sw_ulb/43-LUK.usfm

1607 lines
137 KiB
Plaintext
Raw Normal View History

2017-11-08 21:23:27 +00:00
\id LUK
\ide UTF-8
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\h Luke
\toc1 Luke
\toc2 Luke
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\toc3 luk
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\mt Luke
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 1
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 1
\p
\v 1 Wengi wamejitahidi kuweka katika mpangilio simulizi kuhusu masuala ambayo yametimizwa kati yetu,
\v 2 kama walivyotupatia sisi, ambao tangu mwanzo ni mashahidi wa macho na watumishi wa ujumbe.
\v 3 Hivyo nami pia, baada ya kuchuguza kwa uangalifu chanzo cha mambo haya yote tokea mwanzo - nimeona ni vema kwangu pia kukuandikia katika mpangilio wake - mheshimiwa sana Theofilo.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 4 Ili kwamba uweze kujua ukweli wa mambo uliyofundishwa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 5 Katika siku za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani fulani aliyeitwa Zekaria, wa ukoo wa Abiya. Mke wake alitoka kwa binti za Haruni, na jina lake aliitwa Elizabeti.
\v 6 Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu; walitembea bila lawama katika amri zote na maagizo ya Bwana.
\v 7 Lakini hawakuwa na mtoto, kwa sababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
\p
\v 8 Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.
\v 9 Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.
\v 12 Zakaria alitishika alipomuona; hofu ikamwangukia.
\v 13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope Zakaria, kwa sababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.
\v 14 Utakuwa na furaha na uchangamfu, na wengi watafurahia kuzaliwa kwake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 16 Na watu wengi wa Israel watageuzwa kwa Bwana Mungu wao.
\v 17 Atakwenda mbele za uso wa Bwana katika roho na nguvu ya Eliya. Atafanya hivi ili kurejesha mioyo ya baba kwa watoto, ili kwamba wasiotii wataenenda katika hekima ya wenye haki. Atafanya hivi kuweka tayari kwa Bwana watu ambao wameandaliwa kwa ajili yake.”
\p
\v 18 Zakaria akamwambia malaika, “Nitawezaje kujua hili? Kwa sababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana.”
\p
\v 19 Malaika akajibu na kumwambia, “Mimi ni Gabrieli, ambaye husimama mbele za Mungu. Nilitumwa kukwambia, kukuletea habari hii njema.
\v 20 Na tazama, hutaongea, utakuwa kimya, hutaweza kuongea mpaka siku ile mambo haya yatakapotokea. Hii ni kwa sababu ulishindwa kuamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati mwafaka.”
\p
\v 21 Sasa watu walikuwa wakimsubiri Zakaria. Walishangazwa kwa kutumia muda mwingi hekaluni.
\v 22 Lakini alipotoka nje, hakuweza kuongea nao. Wakatambua kwamba alikuwa amepata maono alipokuwa hekaluni. Aliendelea kuonesha ishara na alibaki kimya.
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Ikatokea kwamba siku za huduma yake zilipokwisha aliondoka kurudi nyumbani kwake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 24 Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema,
\v 25 “Hili ndilo ambalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu.”
\p
\v 26 Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti,
\v 27 kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.
\v 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, “Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 29 Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 30 Malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu.
\v 31 Na tazama, utabeba mimba katika tumbo lako na utazaa mwana. Nawe utamwita jina lake Yesu.
\v 32 Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 33 Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 34 Mariamu akamwambia malaika, “Hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote?”
\v 35 Malaika akajibu na akamwambia, “Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu.
\v 36 Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.
\v 37 Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”
\p
\v 38 Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako.” Kisha malaika akamwacha.
\p
\v 39 Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea.
\v 40 Alikwenda nyumbani kwa Zakaria na akamsalimia Elizabeti.
\v 41 Ikawa, Elizabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
\v 42 Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “Umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
\v 43 Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
\v 44 Maana, iliposikika sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa furaha.
\v 45 Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”
\p
\v 46 Mariamu akasema, “Nafsi yangu inamsifu Bwana,
\q
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 47 na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\q
\v 48 Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
\q
\v 49 Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.
\q
\v 50 Na rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mtii yeye.
\q
\v 51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
\q
\v 52 Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
\q
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 53 Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\q
\v 54 Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
\v 55 (kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”
\p
\v 56 Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
\p
\v 57 Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 58 Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 59 Sasa ilitokea siku ya nane kwamba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zakaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake,
\v 60 Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.”
\v 61 Wakamwambia, “Hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.”
\v 62 Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
\v 63 Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.
\v 64 Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
\v 65 Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.
\v 66 Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, “Mtoto huyu kuwa wa namna gani?” Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
\v 67 Baba yake Zakaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
\q
\v 68 “Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
\q
\v 69 Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
\q
\v 70 kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
\q
\v 71 Atatuokoa kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
\q
\v 72 Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
\q
\v 73 kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
\q
\v 74 Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu,
\q
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 75 katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 76 Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
\q
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 77 kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\q
\v 78 Hili litatokea kwa sababu ya huruma ya Mungu wetu, sababu ambayo jua tokea juu litatujia,
\q
\v 79 kuangaza kwao wakaao gizani na katika uvuli wa mauti. Atafanya hivi kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 80 Sasa, yule mtoto akakua na kuwa mwenye nguvu rohoni na alikaa nyikani mpaka siku ya kujitokeza kwake kwa Israeli.
\c 2
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 2
\p
\v 1 Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani.
\v 2 Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 4 Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo wa Daudi.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 5 Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 6 Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 7 Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 8 Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 9 Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 10 Ndipo malaika akwaambia, “Msiogope, kwa sababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote.
\v 11 Leo Mwokozi kazaliwa kwa ajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana!
\v 12 Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.”
\p
\v 13 Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema,
\q1
\v 14 “Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao.”
\p
\v 15 Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, “Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 16 Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 17 Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto.
\v 18 Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji.
\v 19 Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 20 Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 21 Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 22 Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.
\v 23 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.”
\v 24 Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.”
\p
\v 25 Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. Mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 26 Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 27 Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,
\v 28 ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
\q1
\v 29 “Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
\q1
\v 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
\q1
\v 31 ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
\q1
\v 32 Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo wa mataifa na utukufu wa watu Israeli.”
\p
\v 33 Baba na mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.
\v 34 Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kuanguka na kuinuka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.
\v 35 Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike.”
\p
\v 36 Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,
\v 37 na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 38 Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 39 Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 40 Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 41 Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka.
\v 42 Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
\v 43 Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 45 Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
\v 46 Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 47 Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 48 Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”
\v 49 Akawaambia, “Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 50 Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 51 Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 52 Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.
\c 3
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 3
\p
\v 1 Sasa, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberia, wakati Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo ndugu yake alikuwa mkuu wa mkoa wa Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 na wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria, jangwani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 3 Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi
\v 4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, Sauti ya mtu aliaye nyikani: Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
\q1
\v 5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
\q1
\v 6 Watu wote watauona wokovu wa Mungu.
\p
\v 7 Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
\v 8 Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu,” kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 9 Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 10 Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”
\p
\v 11 Alijibu na kuwaambia, “Kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo.”
\p
\v 12 Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?
\p
\v 13 Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”
\p
\v 14 Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, “Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?” Akawaambia, “Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu.”
\v 15 Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.
\v 16 Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, “Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
\v 17 Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.”
\p
\v 18 Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.
