lakini yeye asikubali kwenda, ila alimbariki Absalomu.
\p
\v 26 Kisha Absalomu akasema, “Kama sivyo, basi tafadhali mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi.” Mfalme akamuliza, “Kwa nini Amnoni aende nanyi?”
\p
\v 27 Absalomu akamsihi Daudi, hivyo akamruhusu Amnoni na wana wengine wa mfalme kwenda naye.
\p
\v 28 Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, “Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, msiogope muueni. Je, siyo mimi niliyewaamuru? Muwe jasiri na hodari.”
\v 29 Hivyo watumishi wa Absalomu wakamtendea Amnoni kama walivyoamriwa. Kisha wana wote wa mfalme wakainuka na kila mmoja akapanda nyumbu wake akakimbia.
\p
\v 30 Hata ikawa wakati wakiwa njiani habari zikafika kwa Daudi kusema, “Absalomu ameua wana wote wa mfalme na hakuna hata mmoja aliyesalia.”
\v 31 Kisha mfalme akainuka na kurarua mavazi yake na kujilaza juu ya sakafu; watumishi wake wote wakasimama karibu naye mavazi yao yameraruriwa.
\p
\v 32 Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi, akajibu na kusema, “Bwana wangu asidhani kuwa vijana wote ambao ni wana wa mfalme wameuawa, kwa maana ni Amnoni pekee ndiye aliyeuawa. Absalomu alilipanga jambo hili tangu siku ile Amnoni alivyomdhulumu Tamari, dada yake.
\v 33 Kwa hiyo basi, bwana wangu mfalme asiiweke taarifa hii moyoni, kudhani kwamba wana wote wa mfalme wameuawa, kwani aliyeuawa ni Amnoni peke yake.”
\p
\v 34 Absalomu akakimbia. Mtumishi aliyekuwa akiangalia akainua macho yake na kuona watu wengi wakija njiani kando ya kilima upande wake wa magharibi.
\v 35 Kisha Yehonadabu akamwambia mfalme, “Tazama, wana wa mfalme wanakuja, kama mtumishi wako alivyosema.”
\p
\v 36 Ikawa mara alipomaliza kusema wana wa mfalme wakafika, wakainua sauti zao na kulia. Na mfalme pamoja na watumishi wake wote pia wakalia kwa uchungu.
\p
\v 37 Lakini Absalomu akakimbia na kwenda kwa Talmai mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Mfalme akaomboleza kila siku kwa ajili ya mwanaye.
\v 38 Hivyo Absalomu akakimbia na kwenda Geshuri na akakaa huko kwa miaka mitatu.
\v 39 Moyo wa mfalme Daudi ukatamani kwenda kumwona Absalomu, kwa maana alikuwa amefarijika kwa habari ya kifo cha Amnoni.
\c 14
\cl Sura 14
\p
\v 1 Yoabu mwana wa Seruya akatambua kwamba moyo wa mfalme ulitamani kumwona Absalomu.
\v 2 Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwerevu. Akamwambia, “Tafadhali, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa.
\v 3 Kisha ingia kwa mfalme na umwambie maneno nitakayokueleza.” Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme.
\p
\v 4 Wakati mwanamke kutoka Tekoa alipoongea na mfalme, aliinamisha uso wake chini na kusema,
\p
\v 5 “Mfalme, nisaidie.” Mfalme akamwambia, “Shida yako ni nini?” Akajibu, Ukweli ni kwamba mimi ni mjane, mme wangu alikufa.
\v 6 Mimi, mtumishi wako, nilikuwa na wana wawili, wakagombana shambani, na hakukuwa na wa kuwaachanisha. Mmoja wao akampiga mwenziwe na kumwua.
\v 7 Na sasa ukoo wote umeinuka juu ya mtumishi wako, wanasema, Mtoe aliyempiga nduguye, ili tumuue kulipa uhai wa nduguye aliyeuawa. Na hivyo watamwangamiza mrithi. Hivyo watalizima kaa liwakalo nililobakisha, hata kumwondolea mme wangu jina na uzao juu ya uso wa nchi.”
\p
\v 8 Hivyo mfalme akamwambia mwanamke, “Nenda nyumbani kwako, nami nitaagiza jambo la kukufanyia.”
\p
\v 9 Mwanamke kutoka Tekoa akamjibu mfalme, “Bwana wangu mfalme, hatia na iwe juu yangu na juu ya familia ya baba yangu. Mfalme na kiti chake cha enzi hawana hatia.”
\p
\v 10 Mfalme akasema, “Yeyote atakayekwambia neno umlete kwangu, naye hatakugusa tena.”
\p
\v 11 Kisha mwanamke akasema, “Tafadhali mfalme amkumbuke Yahwe Mungu wake, ili kwamba mlipa kisasi cha damu asiharibu zaidi, ili kwamba wasimwangamize mwanangu.” Mfalme akajibu, “Kama Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utaanguka chini.”
\v 12 Kisha mwanamke akasema, “Tafadhali acha mtumishi wako anene neno moja zaidi kwa bwana wangu mfalme.” Akasema, “Sema.”
\p
\v 13 Hivyo mwanamke akasema, “Kwa nini basi umetenda kwa hila dhidi ya watu wa Mungu? Maana kwa kusema hivi, mfalme ni kama mtu mwenye hatia, kwa kuwa mfalme hajamrudisha tena mwanaye aliyeondoka.
\v 14 Kwa maana sisi sote tutakufa, kwa kuwa tu kama maji yamwagwayo juu ya ardhi na kwamba hayawezi kukusanywa tena. Lakini Mungu hatachukua uhai; badala yake, utafuta njia kwa walio mbali kurejeshwa.
\p
\v 15 Sasa basi, nimesema jambo hili kwa bwana wangu mfalme, kwa sababu watu wamenitisha. Hivyo mtumishi wako akajinenea nafsini mwake, Sasa nitaongea na mfalme. Huenda mfalme akampa mtumishi wake haja yake.
\v 16 Kwa maana mfalme atanisikiliza, ili kwamba kumtoa mtumishi wake katika mikono ya mtu ambaye angeniangamiza mimi na mwanangu pamoja, tutoke katika urithi wa Mungu.
\p
\v 17 Kisha mtumishi wako akaomba, Yahwe, tafadhali ruhusu neno la bwana wangu mfalme linipe msaada, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu kwa kutofautisha wema na ubaya. Yahwe, Mungu na awe pamoja nawe.”
\p
\v 18 Ndipo mfalme akajibu na kumwambia yule mwanamke, “Tafadhali usinifiche neno lolote nikuulizalo.” Mwanamke akajibu, “Basi bwana wangu mfalme na aseme sasa.”
\p
\v 19 Mfalme akasema, “Je siyo mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu na kusema, “Kama uishivyo bwana wangu mfalme, hakuna awezaye kuelekea mkono wa kulia wala wa kushoto kwa yale bwana wangu mfalme aliyosema. Ni mtumishi wako Yoabu aliyeniambia na kuniagiza kusema kile mtumishi wako alichokisema.
\v 20 Mtumishi wako Yoabu amefanya hivi ili kubadilisha hali ya kile kinachotendeka. Bwana wangu ni mwenye akili kama hekima ya malaika wa Mungu, ajuaye yote yatendekayo ndani ya nchi.”
\p
\v 21 Hivyo mfalme akamwambia Yoabu, “Tazama, nitatenda jambo hili. Nenda na umrudishe huyo kijana Absalomu.”
\p
\v 22 Hivyo Yoabu akainamisha uso wake chini juu ya ardhi katika heshima na shukrani kwa mfalme. Yoabu akasema, “Mtumishi wako amejua kwamba amepata neema mbele zako, bwana wangu, mfalme, kwa vile mfalme amempa mtumishi wake haja ya moyo wake.” Ycv
\p
\v 23 Hivyo Yoabu akainuka na kwenda Geshuri, akamrejesha Absalomu Yerusalemu tena.
\v 24 Mfalme akasema, “Na arudi nyumbani kwake, lakini hasinione uso wangu.” Hivyo Absalomu akarudi katika nyumba yake mwenyewe, na hakuweza kuuona uso wa mfalme.
\p
\v 25 Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa urembo wake kama Absalomu. Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote.
\v 26 Alipokata nywele za kichwa chake mwishoni mwa kila mwaka, kwa sababu zilikuwa nzito juu yake, alipima nywele zake zaidi ya shekeli mia mbili, kwa kiwango cha kipimo cha mfalme.
\v 27 Kwake Absalomu walizaliwa wana watatu na binti mmoja, jina lake Tamari. Alikuwa mwanamke mzuri.
\p
\v 28 Absalomu akaishi Yerusalem miaka miwili pasipo kuona uso wa mfalme.