\v 19 Yohana alimkemea pia Herode mkuu wa mkoa kwa kumuoa Herodia, mke wa ndugu yake na kwa maovu mengine mengi ambayo Herode alikuwa ameyatenda.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 20 Lakini baadaye Herode alifanya uovu mwingine mbaya sana. Alimfunga Yohana gerezani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 21 Kisha ilitokea kwamba, wakati watu wote walipokuwa wakibatizwa na Yohana, naye Yesu alibatizwa pia. Wakati alipokuwa akiomba, mbingu zikafunguka.
\v 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama njiwa, wakati huo huo sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”
\v 23 Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyodhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 24 mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu,
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 26 mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda,
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 27 mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
\v 28 mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
\v 29 mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi,
\v 30 mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu,
\v 31 mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 33 mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda,
\v 34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
\v 35 mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala.
\v 36 Mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki,
\v 37 mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 38 mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.
\c 4
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 4
\p
\v 1 Kisha, Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka mto Jordani, na aliongozwa na Roho jangwani
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 kwa siku arobaini, na huko alijaribiwa na Ibilisi. Wakati huo hakula chochote, na mwisho wa wakati huo alihisi njaa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 3 Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, liamru jiwe hili kuwa mkate.”
\p
\v 4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa; Mtu hataishi kwa mkate pekee.’”
\p
\v 5 Kisha Ibilisi alimwongoza juu kwenye kilele cha mlima, na akamwonyesha falme zote za dunia kwa muda mfupi.
\v 6 Ibilisi akamwambia, “Nitakupa mamlaka ya kutawala falme hizi zote pamoja na fahari zake. Naweza kufanya hivyo kwa sababu vyote vimekabidhiwa kwangu nivitawale, na ninaweza kumpa yeyote nitakaye kumpa.
\v 7 Kwa hiyo, kama utaniinamia na kuniabudu, vitu hivi vyote vitakuwa vyako.”
\p
\v 8 Lakini Yesu alijibu na kumwambia, “Imeandikwa, lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na lazima umtumikie Yeye peke yake.’”
\p
\v 9 Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.
\v 10 Kwa sababu imeandikwa, Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,
\v 11 na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe.’”
\p
\v 12 Yesu akijibu alimwambia, “Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 13 Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 14 Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 16 Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.
\v 17 Alikabidhiwa kitabu cha nabii Isaya, hivyo, alikifungua kitabu na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
\q1
\v 18 Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,
\q1
\v 19 kuutangaza mwaka ambao Bwana ataonesha wema wake.
\p
\v 20 Kisha akalifunga gombo, akamrudishia kiongozi wa sinagogi, na akaketi chini. Macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yalimwangalia yeye.
\v 21 Alianza kuzungumza nao akisema, “Leo andiko hili limetimizwa masikioni mwenu.”
\p
\v 22 Kila mmoja pale alishuhudia kile alichokisema Yesu, na wengi miongoni mwao walishangazwa na maneno ya hekima yaliyokuwa yakitoka katika kinywa chake. Walikuwa wakisema, “Huyu ni kijana tu wa Yusufu, siyo hivyo?”
\p
\v 23 Yesu akawaambia, “Hakika mtasema methali hii kwangu, Tabibu, jiponye mwenyewe. Chochote tulichosikia ukifanya Kapernaumu, kifanye hapa pia kijijini kwako.’”
\v 24 Pia alisema, “Hakika nawaambia ninyi, hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake.
\v 25 Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na mvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
\v 26 Lakini Eliya hakutumwa kwa yeyote mmoja wao, lakini kwa mjane mmoja tu aliyeishi Sarepta karibu na mji wa Sidoni.
\v 27 Pia, kulikuwa na wakoma wengi Israel katika kipindi cha Elisha nabii, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeponywa isipokuwa Naamani mtu wa Siria.”
\v 28 Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na hasira walipoyasikia haya yote.
\v 29 Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 Lakini alipita salama katikati yao na akaenda zake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 31 Kisha alitelemkia Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato moja alikuwa akifundisha watu ndani ya sinagogi.
\v 32 Walishangazwa na mafundisho yake, kwa sababu alifundisha kwa mamlaka.
\v 33 Sasa siku hiyo ndani ya sinagogi, kulikuwa na mtu aliyekuwa na roho ya pepo mchafu, na alilia kwa sauti ya juu,
\v 34 “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani! Wewe ni mtakatifu wa Mungu!”
\p
\v 35 Yesu alimkemea pepo akisema, “Nyamaza kimya, na umtoke mtu huyu!” Pepo yule alipomtupa mtu yule chini katikati yao, alimtoka yule mtu bila ya kumsababishia maumivu yoyote.
\p
\v 36 Watu wote walishangaa, na waliendelea kuzungumzia jambo hilo kila mmoja na mwenzake. Wakasema, “Ni maneno ya aina gani haya?” Anawaamuru roho wachafu kwa mamlaka na nguvu na wanatoka.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 37 Hivyo, habari juu ya Yesu zilienea kila sehemu katika maeneo yanayozunguka mkoa huo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 38 Kisha Yesu aliondoka katika mji huo na akaingia katika nyumba ya Simoni. Sasa, mama mkwe wake na Simoni alikuwa anaumwa homa kali, na wakamsihi kwa niaba yake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 39 Hivyo, Yesu alimsogelea, akaikemea ile homa na ikamwachia. Ghafla alisimama na akaanza kuwatumikia.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 40 Jua lilipokuwa likizama, watu walimletea Yesu kila mmoja aliyekuwa mgonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na akawaponya wote.
\v 41 Mapepo pia yaliwatoka wengi wao yakilia kwa sauti na kusema, “Wewe ni mwana wa Mungu!” Yesu aliwakemea mapepo na hakuwaruhusu waongee, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa ni Kristo.
\p
\v 42 Hata kulipokucha, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao.
\v 43 Lakini akawaambia, “Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.
\c 5
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 5
\p
\v 1 Ikawa makutano walipomsonga Yesu na kusikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti.
\v 2 Akaona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 4 Kuongea, akamwambia Simoni, “Ipeleke mashua yako mpaka kwenye kina kirefu cha maji nakushusha nyavu zako ili kuvua samaki.”
\p
\v 5 Simon akajibu na kusema, “Bwana, tumefanya kazi usiku wote, na hatukupata chochote, lakini kwa neno lako, nitazishusha nyavu.”
\v 6 Walipofanya hivyo walikusanya kiasi kikubwa cha samaki na nyavu zao zikaanza kukatika.
\v 7 Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waje na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.
\v 8 Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema, “Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana.”
\v 9 Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.
\v 10 Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 11 Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 12 Ikawa alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, “Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa.”
\p
\v 13 Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, “Nataka. Takasika.” Na saa ileile ukoma ukamwacha.
\v 14 Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, “Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao.”
\v 15 Lakini habari kumuhusu yeye zikaenea mbali zaidi, na umati mkubwa wa watu ukaja pamoja kumsikiliza akifundisha na kuponywa magonjwa yao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 16 Lakini mara kwa mara alijitenga faraghani na kuomba.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 17 Ikawa moja kati ya hizo siku alikuwa akifundisha, na walikuwapo Mafarisayo na waalimu wa sheria wamekaa hapo ambao walikuja wakitokea vijiji vingi tofauti katika mkoa wa Galilaya na Yudea, na pia kutokea katika mji wa Yerusalemu. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kuponya.
\v 18 Watu kadhaa walikuja, wamembeba kwenye mkeka mtu aliyepooza, na wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ili kumlaza chini mbele ya Yesu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 19 Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 20 Akiangalia imani yao, Yesu alisema, “Rafiki, dhambi zako umesamehewa.”
\p
\v 21 Waandishi na Mafarisayo waliaanza kuhoji hilo, wakisema, “Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani anaweza kusamehe dhambi ila Mungu pekee yake?”
\p
\v 22 Lakini Yesu, akitambua nini walichokuwa wakifikiri, aliwajibu na kuwaambia, “Kwa nini mnaulizana hili mioyoni mwenu?
\v 23 Kipi ni rahisi kusema, Dhambi zako zimesamehewa au kusema Simama utembee?
\v 24 Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi, nakwambia wewe, Amka, chukua mkeka wako na uende nyumbani kwako.’”
\v 25 Wakati huo huo akaamka mbele yao na akachukua mkeka wake aliokuwa ameulalia. Kisha akarudi nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
\p
\v 26 Kila mmoja alishangazwa na wakamtukuza Mungu. Walijawa na hofu, wakisema, “Tumeona mambo yasiyo ya kawaida leo.”
\p
\v 27 Baada ya mambo haya kutokea, Yesu alitoka huko na akamwona mtoza ushuru aliyeitwa Lawi amekaa eneo la kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 28 Hivyo Lawi akanyanyuka na kumfuata, akiacha kila kitu nyuma.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 29 Kisha Lawi akaandaa nyumbani kwake sherehe kubwa kwa ajili ya Yesu. Walikuwapo watozaushuru wengi kule na watu wengi walioketi mezani wakila pamoja nao.
\v 30 Lakini Mafarisayo na waandishi wao walikuwa wakiwanung'unikia wanafunzi, wakisema, “Kwa nini mnakula na kunywa na watoza ushuru pamoja na watu wengine wenye dhambi?”
\p
\v 31 Yesu akawajibu, “Watu walio katika afya njema hawahitaji tabibu, ni wale tu wanaoumwa ndiyo watakao mhitaji mmoja.
\v 32 Sikuja kuwaita watu wenye haki wapate kutubu, bali kuwaita wenye dhambi wapate kutubu.”
\p
\v 33 Wakamwambia, “Wanafunzi wa Yohana mara nyingi hufunga na kuomba, na wanafunzi wa Mafarisayo nao hufanya vivyo hivyo. Lakini wanafunzi wako hula na kunywa.”
\p
\v 34 Yesu akawaambia, “Inawezekana mtu yeyote akawafanya waliohudhuria harusi ya Bwana Arusi kufunga wakati Bwana Arusi bado yu pamoja nao?
\v 35 Lakini siku zitakuja wakati Bwana Arusi atakapoondolewa kwao, ndipo katika siku hizo watafunga.”
\p
\v 36 Kisha Yesu aliongea pia kwao kwa mfano. “Hakuna anayechana kipande cha nguo kutoka kwenye vazi jipya na kukitumia kurekebisha vazi la zamani. Kama akifanya hivyo, ataichana nguo mpya, na kipande cha nguo kutoka vazi jipya kisengefaa kutumika na nguo ya vazi la zamani.
\v 37 Pia, hakuna mtu ambaye huweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai mpya ingepasua kile chombo, na divai ingemwagika, na viriba vingeharibika.
\v 38 Lakini divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.
\p
\v 39 Na hakuna mtu baada ya kunywa divai ya zamani, hutaka mpya, kwa sababu husema, Ya zamani ni bora.”’
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 6
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 6
\p
\v 1 Ikawa siku ya sabato moja Yesu alikuwa akipita katika shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma mbegu, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka.
\v 2 Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato?”
\p
\v 3 Yesu, akawajibu, akisema, “Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye?
\v 4 Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hata kama ilikuwa halali kwa makuhani kuila.”
\v 5 Kisha akawaambia, “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.”
\p
\v 6 Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza.
\v 7 Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa.
\v 8 Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale.
\v 9 Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu,
\v 10 “Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 11 Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 12 Ikawa siku zile aliondoka kwenda mlimani kuomba. Aliendelea usiku mzima akimwomba Mungu.
\v 13 Ilipokuwa asubuhi, aliwaita wanafunzi wake kwake, na akawachagua kumi na wawili kati yao, ambao pia aliwaita “Mitume.”
\v 14 Majina ya wale mitume yalikuwa Simoni (ambaye pia alimwita Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,
\v 15 Mathayo, Tomaso na Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni, ambaye aliitwa Zelote,
\v 16 Yuda mwana Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye alikuwa msaliti.
\p
\v 17 Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
\v 18 Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 19 Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 20 Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 22 Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 24 Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 25 Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye.
\v 26 Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 27 Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 28 Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 29 Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 31 Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo.
\p
\v 32 Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
\v 33 Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 34 Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 35 Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa sababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 36 Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 37 Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 38 Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”
\p
\v 39 Kisha akawaambia mfano pia. “Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 40 Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 41 Na kwa nini basi wakitazama kijiti kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na kigogo kilicho ndani ya jicho lako hukiangalii?
\v 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, naomba nikitoe kijiti kilicho ndani ya jicho lako, nawe huangalii kigogo kilicho katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza kitoe kigogo katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kijiti katika jicho la ndugu yako.
\p
\v 43 Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma.
\v 45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 46 Kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, na bado hamyatendi yale nisemayo?
\v 47 Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 48 Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 49 Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile iliharibika kabisa.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 7
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 7
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 1 Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 2 Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa.
\v 3 Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife.
\v 4 Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, “Anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake,
\v 5 kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu.”
\p
\v 6 Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. Lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu.
\v 7 Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona.
\v 8 Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu Nenda na huenda, na kwa mwingine, Njoo naye huja, na kwa mtumishi wangu Fanya hiki, na yeye hufanya.”
\p
\v 9 Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema. “Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 11 Baada ya haya, Yesu alikwenda mji ulioitwa Naini. Wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambatana na umati wa watu.
\v 12 Alipokaribia lango la mji, tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake aliyekuwa mjane, na watu wengi kutoka kwenye mji walikuwa pamoja naye.
\v 13 Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie.”
\v 14 Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 16 Kisha hofu ikawajaa wote, wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu na Mungu amewaangalia watu wake.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 17 Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 18 Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.
\v 19 Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?”
\p
\v 20 Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?’”
\p
\v 21 Kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.
\v 22 Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.
\v 23 Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa.”
\p
\v 24 Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?
\v 25 Lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? Tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.
\v 26 Lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.
\v 27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu.
\p
\v 28 Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.”
\p
\v 29 Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 31 Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasa?
\v 32 Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, “Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. Tumeomboleza na hamkulia.”
\v 33 Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema, “Ana pepo.”
\v 34 Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, “Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!”
\v 35 Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
\p
\v 36 Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.
\v 37 Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 38 Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 39 Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.”
\p
\v 40 Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia.” Akasema, “Kiseme tu mwalimu!”
\v 41 Yesu akasema, “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini.
\v 42 Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?”
\p
\v 43 Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.”
\v 44 Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 45 Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 46 Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato.
\v 47 Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.”
\v 48 Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”
\p
\v 49 Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?”
\p
\v 50 Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 8
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 8
\p
\v 1 Ikawa baada ya hayo Yesu alianza kusafiri katika miji na vijiji mbalimbali, akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu. Na wale kumi wawili walikwenda pamoja naye,
\v 2 vilevile wanawake fulani waliokuwa wameponywa kutoka kwa roho wachafu na magonjwa mbalimbali. Walikuwa ni Mariamu aliyeitwa Magdalena ambaye alikuwa ametolewa pepo saba.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Yoana mke wa Kuza na meneja wa Herode, Susana, na wanawake wengine wengi, waliotoa mali vyao kwa ajili yao wenyewe.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 4 Na baada ya umati wa watu kukusanyika pamoja, wakiwemo na watu waliokuja kwake kutoka miji mbalimbali, akazungumza nao kwa kutumia mifano.