\v 29 Kisha Absalomu akatuma neno kwa Yoabu ili ampeleke kwa mfalme, lakini Yoabu hakuenda kwake. Hivyo Absalomu akatuma neno mara ya pili, lakini Yoabu hakuja bado.
\p
\v 30 Hivyo Absalomu akawaambia watumishi wake, “Tazameni, shamba la Yoabu lipo karibu na langu, naye ana shayiri kule. Nendeni mkalichome moto.” Hivyo watumishi wa Absalomu wakalichoma moto lile shamba.
\p
\v 31 Kisha Yoabu akainuka na kwenda nyumbani kwa Absalomu akamwambia, “Kwa nini watumishi wako wamelichoma moto shamba langu?”
\v 32 Absalomu akamjibu Yoabu, “Tazama nilituma neno kwako kusema, Njoo ili nikutume kwa mfalme kusema, kwa nini nilikuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningesalia huko. Kwa hivyo sasa niache niuone uso wa mfalme na kama nina hatia basi na aniue.”
\v 33 Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi ardhini mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.
\c 15
\cl Sura 15
\p
\v 1 Ikawa baada ya haya Absalomu akaandaa gari la farasi na farasi kwa ajili yake pamoja na watu hamsini wa kwenda mbele zake.
\v 2 Absalomu alikuwa akiamka mapema na kusimama kando ya njia iliyoelekea katika lango la mji. Mtu yeyote aliyekuwa na shauri la kuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu, Absalomu alimwita na kumuuliza, “Unatoka mji upi?” Na mtu yule hujibu, Mtumishi wako anatoka mojawapo ya kabila za Israeli.”
\v 3 Hivyo Absalomu angemwambia, “Tazama, shitaka lako ni jema na la haki, lakini hakuna aliyepewa mamlaka na mfalme kusikiliza shitaka lako.”
\v 4 Tena Absalomu huongeza, “Natamani kwamba ningefanywa mwamuzi ndani ya nchi ili kwamba kila mtu aliye na shitaka angeweza kuja kwangu nami ningempa haki.”
\p
\v 5 Hivyo ikawa kila mtu aliyekuja kumheshimu Absalomu yeye angenyosha mkono na kumshika na kumbusu.
\v 6 Absalomu alifanya hivi kwa Israeli wote waliokuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu. Hivyo Absalomu akaipotosha mioyo ya watu wa Israeli.
\p
\v 7 Ikawa mwishoni mwa miaka minne Absalomu akamwambia mfalme, “Tafadhali niruhusu niende ili nitimize nadhili niliyoiweka kwa Yahwe huko Hebroni.
\v 8 Kwa maana mtumishi wako aliweka nadhili alipokuwako Geshuri katika Shamu akisema, Ikiwa Yahwe kweli atanirejesha Yerusalemu, ndipo nitamwabudu yeye.”
\p
\v 9 Hivyo mfalme akamwambia, “Nenda kwa amani.” Absalomu akainuka na kwenda Hebroni.
\p
\v 10 Kisha Absalomu akatuma wapelelezi katika jamaa zote za Israeli, kusema, “Mara msikiapo sauti ya tarumbeta semeni, Absalomu anatawala katika Hebroni.”
\v 11 Watu mia mbili waliokuwa wamealikwa kutoka Yerusalemu wakaenda na Absalomu. Wakaenda katika ujinga wao bila kujua Absalomu alichokipanga.
\v 12 Wakati Absalomu akitoa dhabihu, alituma watu kwa Ahithofeli katika mji wake huko Gilo. Yeye alikuwa mshauri wa Daudi. Fitina za Absalomu zikawa na nguvu kwa kuwa watu waliomfuata waliendelea kuongezeka.
\p
\v 13 Mjumbe akaja kwa Daudi na kusema, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”
\p
\v 14 Hivyo Daudi akawaambia watumishi wake waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Haya na tuinuke na kukimbia kwani hakuna hata mmoja atakayeokoka kwa Absalomu. Jiandaeni kuondoka mara moja asije akatupata mara hata akasababisha madhara juu yetu na kuushambulia mji kwa makali ya upanga.”
\p
\v 15 Watumishi wa mfalme wakamwambia, “Tazama, watumishi wako wapo tiyari kufanya lolote bwana wetu mfalme atakaloamua.
\p
\v 16 Mfalme akaondoka na familia yake yote pamoja naye, lakini mfalme akawaacha wanawake kumi waliokuwa masuria wa mfalme ili walitunze kasri.
\v 17 Baada ya mfalme kwenda na watu wote pamoja naye, wakasimama katika nyumba ya mwisho.
\v 18 Watumishi wako wote wakaenda pamoja naye na mbele yake wakaenda Wakerethi na Wapelethi, na Wagiti 600 wote waliokuwa wamemfuata kutoka Gathi.
\p
\v 19 Kisha mfalme akamwambia Itai Mgiti, “Kwa nini wewe pia uende nasi? Rudi na ukae na mfalme Absalomu kwa kuwa wewe ni mgeni tena mfungwa. Rudi mahali pako mwenyewe.
\v 20 Kwani ni jana tu umeondoka, kwa nini nikufanye uzunguke nasi popote? Hata sijui niendako. Hivyo rudi pamoja na wenzako. Utiifu na uaminifu viambatane nawe.”
\p
\v 21 Lakini Itai akamjibu mfalme na kusema, “Kama Yahwe aishivyo na kama bwana wangu mfalme aishivyo, kwa hakika mahali popote bwana wangu mfalme aendako, mtumishi wako pia ndipo atakapokwenda, kwamba ni maisha au kifo.”
\p
\v 22 Hivyo Daudi akamwambia Itai, haya tangulia uende pamoja nasi.” Hivyo Itai Mgiti akaenda pamoja na mfalme, pamoja na watu wake wote na familia zao zote.
\p
\v 23 Nchi yote ikalia kwa sauti kama watu walivyokuwa wakivuka Bonde la Kidroni, na pia mfalme naye akivuka. Watu wote wakasafiri kuelekea nyikani.
\p
\v 24 Walikuwepo pia Sadoki pamoja na Walawi wote wamebeba sanduku la Mungu la agano. Wakaliweka sanduku la Mungu chini na kisha Abiathari akaungana nao. Wakasubiri mpaka watu wote wakapita kutoka mjini.
\p
\v 25 Mfalme akamwambia Sadoki, “Ulirudishe sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitaona neema machoni pa Yahwe atanirudisha na kunionyesha tena sanduku na mahali likaapo.
\v 26 Lakini ikiwa atasema, Sipendezwi nawe, tazama mimi nipo hapa, na anitendee yaliyo mema machoni pake.”
\p
\v 27 Pia mfalme akamwambia Sadoki kuhani, “Je wewe siyo mwonaji? Rudi mjini kwa amani na wanao wawili, Ahimaazi mwanao na Yonathani mwana wa Abiathari.
\v 28 Tazama nitasubiri katika vivuko vya nyikani mpaka nitakapo pata neno kutoka kwenu kunipasha habari.”
\v 29 Hivyo Sadoki na Abiathari wakalirudisha sanduku la Mungu Yerusalemu nao wakakaa humo.
\p
\v 30 Lakini Daudi akaenda bila viatu huku akilia hata Mlima wa Mizeituni, naye alikuwa amefunika kichwa chake. Kila mtu miongoni mwao waliokuwa pamoja naye akafunika kichwa chake, nao wakaenda huku wakilia.
\v 31 Mtu mmoja akamwambia Daudi akisema, “Ahithofeli ni miongoni mwa wafitini walio pamoja na Absalomu.” Hivyo Daudi akaomba, “Ee Yahwe, tafadhali badili ushauri wa Ahithofeli kuwa upumbavu.”
\p
\v 32 Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake likiwa limeraruliwa na mavumbi kichwani pake.
\v 33 Daudi akamwambia, “Ikiwa utaenda nami utakuwa mzigo kwangu.
\v 34 Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wa mfalme kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako, ndipo utayageuza mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
\v 35 Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Hivyo chochote ukisikiacho katika kasri, uwaambie Sadoki na Abiathari makuhani.
\v 36 Tazama wanao pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani mwana wa Abiathari. Mniletee habari juu ya kila mnachokisikia.”
\p
\v 37 Hivyo Hushai, rafiki wa Daudi, akaja mjini wakati Absalomu anafika na kuingia Yerusalemu.
\c 16
\cl Sura 16
\p
\v 1 Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo.
\p
\v 2 Mfalme akamuuliza Siba, “Kwa nini umeleta hivi vitu?” Siba akajibu, “Punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili ya kunywa kwa yeyote atakayezimia nyikani.”