\v 5 “Mpandaji alienda kupanda mbegu, alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu hizo ziliangukia kando ya njia zikakanyagwa chini ya miguu, na ndege wa angani wakazila.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 6 Mbegu zingine zilianguka juu ya udongo wa miamba na zilipoota na kuwa miche zilipooza kwa sababu hakukuwa na unyevunyevu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 7 Mbegu zingine ziliangukia kwenye miti ya miiba, nayo hiyo miti ya miiba ikakua pamoja na zile mbegu na zikasongwa.
\v 8 Lakini mbegu zingine ziliangukia kwenye udongo unaofaa na zikazaa mazao mara mia zaidi.” Baada ya Yesu kusema mambo haya, alipaza sauti, “Yeyote aliye na masikio ya kusikia na asikie.”
\p
\v 9 Tena wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo,
\v 10 Yesu akawaambia, “Mmepewa upendeleo wa kujua siri ya ufalme wa Mungu, lakini watu wengine watafundishwa tu kwa mifano, ili kwamba wakiona wasione na wakisikia wasielewe.
\p
\v 11 Na hii ndiyo maana ya mfano huu. Mbegu ni neno la Mungu.
\v 12 Mbegu zile zilizoanguka kando kando ya njia ndiyo wale watu wanaolisikia neno, na baadaye mwovu shetani hulichukua mbali kutoka moyoni, ili kwamba wasiamini na kuokolewa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 13 Kisha na zile zilizoangukia kwenye mwamba ni watu wale wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha lakini hawana mizizi yeyote, wanaamini tu kwa muda mfupi, na wakati wa majaribu huanguka.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 14 Na mbegu zile zilizoangukia kwenye miiba ni watu wanaosikia neno, lakini wanapoendelea kukua husongwa na shughuli na utajiri na anasa za maisha haya na hawazai matunda.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 Lakini zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri ni wale watu, ambao ni wanyeyekevu na mioyo mizuri, baada ya kulisikia neno hulishikilia na likawa salama na kuazaa matunda ya uvumilivu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 16 Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka taa juu ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona.
\v 17 Kwa kuwa hakuna kitakachojificha ambacho hakitajulikana, au chochote kilicho sirini ambacho hakitajulikana kikiwa kwenye mwanga.
\v 18 Kwa hiyo kuwa makini unapokuwa unasikiliza. Kwa sababu aliye nacho, kwake ataongezewa zaidi, lakini asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitachukuliwa.”
\p
\v 19 Baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakukaribia kwa sababu ya umati wa watu.
\v 20 Na akataarifiwa, “Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe.
\p
\v 21 Lakini, Yesu akajibu akasema, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
\p
\v 22 Ikawa siku mojawapo kati ya siku zile Yesu na wanafunzi wake walipanda kwenye mtumbwi, na akawaambia, “Na tuvuke ng'ambo ya pili ya ziwa.” Wakaandaa mashua yao.
\v 23 Lakini walipoanza kuondoka, Yesu akalala usingizi, na dhoruba kali yenye upepo, na mashua yao ikaanza kujaa maji na walikuwa kwenye hatari kubwa sana.
\p
\v 24 Baadaye wanafunzi wake wakaja kwake na kumwamsha, wakisema, “Bwana mkubwa! Bwana mkubwa! Tuko karibu kufa!” Akaamka na akaukemea upepo na mawimbi ya maji vikatulia na kukawa na utulivu.
\p
\v 25 Tena akawaambia, “Imani yenu iko wapi?” Wakaogopa, walishangaa, wakasemezana kia mmoja na mwenzake, “Huyu ni nani, kiasi kwamba anaamuru hata upepo, na maji na humtii?”
\p
\v 26 Wakafika kwenye mji wa Gerasini iliyo upande wa nyuma ya Galilaya.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 27 Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 28 Alipomwona Yesu akalia kwa sauti, na akaanguka chini mbele yake, kwa sauti kubwa akisema, “Nimefanya nini kwako, Yesu mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, usiniadhibu mimi.”
\v 29 Yesu akaamuru roho mchafu imtoke mtu yule, kwa kuwa amepagawa naye mara nyingi. Hata kama alikuwa amefungwa minyororo na kubanwa na kuwekwa chini ya ulinzi, alivunja vifungo na kuendeshwa na mapepo mpaka jangwani.
\p
\v 30 Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Akajibu akisema, “Legioni.” Kwa maana mapepo mengi yameingia kwake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 31 Wakaendelea kumsihi usituamuru twende kwenye shimo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 32 Kundi la Nguruwe lilikuwa likichunga juu ya kilima, wakamsihi awaruhusu wakaingie kwa hao nguruwe. Na akawaruhusu kufanya hivyo.
\v 33 Kwa hiyo wale mapepo wakamtoka mtu yule na kuingia kwa wale nguruwe, na lile kundi likakimbia kwenye mwinuko wa mlima mpaka ziwani na wakazama humo.
\p
\v 34 Wale watu waliokuwa wanachunga wale nguruwe walipoona kilichotokea, wakakimbia na wakatoa taarifa pale mjini na nje katika miji iliyowazunguka.
\v 35 Watu waliposikia hayo walienda kuona kilichotokea, na wakaja kwa Yesu na wakamwona mtu ambaye mapepo yalikuwa yamemtoka, alikuwa amevaa vizuri na mwenye akili timamu, amekaa kwenye miguu ya Yesu, na waliogopa.
\v 36 Ndipo mmoja wao aliyeona kilichotokea alianza kuwasimlia wengine jinsi huyu mtu aliyekuwa anaongozwa na mapepo alivyoponywa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 37 Watu wote wa mkoa wa Wagerasi na maeneo yaliyozunguka walimwomba Yesu aondoke kwao kwa sababu walikuwa na hofu kuu. Na aliingia kwenye mtumbwi ili arudi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 38 Mtu yule aliyetokwa na pepo alimsihi Yesu kwenda naye, lakini Yesu alimwambia aende na kusema,
\v 39 “Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea.” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.
\p
\v 40 Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.
\v 41 Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,
\v 42 kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakimsonga.
\v 43 Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 45 Yesu akasema, “Nani ambaye kanigusa?” Walipokataa wote, Petro akasema, “Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga.”
\p
\v 46 Lakini Yesu akasema, “Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu.”
\v 47 Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.
\v 48 Kisha akasema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani.”
\p
\v 49 Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, “Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu.”
\p
\v 50 Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, “Usiogope. Amini tu, naye ataponywa.”
\v 51 Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.
\v 52 Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, “Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 53 Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 54 Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, “Mtoto, inuka,”
\v 55 roho yake ikamrudia, na akainuka wakati huohuo. Akaamrisha kwamba, apewe kitu furani ili ale.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 56 Wazazi wake wakashangaa, lakini aliwaamuru wasimwambie mtu kilichokuwa kimetokea.
\c 9
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 9
\p
\v 1 Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 3 Akawaambia, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala pesa wala msichukue kanzu mbili.
\v 4 Na nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo.
\v 5 Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 6 Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 7 Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu,
\v 8 na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena.
\v 9 Herode alisema, “Nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake?” Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu.
\p
\v 10 Wakati waliporudi wale waliotumwa, wakamwambia kila kitu walicho fanya. Akawachukua pamoja naye, akaenda peke yake katika mji uitwao Bethsadia.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 11 Lakini makutano wakasikia kuhusu hili wakamfuata, na aliwakaribisha, na akaongea nao kuhusu ufalme wa Mungu, na aliwaponya wale waliohitaji uponyaji.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 12 Siku ikaanza kuisha, na wale kumi na wawili wakaenda kwake na kusema, “Watawanye makutano kwamba waende katika vijiji vya karibu na mijini wakatafute mapumziko na chakula, kwa sababu tupo eneo la nyikani.”
\p
\v 13 Lakini akawaambia, “Nyie wapeni kitu cha kula.” Wakasema, “Hatuna zaidi ya vipande vitano vya mikate na samaki wawili, isipokuwa tungeenda na kununua chakula kwa ajili ya kusanyiko hili la watu.”
\p
\v 14 Kulikua na wanaume wapatao elfu tano pale. Akawambia wanafunzi wake. “Wakalisheni chini katika makundi ya watu wapatao hamsini kwa kila kundi.”
\v 15 Kwa hiyo wakafanya hivyo na watu wa wakaketi chini.
\v 16 Akachukua mikate mitano na samaki wawili na akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvimega katika vipande, akawapa wanafunzi wake ili waviweke mbele ya makutano.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 17 Wote wakala na wakashiba, na vipande vya chakula vilivyo baki viliokotwa na kujaza vikapu kumi na viwili.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 18 Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, “Watu husema mimi ni nani?”
\p
\v 19 Wakijibu, wakasema, “Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena.”
\p
\v 20 Akawaambia, “Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?” Akijibu Petro akasema, “Kristo kutoka kwa Mungu.”
\p
\v 21 Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili,
\v 22 akasema kwamba mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.
\p
\v 23 Akawaambia wote, “Kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate.
\v 24 Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa.
\v 25 Je itamfaidi nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake?
\v 26 Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye Mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu.
\v 27 Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu.”
\p
\v 28 Baada ya maneno hayo yapata siku nane, akawachukua Petro, Yohana na, Yakobo, wakapanda mlimani kuomba.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 29 Na alipokuwa katika kuomba, muonekano wa uso wake ulibadilika, na mavazi yake yakawa meupe na ya kung'aa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 30 Na tazama, walikuwepo wanaume wawili wakiongea naye! Walikuwa Musa na Elia,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 31 walionekana katika utukufu. Waliongea kuhusu kuondoka kwake, jambo ambalo alikaribia kulitimiza Yerusalem.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 32 Sasa Petro na wale waliokua pamoja naye walikuwa katika usingizi mzito. Lakini walipokuamka, waliuona utukufu wake na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja nae.
\v 33 Ikatokea kwamba, walipokuwa wakiondoka kwa Yesu, Petro akamwambia, “Bwana, ni vizuri kwetu kukaa hapa na inatupasa tutengeneze makazi ya watu watatu. Tutengeneze moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa, na moja kwa ajili ya Eliya.” Hakuelewa alichokuwa akiongelea.
\v 34 Alipokuwa akisema hayo, likaja wingu na likawafunika; na waliogopa walipoona wamezunguwa na wamezungukwa na wingu.
\p
\v 35 Sauti ikatoka kwenye wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mteule. Msikilizeni yeye.”
\v 36 Sauti iliponyamaza, Yesu alikuwa peke yake. Walikaa kimya, na katika siku hizo hawakumwambia yeyote lolote miongoni mwa waliyoyaona.
\p
\v 37 Siku iliyofuata, baada ya kutoka mlimani, kusanyiko kubwa la watu lilikutana naye.
\v 38 Tazama, mwanaume kutoka kwenye kusanyiko alilia kwa sauti, akisema, “Mwalimu ninakuomba umtazame mwanangu, kwa kuwa ni mwanangu wa pekee.
\v 39 Unaona roho chafu humshika, na mara hupiga kelele, na pia humfanya achanganyikiwe na kutokwa povu kinywani. Nayo humtoka kwa shida, ikimsababshia maumivu makali.
\v 40 Niliwasihi wanafunzi wako wamtoe, lakini hawakuweza.”
\p
\v 41 Yesu akajibu akasema, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka, mpaka lini nitakaa nanyi na kuchukuliana nanyi? Mlete mwanao hapa.”
\v 42 Kijana alipokuwa anakuja, pepo akamuangusha chini na kumtikisa kwa kifafa. Lakini Yesu aliikemea ile roho chafu, alimponya mvulana, na kamkabidhi kwa baba yake.
\v 43 Wote walishangazwa na ukuu wa Mungu. Lakini walipokuwa wakistaajabu wote kwa mambo yote aliyo yaliyotedeka, akasema kwa wanafunzi wake,
\v 44 “Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu.”
\v 45 Lakini hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo.
\p
\v 46 Wakaanza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao.
\v 47 Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake,
\v 48 na akasema, “Kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu.”
\p
\v 49 Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.”
\p
\v 50 Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu.”
\p
\v 51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye alielekeza uso wake Yerusalemu.
\v 52 Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
\v 53 Lakini watu huko hawakumpokea, kwa sababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu.
\v 54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?”
\v 55 Lakini aliwageukia akawakemea.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 56 Kisha walikwenda kijiji kingine.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 57 Walipokuwa wakienda katika njia yao, mtu mmoja akamwambia, “Nitakufuata popote uendapo.”
\p
\v 58 Yesu akamwambia, “Mbweha wanamashimo, ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pakulaza kichwa chake.”
\v 59 Ndipo akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Lakini yeye akasema, “Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzika baba yangu,”
\p
\v 60 Lakini yeye akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu kila mahali.”
\p
\v 61 Pia mtu mwingine akasema. “Nitakufuata, Bwana, lakini niruhusu kwanza nikawaage walio katika nyumba yangu.”
\p
\v 62 Lakini Yesu akamwambia, “Hakuna mtu, atiaye mkono wake kulima na kuangalia nyuma atakayefaa kwa ufalme wa Mungu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 10
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 10
\p
\v 1 Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda.
\v 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake.
\v 3 Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 4 Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 5 Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, Amani iwe katika nyumba hii.
\v 6 Kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 7 Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 8 Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu,
\v 9 na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
\v 10 Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni,
\v 11 Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.
\v 12 Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahimilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.
\p
\v 13 Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu.
\v 14 Lakini itakuwa usitahimilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu.
\v 15 Wewe Kapernaumu, unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu.
\p
\v 16 Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi amtakaa aliyenituma.”
\p
\v 17 Wale sabini walirud i kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
\v 18 Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
\v 19 Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
\v 20 Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”
\p
\v 21 Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”
\v 22 “Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”
\p
\v 23 Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.
\v 24 Ninawaambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”
\p
\v 25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi uzima wa milele?”
\p
\v 26 Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”
\p
\v 27 Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.”
\p
\v 28 Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.”
\p
\v 29 Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
\p
\v 30 Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu ya kufa.
\v 31 Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 32 Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 33 Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. Alipomuona, alisukumwa kwa huruma.
\v 34 Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.
\v 35 Siku ilyofuata alichukua dinari mbili, na akampatia mmiliki wa nyumba ya wageni na kumwambia, Muhudumie na chochote cha ziada utakacho tumia, nitakulipa nitakaporudi.
\v 36 Ni yupi kati ya hawa watatu, unafikiri, alikuwa ni jirani kwake yeye aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?”