\p
\v 3 Mfalme akauliza, “Na mjukuu wa bwana wako yuko wapi?” Siba akamjibu mfalme, “Tazama, yeye amesalia Yerusalemu kwa maana alisema, Leo nyumba ya Israeli itanirudishia ufalme wa baba yangu.”
\p
\v 4 Kisha mfalme akamwambia Siba, “Tazama, yote yaliyomilikiwa na Mefiboshethi sasa yatakuwa yako.” Siba akajibu, “Nainama kwa unyenyekevu kwako bwana wangu mfalme. Na nipate kibali mbele zako.”
\p
\v 5 Mfalme Daudi alipokaribia Bahurimu, akaja mtu kutoka katika ukoo wa Sauli, jina lake Shimei mwana wa Gera. Kadiri alivyokuwa akitembea alikuwa akilaani.
\v 6 Akamrushia Daudi mawe na maofisa wa mfalme, bila kujali jeshi na walinzi wa mfalme waliokuwa kulia na kushoto mwa mfalme.
\v 7 Shimei akalaani, “Nenda zako, toka hapa, mwovu wewe, mtu wa damu!
\v 8 Yahwe amelipa yote kwa ajili ya damu ya familia ya Sauli, ambaye unatawala badala yake. Yahwe ameweka ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao. Na sasa umeangamia kwa kuwa wewe ni mtu wa damu.”
\p
\v 9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, “Kwa nini mbwa mfu anamlaani bwana wangu mfalme? Tafadhali niache niende nikamwondolee kichwa chake.”
\p
\v 10 Lakini mfalme akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya? Pengine ananilaani kwa kuwa Yahwe amemwambia, Mlaani Daudi. Nani sasa awezaye kumwambia, Kwa nini unamlaani mfalme.”
\p
\v 11 Hivyo Daudi akamwambia Abishai na watumishi wake wote, “Tazameni, mwanangu aliyezaliwa kutoka katika mwili wangu anatafuta uhai wangu. “Si zaidi sana mbenjamini huyu akatamani anguko langu? Mwacheni alaani, kwa maana Yahwe amemwamuru kufanya hivyo.
\v 12 Huenda Yahwe akaangalia taabu iliyonijia, na kunirudishia mema kwa jinsi nilivyolaaniwa leo.”
\v 13 Hivyo Daudi na watu wake wakaendelea njiani wakati Shimei kando yake ubavuni mwa mlima, aliendelea kulaani na kumrushia mavumbi na mawe huku akienda.
\v 14 Kisha mfalme na watu wake wote wakachoka, na akapumzika wakati wa usiku walipopumzika wote.
\p
\v 15 Absalomu na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye wakaja Yerusalemu na Ahithofeli alikuwa pamoja naye.
\v 16 Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, “Mfalme aishi daima! Mfalme aishi daima.”
\p
\v 17 Absalomu akamwambia Hushai, “Je huu ndio utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?”
\p
\v 18 Hushai akamwambia Absalomu, “Hapana! Badala yake, yule ambaye Yahwe, watu hawa na watu wote wa Israeli wamemchagua huyo ndiye nitakaye kuwa upande wake na ndiye nitakaye kaa naye.
\v 19 Kwani ni nani ninayepaswa kumtumikia? Je sipaswi kutumika mbele za mwana wake? Kama nilivyotumika mbele za baba yako ndivyo nitakavyofanya mbele zako”
\p
\v 20 Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako kuhusu tunachopaswa kufanya.”
\p
\v 21 Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Nenda kwa masuria wa baba yako aliowaacha kutunza kasri, na Waisraeli wote watasikia kwamba umekuwa chukizo kwa baba yako. Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu.”
\v 22 Hivyo wakasimamisha hema kwa ajili ya Absalomu juu ya kasiri na, Absalomu akalala na masuria wa baba yake mbele za Israeli wote.
\p
\v 23 Nyakati hizo ushauri aliokuwa akitoa Ahithofeli ulikuwa ni kama mtu anavyosikia kutoka katika kinywa cha Mungu mwenyewe. Hivyo ndivyo jinsi ushauri wa Ahithofeli ulivyoonekana kwa Daudi na Absalomu.
\c 17
\cl Sura 17
\p
\v 1 Kisha Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Niruhusu sasa nichague watu 12,000 nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu.
\v 2 Nitampata kwa ghafla wakati amechoka na dhaifu nami nitamstukiza kwa hofu. Watu waliopamoja naye watakimbia nami nitamshambulia mfalme peke yake.
\v 3 Nitawarejesha watu wote kwako kama bibi harusi ajavyo kwa bwana wake, na watu wote watakuwa katika amani chini yako.”
\v 4 Alichokisema Ahithofeli kikampendeza mfalme na wazee wote wa Israeli.
\p
\v 5 Kisha Absalomu akasema, “Sasa mwiteni pia Hushai Mwarki ili tusikie yeye pia anavyosema.”
\v 6 Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamweleza kile ambacho Ahithofeli alikuwa amesema na kisha akamwuliza Hushai, “Je tufanye alivyosema Ahithofeli? Ikiwa hapana, tueleze kile unachoshauri.”
\p
\v 7 Hivyo Hushai akamwambia Absalomu, “Ushauri aliotoa Ahithofeli siyo mzuri kwa wakati huu.”
\v 8 Hushai akaongeza, “Unamjua baba yako na kwamba watu wake ni mashujaa na kwa sasa wanauchungu, ni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake mwituni. Baba yako ni mtu wa vita; hatalala na jeshi usiku huu.
\v 9 Tazama, kwa wakati huu pengine amejificha katika shimo fulani au mahali pengine. Itakuwa kwamba baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa mwanzoni mwa shambulio hata kila mtu atakayesikia atasema, mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu.
\v 10 Kisha hata askari jasiri zaidi ambao moyo wao ni kama moyo wa simba, wataogopa kwa kuwa Israeli yote inajua kwamba baba yako ni mtu mwenye nguvu na kwamba watu alionao ni wenye nguvu sana.
\p
\v 11 Hivyo ninashauri kwamba Israeli wote wakutanike kwako pamoja kutoka Dani hadi Beersheba, wengi kama mchanga ufuoni mwa bahari na kwamba wewe mwenyewe uende vitani.
\v 12 Kisha tutampata popote atakapokuwa nasi tutamfunika kama umande uangukavyo juu ya nchi. Hatutamwachia hata mmoja aliye hai kati ya watu wake wala yeye mwenyewe.
\v 13 Ikiwa ataingia ndani ya mji kisha Israeli wote tutaleta kamba juu ya mji huo na kuukokotea mtoni, hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia.”
\p
\v 14 Kisha Absalomu na watu wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai Mwarki ni jema kuliko lile la Ahithofeli. Yahwe aliwafanya wakatae shauri jema la Ahithofeli ili kumwangamiza Absalomu.
\p
\v 15 Kisha Hushai akawaambia Sadoki na Abiathari makuhani, “Ahithofeli alimshauri Absalomu na wazee wa Israeli hivi na hivi, lakini mimi nimeshauri vinginevyo.
\v 16 Sasa basi, nendeni haraka na mmpashe habari Daudi kusema, Usipige kambi usiku huu katika vivuko vya Araba, lakini kwa namna yoyote vukeni, tofauti na hapo mfalme atamezwa pamoja na watu wote walio pamoja naye.”
\p
\v 17 Yonathani na Ahimaasi walikuwako katika chemichemi za En Rogeli. Hivyo kijakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapasha habari waliyopaswa kuifahamu, ili kwamba wasihatarishe maisha yao kwa kuonekana wakiingia mjini. Ujumbe ulipofika ndipo walikuwa wanaenda kumpasha habari mfalme Daudi.
\v 18 Lakini kijana mmoja akawaona wakati huo na akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima uani mwake, wakashuka humo.
\v 19 Mke wa mtu huyo akachukua kifuniko na kukikufunika kwenye mlango wa kisima kisha akaanika nafaka juu yake, hivyo hakuna aliyejua kwamba Yonathani na Ahimaasi walikuwa kisimani.
\p
\v 20 Watu wa Absalomu wakaja kwa mwanamke na kumuuliza, “Ahimaasi na Yonathani wako wapi?” Mwanamke akawaambia, “Wamevuka mto.” Hivyo baada ya kuwatafuta bila kuwaona, wakarejea Yerusalemu.
\v 21 Ikawa baada yao kuondoka Yonathani na Ahimaasi wakatoka ndani ya kisima. Wakaenda kumtaarifu mfalme Daudi; wakamwambia, “Inuka na uvuke maji haraka kwa maana Ahithofeli ametoa mashauri haya na haya juu yako.”