\p
\v 37 Mwalimu alisema, “Ni yule aliyeonesha huruma kwake.” Yesu akamwambia, “Nenda na ukafanye vivyo hivyo”
\p
\v 38 Ikawa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 39 Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 40 Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.”
\p
\v 41 Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi,
\v 42 lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 11
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 11
\p
\v 1 Ilitokea wakati Yesu alipokuwa anaomba mahali fulani, mmoja wa mwanafunzi wake alimwambia, “Bwana, tufundishe sisi kuomba kama Yohana alivyo wafundisha wanafunzi wake.”
\p
\v 2 Yesu akawaambia, Msalipo, semeni, “Baba, Jina lako litakazwe. Ufalme wako uje.
\v 3 Utupe mkate wetu wa kila siku.
\v 4 Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe wote waliotukosea. Usituongoze katika majaribu.”
\p
\v 5 Yesu akawaambia, “Ni nani kwenu atakuwa na rafiki, ambaye atamuendea usiku, na kumwambia, Rafiki niazime mikate mitatu.
\v 6 Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.
\p
\v 7 Na yule aliyeko ndani akamjibu, Usinitaabishe, mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 8 Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 9 Nami pia nawaambieni, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake?
\v 12 Au akimuomba yai atampa nge?
\v 13 Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”
\p
\v 14 Baadaye, Yesu akawa anakemea pepo, na mtu mwenye pepo alikuwa bubu. Ikawa pepo lilipomtoka, mtu huyo aliweza kuongea. Umati wakastaajabu sana.
\v 15 Lakini watu wengine wakasema, huyu anatoa mapepo kwa Beelzebul, mkuu wa mapepo.
\v 16 Wengine walimjaribu na kumtaka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
\p
\v 17 Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao na kuwaambia, “Kila ufalme utakaogawanyika itakuwa ukiwa, na nyumba iliyo gawanyika itaanguka.
\v 18 Kama Shetani atakuwa amegawanyika, ufalme wake utasimamaje? Kwa sababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli
\v 19 Kama mimi natoa mapepo kwa Belzebuli, je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani? Kwa sababu hii, wao watawahukumu ninyi.
\v 20 Lakini, kama natoa mapepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umewajia.
\p
\v 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha akilinda nyumba yake, vitu vyake vitakaa salama.
\v 22 Lakini akivamiwa na mtu mwenye nguvu zaidi, Yule mtu mwenye nguvu atamnyang'anya silaha zake, na kuzichukua mali zake zote.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Yeye asiye pamoja nami yuko kinyume nami, na yeye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 24 Pepo mchafu amtokapo mtu, huenda na kutafuta mahali pasipo na maji ili ajipumzishe. Atakapokuwa amekosa, husema, Nitarudi nilipotoka.
\v 25 Akirudi na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri.
\v 26 Hivyo huenda na kutafuta mapepo saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe na kuwaleta waje wakae mahali pale. Na hali ya mtu huyo huwa mbaya kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza.”
\p
\v 27 Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipaza sauti yake zaidi ya wote kwenye mkutano wa watu na kusema “Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya.”
\v 28 Lakini yeye akasema, “Wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.”
\p
\v 29 Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema, “Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki
\v 31 Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni.
\v 32 Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 33 Hakuna Mtu yeyote, awashaye taa na kuiweka sehemu ya chini yenye giza isiyoonekana au chini ya kikapu, ila huwasha na kuweka juu ya kitu ili kila mtu aingiaye aweze kuona mwanga.
\v 34 Jicho lako ni taa ya mwili. Jicho lako likiwa zuri basi mwili wako wote utakuwa kwenye mwanga. Lakini jicho lako likiwa baya basi mwili wako wote utakuwa kwenye giza.
\v 35 Kwa hiyo, mjihadhari ili mwanga ulio ndani yenu usitiwe giza.
\v 36 Hivyo basi, kama mwili wako wote uko kwenye mwanga, na hakuna sehemu iliyo katika giza, basi mwili wako utakuwa sawa na taa iwakayo na kutoa mwanga kwenu.”
\p
\v 37 Alipomaliza kuongea, Farisayo alimwalika akale chakula nyumbani kwake, naye Yesu akaingia ndani na kuwa pamoja nao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 38 Na Mafarisayo wakashangaa kwa jinsi ambavyo hakunawa kwanza kabla ya chakula cha jioni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 39 Lakini Bwana akawaambia, “Ninyi Mafarisayo mnaosha nje ya vikombe na bakuli, lakini ndani yenu mmejaa tamaa na uovu.
\v 40 Ninyi watu msio na ufahamu, Je yeye aliyeumba nje hakuumba na ndani pia?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 41 Wapeni masikini yaliyo ndani, na mambo yote yatakuwa safi kwenu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 42 Lakini ole wenu Mafarisayo, kwani mnatoa zaka ya mnanaa na mchicha na kila aina ya mboga ya bustani. Lakini mmeacha mambo ya haki na kumpenda Mungu. Ni muhimu zaidi kufanya yaliyo ya haki na kumpenda Mungu, bila kuacha kufanya na hayo mengine pia.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 43 Ole wenu Mafarisayo, kwa kuwa mnapenda kukaa katika viti vya mbele kwenye masinagogi na kuamkiwa kwa salamu za heshima sokoni.
\v 44 Ole wenu, kwani mnafanana na makaburi yasiyo na alama ambayo watu hutembea juu yake pasipokujua.”
\p
\v 45 Mwalimu mmoja wa sheria za Kiyahudi akamjibu na kumwambia, “Mwalimu, unachokisema kinatuudhi pia sisi.”
\p
\v 46 Yesu akasema, “Ole wenu, waalimu wa sheria! Kwani mnawapa watu mizigo mikubwa wasiyoweza kuibeba, walakini ninyi hamgusi mizigo hiyo hata kwa moja ya vidole vyenu.
\v 47 Ole wenu, kwa sababu mnajenga na kuweka kumbukumbu kwenye makaburi ya manabii ambao waliuwawa na mababu zenu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 48 Hivyo ninyi mwashuhudia na kukubaliana na kazi walizozifanya mababu zenu, kwa sababu hakika waliwauwa manabii ambao mnajenga kumbukumbu katika makaburi yao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 49 Kwa sababu hiyo pia, hekima ya Mungu inasema, Nitawatumia manabii na mitume nao watawatesa na kuwaua baadhi yao.
\v 50 Kizazi hiki kitawajibika kwa damu ya manabii waliouawa tangu kuanza kwa dunia,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 51 Kutoka damu ya Abeli hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa katikati ya madhabahu na patakatifu. Ndiyo, nawaambia ninyi, kizazi hiki kitawajibika.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 52 Ole wenu waalimu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu mmechukua funguo za ufahamu; nyie wenyewe hamuingii, na wale wanaotaka kuingia mnawazuia.”
\p
\v 53 Baada ya Yesu kuondoka pale, waandishi na mafarisayo walimpinga na kubishana naye juu ya mambo mengi,
\v 54 wakimvizia, ili wapate neno litokalo kinywani mwake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 12
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 12
\p
\v 1 Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki.
\v 2 Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 4 Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 5 Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 6 Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? Hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 7 Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 8 Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
\v 9 Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wenye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
\v 12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
\p
\v 13 Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
\p
\v 14 Yesu akamjibu, “Ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu?”
\v 15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
\p
\v 16 Yesu akawaambia mfano, akisema, “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
\v 17 na akajiuliza ndani yake, akisema, Nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
\v 18 Akasema, Nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
\v 19 Nitaiambia nafsi yangu, Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”
\p
\v 20 Lakini Mungu akamwambia, Ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
\p
\v 21 Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.”
\p
\v 22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu__ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu __ya kuwa mtavaa nini
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 24 Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
\v 25 Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
\v 26 Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?
\v 27 Tafakarini jinsi maua yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
\v 28 Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? Enyi wa imani haba!
\v 29 Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 31 Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 32 msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 33 Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa, hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 34 Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 35 Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 36 na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 37 Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 38 Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 39 Lakini fahamuni neno hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 40 Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 41 Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu?”
\p
\v 42 Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
\v 43 Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 45 Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
\v 46 bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu.
\v 47 Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 48 Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 49 Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka.
\v 50 Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utakapokamilika!
\v 51 Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
\v 52 Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.
\v 53 Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.”
\p
\v 54 Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema, Nyakati za mvua zimewadia, na ndivyo inavyo kuwa,
\v 55 Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 56 Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 57 Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?
\v 58 Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani.
\v 59 Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 13
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 13
\p
\v 1 Wakati huo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao.
\v 2 Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 4 Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 5 Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 6 Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata.
\v 7 Akamwambia mtunza bustani, Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani unaleta uharibifu wa ardhi?
\p
\v 8 Mtunza bustani akajibu na kusema, Uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake.
\v 9 Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate!”’
\p
\v 10 Sasa Yesu alikuwa akifundisha katika mojawapo ya Masinagogi wakati wa Sabato
\v 11 Tazama, alikuwepo mama mmoja ambaye kwa miaka kumi na minane alikuwa na roho mchafu wa udhaifu, na yeye alikuwa amepinda na hana uwezo kabisa wa kusimama.
\v 12 Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umewekwa huru kutoka kwenye udhaifu wako.”
\v 13 Akaweka mikono yake juu yake, na mara mwili wake akajinyoosha na akamtukuza Mungu.
\p
\v 14 Lakini mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo mtawala akajibu akawambia makutano, “Kuna siku sita ambazo ni lazima kufanya kazi. Njoni kuponywa basi, si katika siku ya Sabato.”
\p
\v 15 Bwana akamjibu na akasema, “Wanafiki! Hakuna kila mmoja wenu kufungua punda wako au ng'ombe kutoka zizini na kuwaongoza kumpeleka kunywa siku ya Sabato?
\v 16 Hivyo pia binti wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga kwa miaka kumi na minane, je haikumpasa kifungo chake kisifunguliwe siku ya sabato?”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 17 Alipokuwa akisema maneno hayo, wale wote waliompinga waliona aibu, bali makutano wote wa wengine walishangilia kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyotenda.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 18 Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 19 Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 20 Tena akasema, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?
\v 21 Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganya kwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka.”
\p
\v 22 Yesu alitembelea kila mji na kijiji njiani akielekea Yerusalemu na kuwafundisha.
\v 23 Mtu mmoja akauliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” Hivyo akawaambia,
\v 24 “Jitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa sababu wengi watajaribu na hawataweza kuingia.
\v 25 Mara baada ya mmiliki wa nyumba kusimama na kufunga mlango, basi mtasimama nje na kupiga hodi mlangoni na kusema, Bwana, Bwana, tufungulie, yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui ninyi wala mtokako.
\p
\v 26 Ndipo mtasema, Tulikula na kunywa mbele yako na wewe ulifundisha katika mitaa yetu.
\p
\v 27 Lakini yeye atawajibu, Nawaambia, siwajui mtokako, ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!
\v 28 Kutakuwa na kilio na kusaga meno wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka, Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje.
\v 29 Watafika kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, na kupumzika katika meza ya chakula cha jioni katika ufalme wa Mungu.
\v 30 Na tambua hili, wa mwisho ni wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho.”
\p
\v 31 Muda mfupi baadaye, baadhi ya Mafarisayo walikuja na kumwambia, “Nenda na ondoka hapa kwa sababu Herode anataka kukuua.”
\p
\v 32 Yesu akasema, “Nendeni mkamwambie yule mbweha, Tazama, ninawafukuza pepo na kufanya uponyaji leo na kesho, na siku ya tatu nitatimiza lengo langu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 33 Katika hali yoyote, ni muhimu kwa ajili yangu kuendelea leo, kesho, na siku iliyofuata, kwa vile haikubaliki kumuua nabii mbali na Yerusalemu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 34 Yerusalemu, Yerusalemu, nani anawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wenu kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini humkulitaka hili.
\v 35 Tazama, nyumba yako imetelekezwa. Nami nawaambia, hamuwezi kuniona hata mtakaposema Amebarikiwa huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 14
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 14
\p
\v 1 Ilitokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu.
\v 2 Tazama, pale mbele yake alikuwa mtu ambaye anasumbuliwa na uvimbe.
\v 3 Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, “Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?”
\v 4 Lakini wao walikuwa kimya, kwa hiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake.
\v 5 Naye akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe ametumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 6 Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 7 Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia,
\v 8 “Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketia nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe.
\v 9 Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, “Mpishe mtu huyu nafasi yako,” na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho.
\v 10 Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, Rafiki, nenda mbele zaidi. Ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani.
\v 11 Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa.”
\p
\v 12 Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, “Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
\v 13 Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu,
\v 14 na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”
\p
\v 15 Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwaambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!”
\p
\v 16 Lakini Yesu akamwaambia, “Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi.
\v 17 Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
\p
\v 18 Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.
\p
\v 19 Na mwingine akasema, Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.
\p
\v 20 Na mtu mwingine akasema, Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.
\p
\v 21 Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.
\p
\v 22 Mtumishi akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.
\p
\v 23 Bwana akamwambia mtumishi, Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.
\v 24 Kwa maana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu.”
\p
\v 25 Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,
\v 26 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 27 Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 28 Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?
\v 29 Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki,
\v 30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
\p
\v 31 Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
\v 32 Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 33 Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 34 Chumvi ni nzuri, lakini ikiwa Chumvi imepoteza ladha yake, jinsi gani inaweza kuwa chumvi tena?
\v 35 Haina matumizi kwa udongo au hata kwa mbolea. Hutupwa mbali. Yeye aliye na masikio ya kusikia, na asikie.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 15
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 15
\p
\v 1 Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza.
\v 2 Mafarisayo wote na waandishi wakanung'unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”
\p
\v 3 Yesu akasema mfano huu kwao, akisema
\v 4 “Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 5 Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 6 Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.
\v 7 Nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.
\p
\v 8 Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?
\v 9 Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.
\v 10 Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”
\p
\v 11 Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili
\v 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao.
\v 13 Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 14 Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 15 Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 16 Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 17 Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!
\v 18 Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.
\v 19 Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
\v 20 Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
\v 21 Yule mwana akamwambia, Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.
\p
\v 22 Yule baba aliwaambia watumishi wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.
\v 23 Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.
\v 24 Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana, wakaanza kushangilia.
\p
\v 25 Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.
\v 26 Akaita mtumishi mmoja akamuuliza, Mambo haya maana yake nini?
\v 27 Mtumishi akamwambia, Mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.
\p
\v 28 Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi.
\v 29 Ila akamjibu baba yake akisema, Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu.
\v 30 Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.
\p
\v 31 Baba akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.
\v 32 Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.’”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 16
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 16
\p
\v 1 Yesu aliwaambia tena wanafunzi wake, “Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyekuwa na meneja, na alitaarifiwa ya kwamba meneja huyu anatapanya mali zake.