\v 22 Kisha Daudi akainuka pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye, nao wakauvuka Yordani. Hata ilipofika alfajiri hakuna hata mmoja aliyesalia kwa kutouvuka Yordani.
\p
\v 23 Ikawa Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, akapanda punda wake na kuondoka. Akaenda nyumbani katika mji wake mwenyewe, akaweka mambo yake katika utaratibu na kisha akajinyonga. Kwa hiyo akafa na kuzikwa katika kaburi la baba yake.
\p
\v 24 Ndipo Daudi akaja Mahanaimu. Lakini Absalomu yeye akavuka Yordani yeye pamoja na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye.
\v 25 Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Naye huyo Amasa alikuwa mwana wa Yetheri Mwishmaeli, aliyekuwa ameenda kwa Abigaili, aliyekuwa binti wa Nahashi na dada wa Seruya, mamaye Yoabu.
\v 26 Kisha Israeli na Absalomu wakapiga kambi katika nchi ya Gileadi.
\p
\v 27 Ikawa wakati Daudi alipokuwa amekuja Mahanaimu, huyo Shobi mwana wa Nahashi kutoka Raba ya Waamoni na Makiri mwana wa Amieli wa kutoka Lo Debari, na Berzilai Mgileadi wa Rogelimu,
\v 28 wakaleta magodoro na blanketi, mabakuri na vyungu, na ngano, unga wa shayiri, nafaka zilizokaangwa, maharage, dengu,
\v 29 asali, siagi, kondoo na samli, ili kwamba Daudi na watu waliokuwa pamoja naye waweze kula. Kwani walisema, “Watu wana njaa, wamechoka na wana kiu huko nyikani.”
\c 18
\cl Sura 18
\p
\v 1 Daudi akawahesabu askari waliokuwa pamoja naye na akaweka akida wa elfu na akida wa mia juu yao.
\v 2 Kisha Daudi akalipeleka jeshi, theluthi moja chini ya Yoabu, theluthi nyingine chini ya Abishai mwana wa Seruya, ndugu wa Yoabu, na theluthi nyingine tena chini ya Itai Mgiti. Mfalme akaliambia jeshi, “Kwa hakika mimi mwenyewe pia nitakwenda pamoja nanyi.
\p
\v 3 Lakini watu wakasema, “Wewe usiende vitani, kwani ikiwa tutakimbia hawatatujali sisi, ama nusu yetu wakifa hawatajali. Lakini wewe ni zaidi ya elfu kumi yetu sisi! Kwa hiyo ni afadhali zaidi ukitusaidia ukiwa mjini.”
\p
\v 4 Hivyo mfalme akawajibu, “Nitafanya lolote lionekanalo jema machoni penu.” Mfalme akasimama kati ya lango la mji wakati jeshi lilipoondoka katika mamia na katika maelfu.
\p
\v 5 Mfalme akawaagiza Yoabu, Abishai, na Itai akisema, “Mmtendee huyo kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu.” Watu wote wakasikia jinsi mfalme alivyowaagiza maakida kuhusu Absalomu.
\p
\v 6 Hivyo jeshi likaenda nyikani dhidi ya Israeli; vita ikaenea katika msitu wa Efraimu.
\v 7 Jeshi la Israeli likashindwa mbele ya askari wa Daudi; kulikuwa na machinjo makuu kwa watu 20,000 siku hiyo.
\v 8 Vita ikaenea katika eneo lote na watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga.
\p
\v 9 Ikatukia kwamba Absalomu akakutana na askari wa Daudi. Absalomu alikuwa amepanda juu ya nyumbu wake na nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mti wa mwaloni, na kichwa chake kikanaswa katika matawi ya mti. Akaachwa akining'inia kati ya nchi na anga wakati nyumbu alipoendelea mbele.
\p
\v 10 Mtu mmoja akaona lililotukia na akamwambia Yoabu, “Tazama, nilimuona Absalomu akining'inia katika mwaloni!”
\p
\v 11 Yoabu akamwambia aliyemwambia kuhusu Absalomu, “Tazama! Ulimuona! Kwa nini haukumpiga hata chini. Ningekupa shekeli kumi za fedha na mkanda.”
\p
\v 12 Yule mtu akamjibu Yoabu, “Hata kama ningepewa shekeli elfu za fedha hata hivyo nisingeinua mkono wangu juu ya mwana wa mfalme, kwa maana sisi sote tulimsikia mfalme akiwaagiza wewe, Abishai na Itai akisema, mtu asimguse huyo kijana Absalomu.
\v 13 Ikiwa ningehatarisha maisha yangu kwa uongo (na hakuna jambo linalofichika kwa mfalme), ungejitenga nami.”
\p
\v 14 Ndipo Yoabu akasema, “Sitakusubiri.” Kisha akachukua mishale mitatu mkononi mwake na akairusha katika moyo wa Absalomu wakati yu ngali hai na amening'inia katika mwaloni.
\v 15 Kisha vijana kumi waliochukua silaha za Yoabu wakamzunguka Absalomu, wakampiga na kumuua.
\p
\v 16 Kisha Yoabu akapiga tarumbeta na jeshi likarudi kutoka kuwafuatia Israeli, hivyo Yoabu akalirudisha jeshi.
\v 17 Wakamchukua Absalomu na kumtupa katika shimo kubwa msituni; wakauzika mwili wake chini ya rundo kubwa la mawe, wakati Israeli wote walikimbia kila mtu hemani mwake.
\p
\v 18 Wakati Absalomu alipokuwa yungali hai alijijengea nguzo kubwa ya jiwe katika Bonde la Mfalme, kwani alisema, “Sina mwana wa kuchukua kumbukumbu ya jina langu.” Akaiita nguzo kwa jina lake, hivyo inaitwa Mnara wa Absalomu hata leo.
\p
\v 19 Kisha Ahimaasi mwana wa Sadoki akasema, “Niruhusu niende kwa mfalme na habari njema, jinsi Yahwe alivyomuokoa kutoka mkono wa adui zake.”
\p
\v 20 Yoabu akamjibu, “Wewe hautakuwa mchukua habari leo; utafanya hivyo siku nyingine. Leo hautachukua habari yoyote kwa maana mwana wa mfalme ameuawa.”
\p
\v 21 Ndipo Yoabu akamwambia Mkushi, “Nenda umwambia mfalme ulichokiona.” Mkushi akamuinamia Yoabu, na kisha akakimbia.
\p
\v 22 Kisha tena, Ahimaasi mwana wa Sadoki akamwambia Yoabu, “Pamoja na yote yanayoweza kutokea, tafadhali niruhusu nami pia niende nimfuate Mkushi.” Yoabu akajibu, “Mwanangu kwa nini unataka kwenda, hautapata thawabu yoyote kwa ajili ya habari hii?”
\p
\v 23 “Vyovyote itakavyokuwa niache niende,” Ahimaasi alijibu. Hivyo Yoabu akamjibu, “Nenda.” Ndipo Ahimaasi akakimbia kwa njia ya tambarare na akampita Mkushi.
\p
\v 24 Basi Daudi alikuwa amekaa kati ya lango la ndani na lango la nje. Na mlinzi alikuwa juu ya lango ukutani naye akainua macho yake. Alipokuwa akiangalia, akamwona mtu anakaribia huku akikimbia peke yake.
\v 25 Mlinzi akaita kwa sauti na kumwambia mfalme. Ndipo mfalme akasema, “Ikiwa yupo peke yake ana habari katika kinywa chake.” Mkimbiaji akasogea na kuukaribia mji.
\p
\v 26 Kisha mlinzi akaona mtu mwingine aliyekuwa anakimbia, naye akamwambia bawabu; kusema, “Tazama, kuna mtu mwingine anakimbia peke yake.” Mfalme akasema, “Yeye pia analeta habari.”
\p
\v 27 Ndipo mlinzi akasema, Nadhani kukimbia kwake mtu aliye mbele ni kama kukimbia kwake Ahimaasi mwana wa Sadoki.” Mfalme akasema, “Yeye ni mtu mwema naye anakuja na habari njema.”
\p
\v 28 Ndipo Ahimaasi akaita na kumwambia mfalme, “Yote ni mema.” Kisha akainama yeye mwenyewe uso wake chini mbele ya mfalme na kusema, Atukuzwe Yahwe Mungu wako, aliyewatoa watu walioinua mkono wao kinyume cha bwana wangu mfalme.”
\p
\v 29 Hivyo mfalme akauliza, “Je huyo kijana Absalomu hajambo?” Ahimaasi akajibu, “Wakati Yoabu ananituma kwako mfalme, mimi mtumishi wa mfalme, niliona fujo kubwa sana lakini sikutambua ilihusu nini.”
\p
\v 30 Mfalme akamwambia, “Geuka usimame kando.” Hivyo Ahimaasi akageuka na kusimama.
\p
\v 31 Mara Mkushi akafika na kusema, “Kuna habari njema kwa bwana wangu mfalme kwa kuwa leo Yahwe amekulipia kisasi kwa wale wote walioinuka kinyume chako.”
\p
\v 32 Ndipo mfalme akamuuliza, “Je, huyo kijana Absalomu ni mzima?” Mkushi akajibu, “Adui wa bwana wangu mfalme na wote wainukao kukudhuru na wawe kama huyo kijana.”
\p
\v 33 Ndipo mfalme alipohuzunishwa sana, naye akaenda chumbani juu ya lango na kulia. Kadili alivyokwenda aliomboleza, “Mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! Afadhali ningekufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”
\c 19
\cl Sura 19
\p
\v 1 Yoabu akaambiwa, “Tazama, mfalme analia na kumuomboleza Absalomu.”
\v 2 Hivyo siku ile ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote, kwa maana jeshi likasikia ikisemwa siku hiyo, “Mfalme anaomboleza kwa ajili ya mwanaye.”
\v 3 Siku ile askari waliingia mjini kwa kunyemelea kimyakimya kama watu waonao haya baada ya kukimbia vitani.
\v 4 Mfalme akafunika uso wake na kulia kwa sauti, “Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwangangu!”
\p
\v 5 Ndipo Yoabu akaingia ndani kwa mfalme na kumwambia, “Leo umeziaibisha nyuso za askari wako, waliookoa maisha yako leo, maisha ya wanao na binti zako, maisha ya wake zako na maisha ya masuria wako,
\v 6 kwa maana wawapenda wakuchukiao na kuwachukia wakupendao. Kwa kuwa leo umeonyesha kwamba maakida na askari si chochote kwako. Natambua sasa kwamba kama Absalomu angesalia na sisi sote tungekufa hilo lingekufurahisha.
\v 7 Sasa basi, inuka na uende kuongea na askari wako kwa upole, kwani nakuapia kwa Yahwe, ikiwa hutakwenda hakuna mtu hata mmoja atakayesalia nawe usiku huu. Na hii itakuwa vibaya sana kwako kuliko madhara yoyote yaliyowai kukupata tangu ujana wako.”
\p
\v 8 Hivyo mfalme akainuka na kuketi kati ya lango la mji, watu wote wakaambiwa, “Tazama, mfalme ameketi kati ya lango.” Ndipo watu wote wakaja mbele za mfalme. Walakini, Israeli walikuwa wamekimbia kila mtu hemani mwake.
\p
\v 9 Watu wote wakahojiana wao kwa wao katika jamaa zote za Israeli wakisema, “Mfalme alituokoa na mkono wa adui zetu. Alitukomboa na mkono wa Wafilisti lakini sasa ameikimbia nchi mbele ya Absalomu.
\v 10 Na Absalomu tuliyemtia mafuta juu yetu amekufa vitani. Hivyo kwa nini hatuongei juu ya kumrudisha mfalme tena?”
\p
\v 11 Mfalme Daudi akatuma kwa Sadoki na kwa Abiathari makuhani akisema, “Ongeeni na wazee wa Yuda mkisema, Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme kwenye kasri lake tena, kwa vile usemi wa Israeli wote unamtaka mfalme arudi katika kasri lake?
\v 12 Ninyi ni ndugu zangu, mwili na mifupa yangu. Kwa nini basi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme?”
\v 13 Na mwambieni Amasa, “Je wewe si mwili na mfupa wangu? Mungu anifanyie hivyo na kuzidi pia ikiwa hautakuwa jemedari wa jeshi langu tangu sasa na baadaye mahali pa Yoabu.
\p
\v 14 Naye akaishinda mioyo ya watu wote wa Yuda kama mtu mmoja. Wakatuma kwa mfalme wakisema, “Rudi sasa na watu wako wote.”
\v 15 Hivyo mfalme akarudi naye akaja Yordani. Na watu wa Yuda wakaja Gilgali kwenda kumlaki mfalme ili kumvusha mfalme juu ya Yordani.
\p
\v 16 Shimei mwana wa Gera, Mbenjamini, kutoka Bahurimu, akaharakisha kushuka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki mfalme Daudi.
\v 17 Kulikuwa na watu 1,000 kutoka Benjamini waliokuwa pamoja naye, na Siba mtumishi wa Sauli na wanawe kumi na watano na watumishi wake ishirini walikuwa pamoja naye. Wakavuka Yordani mbele za mfalme.
\v 18 Wakavuka ili kuivusha familia ya mfalme na kumfanyia lolote aliloona jema. Shimei mwana wa Gera akainama chini mbele za mfalme mara alipoanza kuuvuka Yordani.
\p
\v 19 Shimei akamwambia mfalme, “Bwana wangu asinione mwenye hatia au kuyaweka moyoni ambayo mtumishi wake alifanya kwa ukaidi siku bwana wangu mfalme alipoondoka Yerusalemu. Tafadhali, mfalme na asiyaweke moyoni.
\v 20 Kwa maana mtumishi wako anatambua kwamba amekosa. Tazama, ndiyo maana nimekuja leo wa kwanza katika nyumba ya Yusufu ili kumlaki bwana wangu mfalme.”
\p
\v 21 Lakini Abishai mwana wa Seruya akajibu na kusema, “Je Shimei asife kwa hili kwa vile alivyomlaani mtiwa mafuta wa Yahweh?”
\p
\v 22 Ndipo Daudi akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya, hata leo mkawa adui zangu? Je mtu yeyote atauawa leo katika Israeli? Kwani sijui kama leo mimi ni mfalme juu ya Israeli?
\v 23 Hivyo mfalme akamwambia Shimei, “Hautakufa.” Mfalme akamuahidi kwa kiapo.
\p
\v 24 Kisha Mefiboshethi mwana wa Sauli akashuka ili kumlaki mfalme. Hakuwa ameivalisha miguu yake wala kunyoa ndevu zake wala kufua nguo zake tangu siku mfalme alipoondoka hata siku aliporudi kwa amani.
\v 25 Na hivyo alipotoka Yerusalemu ili kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, “Mefiboshethi kwa nini haukwenda pamoja nami?”
\p
\v 26 Akajibu, “Bwana wangu mfalme mtumishi wangu alinidanganya, kwani nilisema, nitapanda juu ya punda ili niende na mfalme, kwa kuwa mtumishi wako ni mlemavu.
\v 27 Mtumishi wangu Siba amenisemea uongo, mtumishi wako, kwa bwana wangu mfalme. Lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu. Kwa hiyo fanya lililojema machoni pako.
\v 28 Kwa maana nyumba yote ya baba yangu walikuwa maiti mbele ya bwana wangu mfalme, lakini ukamuweka mtumishi wako miongoni mwao walao mezani pako. Kwa hiyo nililiye haki gani zaidi kwa mfalme?”
\p
\v 29 “Kisha mfalme akamwambia, “Kwa nini kueleza yote zaidi? Nimekwisha amua kwamba wewe na Siba mtagawana mashamba.”
\p
\v 30 Ndipo Mefiboshethi akamjibu mfalme, “Sawa, acha achukue yote kwa vile bwana wangu mfalme amerudi salama nyumbani kwake.”
\p
\v 31 Kisha Berzilai Mgileadi akashuka kutoka Rogelimu ili avuke Yordani pamoja na mfalme, naye akamsaidia mfalme kuuvuka Yordani.
\v 32 Basi Berzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amemsaidia mfalme kwa mahitaji alipokuwako Mahanaimu kwani alikuwa na mali nyingi.
\v 33 Mfalme akamwambia Berzilai, njoo pamoja nami, nami nitakupa riziki ukae nami huko Yerusalemu.”
\p
\v 34 Berzilai akamjibu mfalme, “Kwani kuna siku ngapi zilizosalia maishani mwangu, hata niende na mfalme huko Yerusalemu?
\v 35 Nina umri wa miaka themanini. Je, naweza kutofautisha mema na mabaya? Je, mtumishi wako anaweza kuonja anachokula au kunywa? Je, naweza kusikia sauti zaidi za wanaume na wanawake waimbao? Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme?
\v 36 Mtumishi wako angependa tu kuvuka Yordani pamoja na mfalme. Kwa nini mfalme anilipe kwa thawabu kama hiyo?
\v 37 Tafadhali mruhusu mtumishi wako arudi nyumbani, ili kwamba nife katika mji wangu katika kaburi la baba na mama yangu. Lakini tazama, huyu hapa mtumishi wako Kimhamu. Haya yeye na avuke na bwana wangu mfalme na umfanyie lolote lipendezalo kwako.”
\p
\v 38 Mfalme akajibu, “Kimhamu atakwenda pamoja nami, nami nitamtendea kila lionekanalo jema kwako, na lolote unalotamani kutoka kwangu nitakutendea.”
\p
\v 39 Kisha watu wote wakavuka Yordani, mfalme naye akavuka, kisha mfalme akambusu Berzilai na kumbariki. Kisha Berzilai akarudi nyumbani kwake.
\p
\v 40 Hivyo mfalme akavuka kuelekea Gilgali, na Kimhamu akavuka pamoja naye. Jeshi la Yuda lote na nusu ya jeshi la Israeli likamleta mfalme.
\p
\v 41 Mara watu wa Israeli wote wakaanza kuja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemuiba na kumleta mfalme na familia yake juu ya Yordani na watu wote wa Daudi pamoja naye?”
\p
\v 42 Hivyo watu wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Ni kwa kuwa mfalme anahusiana nasi kwa karibu zaidi. Kwa nini basi mkasirike juu ya hili? Je sisi tumekula chochote ambacho mfalme amekitoa? Je ametupa zawadi yoyote?”
\p
\v 43 Watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, “Sisi tuna kabila kumi zaidi kwa mfalme hivyo tuna sehemu kubwa zaidi kwa Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mlitudharau? Je hatukuwa wa kwanza kupendekeza kumrudisha mfalme wetu?” Lakini maneno ya watu wa Yuda hata yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.
\c 20
\cl Sura 20
\p
\v 1 Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mtu asiye na thamani jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, “Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende hemani mwake, Israeli!”
\p
\v 2 Hivyo watu wote wa Israeli wakamuacha Daudi na kumfuata Sheba mwana wa Bikri. Lakini watu wa Yuda wakamfuata mfalme wao kwa karibu sana, kutoka Yordani njia yote hadi Yerusalemu.
\p
\v 3 Daudi alipofika katika kasri lake huko Yerusalemu, akawachukua masuria aliokuwa amewaacha kulitunza kasri, na akawaweka katika nyumba chini ya uangalizi. Aliwaandalia mahitaji yao lakini hakuenda kwao tena. Hivyo walikuwa wametengwa hadi siku ya kufa kwao, waliishi kama wajane.
\p
\v 4 Kisha mfalme akamwambia Amasa, “Uwaite watu wa Yuda ndani ya siku hizi tatu; wewe pia uwepo hapa.”
\v 5 Hivyo Amasa akaenda kuwaalika watu wote wa Yuda kwa pamoja, lakini akatumia muda mrefu kuliko mfalme alivyokuwa amemuamuru.
\p
\v 6 Hivyo Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatufanyia madhara zaidi ya Absalomu. Chukua watumishi wa bwana wako, askari wangu, na umfuatie asije akaingia katika mji wenye ngome na kututoroka.”
\v 7 Ndipo watu wa Yoabu wakamfuatia, pamoja na Wakerethi na Wapelethi na mashujaa wote. Wakatoka Yerusalemu ili kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\p
\v 8 Walipokuwa katika jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa silaha ya vita aliyokuwa ameivaa, alikuwa pia na upanga uliokuwa umefungwa na mkanda katika kiuno chake. Kadili alivyoendelea mbele upanga ukaanguka.
\p
\v 9 Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.
\v 10 Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakamwagika chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\p
\v 11 Kisha mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa naye akasema, “Aliye upande wa Yoabu na aliyeupande wa Daudi na amfuate Yoabu.”
\v 12 Amasa akawa anagalagala katika damu yake katikati ya njia. Mtu yule alipoona kwamba watu wote wamesimama, akambeba Amasa na kumuweka shambani kando ya njia. Akatupa vazi juu yake kwa maana aliona kila mmoja aliyekuja alisimama pale.
\v 13 Baada ya Amasa kuondolewa njiani watu wote wakamfuata Yoabu katika kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\p
\v 14 Sheba akazipita kabila zote za Israeli mpaka Abeli wa Beth Maaka, na katika nchi yote ya Berite ambao pia walijikusanya pamoja pia na kumfuatia Sheba.
\v 15 Walimpata na kumzingira huko Abeli wa Bethi Maaka. Wakajenga buruji ya kuhusuru mji nyuma ya ukuta. Jeshi lote lililokuwa pamoja na Yoabu likaugongagonga ukuta ili uanguke.
\v 16 Ndipo mwanamke mwerevu akapiga kelele kutoka ndani ya mji, “Sikiliza, Yoabu, tafadhali sikiliza! Sogea karibu nami ili niongee nawe.”
\v 17 Hivyo Yoabu akakaribia, mwanamke akamwambia, “Je wewe ni Yoabu? Akajibu, “Ni mimi.” Mwanamke akamwambia, “Sikiliza maneno ya mtumishi wako.” Akajibu, “Nasikiliza.”
\v 18 Ndipo aliposema, “Hapo zamani ilisemwa, Bila shaka tafuteni ushauri huko Abeli, na kwamba ushauri huo utamaliza maneno.
\v 19 Sisi ni mji ulio miongoni mwa miji yenye nguvu na aminifu sana katika Israeli. Mnataka kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kuumeza urithi wa Yahwe?”
\p
\v 20 Ndipo Yoabu alipojibu na kusema, “Iwe mbali, iwe mbali nami, hata nikameze au kuharibu.
\v 21 Hiyo si kweli. Lakini mtu kutoka katika nchi ya milima ya Efraimu, aitwaye Sheba mwana wa Bikri, ameinua mkono wake kinyume cha mfalme, kinyume cha Daudi. Mtoeni yeye nami nitauacha mji.” Mwanamke akamwambia Yoabu, “Utarushiwa kichwa chake kutoka juu ya ukuta.”
\p
\v 22 Kisha mwanamke akawaendea watu wote wa mji kwa hekima yake. Wakakiondoa kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumrushia Yoabu. Ndipo alipopiga tarumbeta na watu wa Yoabu wakauacha mji, kila mtu hemani mwake. Na Yoabu akarejea Yerusalemu kwa mfalme.
\p
\v 23 Yoabu alikuwa juu ya jeshi lote la Israeli na Benaya mwana wa Yehoiada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi.
\v 24 Adoramu alikuwa juu ya watu waliofanya kazi ya kulazimishwa na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mkumbushaji.
\v 25 Sheva alikuwa mwandishi, na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.
\v 26 Ira MYairi alikuwa kuhani wa Daudi.
\c 21
\cl Sura 21
\p
\v 1 Kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu katika siku za utawala wa Daudi, na Daudi akautafuta uso wa Yahwe. Hivyo Yahwe akasema, “Njaa hii ni kwa sababu ya mauaji ya Sauli na familia yake, kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni.”
\p
\v 2 Basi Wagibeoni hawakuwa uzao wa Israeli; walikuwa ni masalia ya Waamori. Watu wa Israeli walikuwa wameapa kutowauwa, lakini Sauli alitaka kuwaangamiza wote kwa husuda kwa ajili ya watu wa Israeli na Yuda.
\v 3 Ndipo Daudi alipowaita pamoja Wagibeoni na kuwaambia, “Niwafanyie nini kwa ajili ya upatanisho? Ili kwamba mweze kuwabariki watu wa Yahwe wanaorithi wema na ahadi zake?”
\p
\v 4 Wagibeoni wakamjibu, “Hili siyo jambo la fedha wala dhahabu kati yetu na Sauli au familia yake. Na siyo hitaji letu kumuua mtu yeyote katika Israeli.” Daudi akasema, “Mnasema nini ili niwafanyie nyinyi?”
\v 5 Wakamjibu mfalme, “Mtu aliyetaka kutuuwa aliyepanga kinyume chetu, ili kutuangamiza na kukosa eneo katika mipaka ya Israeli -
\v 6 haya na tupewe watu saba kutoka katika uzao wake, nasi tutawatundika mbele ya Yahwe katika Gibea ya Sauli, palipochaguliwa na Yahwe.” Mfalme akasema, “Nitawapen. I”
\v 7 Lakini mfalme akamuifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Yahwe kati ya Daudi na Yonathani mwana wa Sauli.
\v 8 Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi.
\v 9 Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
\p
\v 10 Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala hayawani wa mwituni wakati wa usiku.
\v 11 Daudi akaambiwa alichokifanya Rispa, binti Aiya, suria wa Sauli.
\v 12 Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumuua Sauli katika Gilboa.
\v 13 Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa.
\p
\v 14 Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.
\p
\v 15 Kisha Wafilisti wakaenda tena katika vita na Israeli. Hivyo Daudi na jeshi lake wakashuka na kupigana na Wafilisti. Akiwa vitani Daudi akachoshwa na vita.
\v 16 Ishbibenobu, wa uzao wa Warefai, ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa shekeli 300 na alikuwa na upanga mpya, alitaka kumuua Daudi.
\v 17 Lakini Abishai mwana wa Seruya akamuokoa Daudi, akampiga Mfilisti na kumuua. Ndipo watu wa Daudi wakamuapia, kusema, “Hautakwenda vitani pamoja nasi tena usije ukaizima taa ya Israeli.”
\p
\v 18 Ikawa baadaye kuwa na vita tena kati ya Wafilisti huko Gobu, wakati Sibekai Mhushathi alipomuua Safu, aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Warefai.
\p
\v 19 Ikawa tena katika vita na Wafilisti huko Gobu, huyo Elhanani mwana wa Jari Mbethlehemu akamuua Goliathi Mgiti, ambaye fumo la mkuki wake lilikuwa kama mti wa mfumaji.
\p
\v 20 Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai.
\v 21 Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamuua.
\p
\v 22 Hawa walikuwa wa uzao wa Warefai wa Gathi, waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake.
\c 22
\cl Sura 22
\p
\v 1 Daudi akamuimbia Yahwe maneno ya wimbo huu siku ile Yahwe alipomuokoa katika mkono wa adui zake wote na katika mkono wa Sauli.
\v 2 Akaomba hivi, “Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, aliyeniokoa.
\q1
\v 3 Mungu ni mwamba wangu. Yeye ni kimbilio langu. Ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu, aniokoaye na mabaya yote.
\q1
\v 4 Nitamuita Yahwe, astahiliye kutukuzwa, nami nitaokolewa kutoka kwa adui zangu.
\q1
\v 5 Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maji ya uharibifu yakanishinda.
\q1
\v 6 Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa.
\q1
\v 7 Katika shida yangu nilimwita Yahwe; nilimwita Mungu wangu; akaisikia sauti yangu katika hekalu lake, na kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake.
\q1
\v 8 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka. Misingi ya mbingu ikatetemeka na kutikiswa, kwa kuwa Mungu alikasirika.
\q1
\v 9 Moshi ukatoka katika pua yake, na miale ya moto ikatoka katika kinywa chake. Makaa yakawashwa nayo.
\q1
\v 10 Alizifungua mbingu akashuka, na giza totoro lilikuwa chini ya miguu yake.
\q1
\v 11 Alipanda juu ya kerubi na kuruka. Alionekana katika mawingu ya upepo.
\q1
\v 12 Naye akalifanya giza kuwa hema kumzunguka, akakusanya mawingu makubwa ya mvua angani.
\q1
\v 13 Makaa ya moto yalidondoka mbele zake kutoka katika radi.
\q1
\v 14 Yahwe alishuka kutoka katika mbingu. Aliye juu alipiga kelele.
\q1
\v 15 Alipiga mishale na kuwatawanya adui zake--miale ya radi na kuwatupa katika kuchanganyikiwa.
\q1
\v 16 Kisha njia za bahari zikaonekana; misingi ya dunia ikawa wazi katika kukanywa na Yahweh, katika sauti za pumzi ya pua zake.
\q1
\v 17 Kutoka juu alifika chini; akanishikilia! Aliniondoa katika vilindi vya maji.
\q1
\v 18 Aliniokoa kutoka kwa adui zangu wenye nguvu, kwao walionichukia, kwa maana walikuwa na nguvu sana kwangu.
\q1
\v 19 Walikuja kinyume changu siku ya shida yangu, lakini Yahwe alikuwa msaada wangu.
\q1
\v 20 Pia aliniweka mahali panapo nafasi. Aliniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
\q1
\v 21 Yahwe amenituza kwa kipimo cha haki yangu; amenirejesha kwa kiwango cha usafi wa mikono yangu.
\q1
\v 22 Kwa maana nimezishika njia za Yahwe na sijafanya uovu kwa kugeuka kutoka kwa Mungu.
\q1
\v 23 Kwa kuwa maagizo yake yote ya haki yamekuwa mbele yangu; kwa kuwa sheria zake, sikujiepusha nazo.
\q1
\v 24 Nimekuwa bila hatia mbele zake pia, na nimejiepusha na dhambi.
\q1
\v 25 Kwa hiyo Yahwe amenirejesha kwa kiasi cha uadilifu wangu, kwa kipimo cha usafi wangu mbele zake.
\q1
\v 26 Kwa mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu; kwake asiye na hatia; unajionyesha kuwa hauna hatia.
\q1
\v 27 Kwa usafi unajionyesha kuwa msafi, lakini kwa wakaidi unajionyesha kuwa mkaidi.
\q1
\v 28 Unaokoa walioteswa, lakini macho yako ni kinyume cha wenye kiburi, na unawashusha chini.
\q1
\v 29 Kwa maana wewe ni taa yangu, Yahwe. Yahwe huangaza katika giza langu.
\q1
\v 30 Kwa ajili yako ninaweza kukimbia juu ya jeshi; kwa msaada wa Mungu wangu naweza kuruka juu ya ukuta.
\q1
\v 31 Maana njia za Mungu ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi. Yeye ni ngao yao wanaomkimbilia.
\q1
\v 32 Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu?
\q1
\v 33 Mungu ni kimbilio langu, na umuongoza katika njia yake mtu asiye na hatia.
\q1
\v 34 Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
\q1
\v 35 Huifundisha mikono yangu kwa vita, na viganja vyangu kupinda upinde wa shaba.
\q1
\v 36 Umenipa ngao ya wokovu wako, na upendeleo wako umenifanya mkuu.
\q1
\v 37 Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu, hivyo miguu yangu haijateleza.
\q1
\v 38 Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza. Sikurudi nyuma hadi walipoangamizwa.
\q1
\v 39 Niliwararua na kuwapiga; hawawezi kuinuka. Wameanguka chini ya miguu yangu.
\q1
\v 40 Ulinifunga mshipi wa nguvu kwa vita; unawaweka chini yangu wanaoinuka kinyume changu.
\q1
\v 41 Ulinipa migongo ya shingo za adui zangu; niliwaangamiza kabisa wale wanaonichukia.
\q1
\v 42 Walilia kwa msaada, lakini hakuna aliyewaokoa; walimlilia Yahwe, lakini hakuwajibu.
\q1
\v 43 Niliwaponda katika vipande kama mavumbi juu ya ardhi, niliwakanyaga kama matope mitaani.
\q1
\v 44 Umeniokoa pia kutoka katika mashutumu ya watu wangu. Umeniweka kama kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua wananitumikia.
\q1
\v 45 Wageni walishurutishwa kuniinamia. Mara waliposikia kuhusu mimi, walinitii.
\q1
\v 46 Wageni walikuja wakitetemeka kutoka katika ngome zao.
\q1
\v 47 Yahwe anaishi! Mwamba wangu atukuzwe. Mungu na ainuliwe, mwamba wa wokovu wangu.
\q1
\v 48 Huyu ndiye Mungu anilipiaye kisasi, awawekaye watu chini yangu.
\q1
\v 49 Uniweka huru mbali na adui zangu. Hakika, uliniinua juu yao walioinuka kinyume changu. Uliniokoa kutoka kwa watu wenye ghasia.
\q1
\v 50 Kwa hiyo nitakushukuru, Yahwe, kati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
\q1
\v 51 Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na huonyesha uaminifu wake wa kiagano kwa mtiwa mafuta wake, kwa Daudi na uzao wake daima.”
\c 23
\cl Sura 23
\p
\v 1 Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi-Daudi mwana wa Yese, mtu aliyeheshimiwa sana, aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo, mwandishi mzuri wa zaburi wa Israeli.
\q1
\v 2 “Roho ya Yahwe alisema nami, na neno lake lilikuwa ulimini mwangu.
\q1
\v 3 Mungu wa Israeli alinena, Mwamba wa Israeli aliniambia, “Atawalaye kwa haki juu yangu, atawalaye katika hofu ya Mungu.
\q1
\v 4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua linapochomoza, asubuhi isiyo na mawingu, wakati mche mwororo unapochipua kutoka ardhini kupitia mwangaza wa mng'ao wa jua baada ya mvua.
\q1
\v 5 Hakika, je familia yangu haiko hivi mbele za Mungu? Je hajafanya nami agano la milele, taratibu la uhakika kwa kila njia? Je yeye haongezi wokovu wangu na kutimiza kila hitaji langu?
\q1
\v 6 Lakini yasiyofaa yote yatakuwa kama miiba na kutupwa mbali, kwa maana haiwezekani kukusanywa kwa mikono.
\q1
\v 7 Ayagusaye ni lazima atumie chombo cha chuma au fumo la mkuki. Ni lazima yachomwe mahali yalipo.
\p
\v 8 Haya ni majina ya askari wa Daudi: Yashobeamu Mhakmoni alikuwa kiongozi wa mashujaa. Aliua watu 800 wakati mmoja.
\p
\v 9 Baada yake alikuwa Elieza mwana wa Dodo, mwana wa mwahohi, mmoja wa mashujaa watatu wa Daudi. Alikuwepo walipowashinda Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kwa vita, na wakati watu wa Israeli walipokuwa wamekimbia.
\v 10 Elieza akasimama na kuwapiga Wafilisti mpaka mkono wake ukachoka, mpaka mkono wake ukang'ang'ania mpini wa upanga wake. Siku hiyo Yahwe akatoa ushindi mkuu. Jeshi likarejea kwa ajili ya kuteka tu nyara za waliouawa na Elieza.
\p
\v 11 Baada yake alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti wakajikusanya pamoja palipokuwa na shamba la dengu, na jeshi likawakimbia.
\v 12 Lakini Shama akasimama katikati ya shamba na kulitetea. Aliwauwa Wafilisti, na Yahwe akaleta ushindi mkuu.
\p
\v 13 Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.
\v 14 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, wakati Wafilisti walikuwa imara Bethlehemu.
\v 15 Daudi alitamani maji na akasema, “Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!”
\v 16 Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.
\v 17 Kisha akasema, “Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je, ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?” Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.
\p
\v 18 Abishai, nduguye Yoabu na mwana wa Seruya, alikuwa akida wa watatu. Alipigana kwa mkuki wake na watu mia tatu na akawauwa wote. Mara kwa mara alitajwa kati ya mashujaa watatu.
\v 19 Je, hakuwa maarufu kuliko wale watatu? Alifanywa akida wao. Lakini, umaarufu wake haukulingana na umaarufu wa wale mashujaa watatu.
\p
\v 20 Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.
\v 21 Na alimuua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumuua nao.
\v 22 Benaya mwana wa Yehoyada alifanya matendo haya, naye alitajwa kati ya mashujaa watatu.
\v 23 Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu. Hata hivyo Daudi alimuweka kuwa mlinzi wake.
\q2
\v 24 Wafuatao ni wale watu thelathini: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
\v 25 Shama Mharodi, Elika Mharodi,
\v 26 Helesi Mpeloni, Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi,
\v 27 Abi Ezeri Mwanathothi, Mebunai Mhushathi,
\v 28 Salmoni Mhahoi, Maharai Mnetofathi;
\v 29 Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi, Itai mwana wa Rabai kutoka Gibea ya Wabenjamini,
\v 30 Benaya Mpirathoni, Hidai wa mabonde ya Gaashi.
\v 31 Abieliboni Mwarbathi, Azmawethi Mbarhumi,
\v 32 Eliaba Mshalboni, wana wa Yasheni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;
\v 33 Ahiamu mwana wa Sharari Mharari,
\v 34 Elifeleti mwana wa Ahasbai Mmaakathi, Eliamu mwana wa Ahithofeli Mgiloni,
\v 35 Hezro Mkarmeli, Parai Mwarbi,
\v 36 Igali mwana wa Nathani kutoka Soba, Bani kutoka kabila la Gadi,
\v 37 Zeleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
\v 38 Ira Mwithri, Garebu Mwithri,
\v 39 Uria Mhiti - jumla yao wote thelathini na saba.
\c 24
\cl Sura 24
\p
\v 1 Kisha hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi kinyume chao kusema, “Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda.”
\p
\v 2 Mfalme akamwambia Yoabu, jemedari wa jeshi, aliyekuwa pamoja naye, “Nenda upite katika kabila zote za Israeli, toka Dani mpaka Beersheba, uwahesabu watu wote, ili niweze kujua idadi kamili ya watu wanaofaa kwa vita.”
\p
\v 3 Yoabu akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na aizidishe hesabu ya watu mara mia, na macho ya bwana wangu mfalme yaone ikifanyika. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme analitaka jambo hili?”
\p
\v 4 Walakini neno la mfalme lilikuwa la mwisho dhidi ya Yoabu na dhidhi ya majemedari wa jeshi. Hivyo Yoabu na majemedari wakatoka mbele ya mfalme kuwahesabu watu wa Israeli.
\p
\v 5 Wakavuka Yordani na kupiga kambi karibu na Aroeri, kusini mwa mji bondeni. Kisha wakasafiri kupitia Gadi mpaka Yazeri.
\v 6 Wakaja Gileadi na nchi ya Tahtimu Hodshi, kisha Dani, Jaani na karibu kuelekea Sidoni.
\v 7 Wakafika ngome ya Tiro na miji yote ya Wahivi na Wakanaani. Kisha wakaenda Negebu katika Yuda huko Beersheba.
\p
\v 8 Walipokuwa wamepita katika nchi yote, wakarejea Yerusalemu mwishoni mwa miezi tisa na siku ishirini.
\p
\v 9 Ndipo Yoabu alipotoa taarifa ya hesabu kamili kwa mfalme kuhusu watu wawezao kupigana vita. Katika Israeli kulikuwa na watu 800,000 jasiri wawezao kutoa upanga, na wale wa Yuda walikuwa watu 500,000.
\p
\v 10 Ndipo moyo wa Daudi ukamsumbua baada ya kuwahesabu watu. Hivyo akamwambia Yahwe, “Kwa kufanya hivi nimetenda dhambi sana. Sasa, Yahwe, uiondoe hatia ya mtumishi wako, kwani nimetenda kwa upumbavu.”
\p
\v 11 Daudi alipoinuka asubuhi, neno la Yahwe likamjia nabii Gadi, mwonaji wa Daudi, ikisema,
\v 12 Nenda umwambie Daudi; “Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Ninakupa mambo matatu. Uchague mojawapo.
\p
\v 13 Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je miaka mitatu ya njaa ije katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie kutoka kwa adui zako huku wakikufuatia? Au kuwe na tauni ya siku tatu katika nchi yako? Amua sasa jibu gani nimrudishie aliyenituma.”
\p
\v 14 Ndipo Daudi akamwambia Gadi, “Nipo katika shida kubwa. Haya na tuanguke katika mikono ya Yahwe kuliko kuanguka katika mikono ya mwanadamu, kwani matendo yake ya rehema ni makuu sana.”
\p
\v 15 Hivyo akatuma tauni juu ya Israeli kuanzia asubuhi kwa muda ulioamliwa, na watu 75,000 kutoka Dani mpaka Beersheba wakafa.
\v 16 Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako sasa.” Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.
\p
\v 17 Daudi alipomwona malaika aliyekuwa amewapiga watu, akamwambia Yahwe akisema, “Nimetenda dhambi, na nimetenda kwa upumbavu. Lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Tafadhali, mkono wako na uniadhibu mimi na familia ya baba yangu!”
\p
\v 18 Kisha Gadi akaja siku hiyo kwa Daudi na kumwambia, “Kwea na ujenge madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.”
\v 19 Hivyo Daudi akakwea kama Gadi alivyomuelekeza kufanya, kama Yahwe alivyokuwa ameagiza.
\v 20 Arauna akatazama na kumuona mfalme na watumishi wake wakikaribia. Ndipo Arauna akaondoka na kumsujudia mfalme uso wake mpaka juu ya ardhi.
\p
\v 21 Kisha Arauna akasema, “Kwa nini bwana wangu mfalme amekuja kwangu, mtumishi wake?” Daudi akajibu, “Kununua uwanja wako wa kupuria, ili nimjengee Yahwe madhabahu, ili kwamba tauni iondolewe kwa watu.”
\p
\v 22 Arauna akamwambia Daudi, “Chukua liwe lako, bwana wangu mfalme. Ulifanyie lolote lililojema machoni pako. Tazama, ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na miganda ya kupuria na nira kwa kuni.
\v 23 Haya Yote bwana wangu mfalme, mimi Arauna nakupa.” Kisha akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na awe nawe.”
\p
\v 24 Mfalme akamwambia Arauna, “Hapana, nahimiza kukinunua kwa thamani yake. Sitatoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe chochote ambacho hakijanigharimu kitu.” Hivyo Daudi akakinunua kiwanja cha kupuria na ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha.
\p
\v 25 Daudi akajenga madhabahu kwa Yahwe pale na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Hivyo wakamsihi Yahwe kwa niaba ya nchi, hivyo akaizuia tauni katika Israeli yote.