\v 2 Hivyo tajiri akamwita, akamwambia, Ni nini hii ninayo isikia juu yako? Toa hesabu ya umeneja wako, kwa kuwa huwezi kuwa meneja tena.
\p
\v 3 Yule meneja akasema moyoni mwake, Nifanye nini, maana bwana wangu ananiondolea kazi yangu ya umeneja? Sina nguvu za kulima, na kuomba naona haya.
\v 4 Najua nitakalotenda ili nitakapotolewa katika kazi yangu ya uwakili watu wanikaribishe nyumbani mwao.
\v 5 Hivyo wakili akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja akamwambia wa kwanza, Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?
\p
\v 6 Akasema Vipimo mia moja vya mafuta, akamwambia, Chukua hati yako keti upesi andika hamsini.
\p
\v 7 Kisha akamwambia mwingine, Na wewe unadaiwa kiasi gani? akasema, Vipimo mia moja vya unga vya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako andika themanini.
\v 8 Yule bwana akamsifu meneja dhalimu kwa vile alivyotenda kwa werevu. Kwakua watoto wa ulimwengu huu ni werevu na hushughulika kwa ujanja na watu wa upande wao kuliko walivyo watoto wa nuru.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 9 Nami nawaambia jifanyieni marafiki kwa mali ya udhalimu ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia. Na aliye dhalimu katika lililo dogo huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
\v 11 Kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu ni nani atakayewaamini katika mali ya kweli?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika kutumia mali ya mtu mwingine ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.”
\p
\v 14 Basi Mafarisayo, ambao walikuwa wanapenda fedha waliyasikia haya yote na wakamdhihaki.
\v 15 Na akawaambia, “Ninyi ndiyo mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.
\p
\v 16 Sheria na manabii vilikuwapo mpaka Yohana alivyokuja. Tangu wakati huo, habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujaribu kujiingiza kwa nguvu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 17 Lakini ni rahisi kwa mbingu na nchi vitoweke kuliko hata herufi moja ya sheria ikosekane.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini, naye amwooaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 19 Palikua na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi na alikua akifurahia kila siku utajiri wake mkubwa.
\v 20 Na maskini mmoja jina lake Lazaro aliwekwa getini pake, na ana vidonda.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 21 Naye alikua akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 22 Ikawa yule maskini alikufa na akachukuliwa na Malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa akazikwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Na kule kuzimu alipokua katika mateso aliyainua macho yake akamuona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 24 Akalia akasema, Baba Ibrahimu, nihurumue umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
\p
\v 25 Lakini Ibrahimu akasema, Mwanangu kumbuka ya kwamba katika maisha yako uliyapokea mambo yako mema, na Lazaro vivyo alipata mabaya. Ila sasa yupo hapa anafarijiwa na wewe unaumizwa.
\v 26 Na zaidi ya hayo, kumewekwa shimo kubwa na refu kati yetu, ili wale wanaotaka kutoka huku kwenda kwenu wasiweze wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
\p
\v 27 Yule tajiri akasema, Nakuomba Baba Ibrahimu, kwamba umtume nyumbani kwa baba yangu
\v 28 kwa kuwa ninao ndugu watano ili awaonye, kwa hofu kwamba wao pia watakuja mahali hapa pa mateso.
\p
\v 29 Lakini Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii. Waache wawasikilize wao.
\p
\v 30 Yule tajiri akasema, Hapana, Baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu watatubu.
\p
\v 31 Lakini Ibrahimu akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.’”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 17
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 17
\p
\v 1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, lakini ole wake mtu anayeyasababisha!
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 3 Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe.
\v 4 Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, Ninatubu, msamehe!”
\p
\v 5 Mitume wake wakamwambia Bwana, “Tuongezee imani yetu.”
\p
\v 6 Bwana akasema, “Kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, N'goka na ukaote baharini, nao ungewatii.
\p
\v 7 Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, Njoo haraka na keti ule chakula?
\v 8 Je hatamwambia, Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa?
\v 9 Hata mshukuru mtumishi huyo kwa sababu katimiza yale aliyoamriwa?
\v 10 Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni, Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’”
\p
\v 11 Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya.
\v 12 Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali
\v 13 wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.”
\p
\v 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokua wakienda wakatakasika.
\v 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 16 Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 17 Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?
\v 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?”
\v 19 Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”
\p
\v 20 Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana.
\v 21 Wala watu hawatasema, Angalia hapa! au, Angalia kule! kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
\p
\v 22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona.
\v 23 Watawaambia, Angalia, kule! Angalia, hapa! Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuata,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 24 kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 25 Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.
\v 26 Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokua katika siku ya Mwana wa Adamu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 27 Walikula, walikunywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile ambayo Nuhu alipoingia katika safina na gharika ikaja na kuwaangamiza wote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 28 Ndivyo ilivyokua katika siku za Lutu, walikula, kunywa, wakinunua na kuuza, kulima na walijenga.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ikawaangamiza wote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 30 Hivyo ndivyo itakavyo kuwa siku ile ya Mwana wa Adamu atakapofunuliwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 31 Siku hiyo, usimruhusu aliye kwenye dari ya nyumba ashuke kuchukue bidhaa zake ndani ya nyumba. Na usimruhusu aliyeko shambani kurudi nyumbani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 32 Mkumbuke mke wa Lutu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 33 Ye yote anaejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 34 Nakwambia, usiku huo kutakua na watu wawili katika kitanda kimoja. Mmoja atachukuliwa, na mwingine ataachwa.
\v 35 Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.”
\p
\v 37 Wakamwuliza, “Wapi, Mungu?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai hukusanyika kwa pamoja.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 18
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 18
\p
\v 1 Kisha akawaambia mfano wa namna wanavyopaswa kuomba daima, na wasikate tamaa.
\v 2 Akaisema, “Kulikuwa na hakimu katika mji fulani, ambaye hakuwa anamwogopa Mungu na hakuwaheshimu watu.
\v 3 Kulikuwa na mjane katika jiji hilo, naye alimwendea mara nyingi, akisema, Nisaidie kupata haki dhidi ya mpinzani wangu.
\p
\v 4 Kwa muda mrefu hakuwa tayari kumsaidia, lakini baada ya muda akasema moyoni mwake, Ingawa mimi simwogopi Mungu au kuheshimu mtu,
\v 5 lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua nitamsaidia kupata haki yake, ili asije akanichosha kwa kunijia mara kwa mara.’”
\v 6 Kisha Bwana akasema, “Sikiliza alivyosema huyo hakimu dhalimu.
\v 7 Je Mungu pia hataleta haki kwa wateule wake ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, yeye hatakuwa mvumilivu kwao?
\v 8 Nawaambia kwamba ataleta haki kwao upesi. Lakini wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atakuta imani duniani?”
\p
\v 9 Ndipo akawaambia mfano huu kwa baadhi ya watu ambao wanajiona wenyewe kuwa wenye haki na kuwadharau watu wengine,
\v 10 “Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo mwingine mtoza ushuru.
\v 11 Farisayo akasimama akaomba mambo haya juu yake mwenyewe, Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang'anyi, watu wasio waadilifu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru.
\v 12 Nafunga mara mbili kila wiki. Natoa zaka katika mapato yote ninayopata.
\p
\v 13 Lakini yule mtoza ushuru, alisimama mbali, bila hakuweza hata kuinua macho yake mbinguni, akagonga kifua chake akisema, Mungu, nirehemu mimi mwenye dhambi.
\v 14 Nawaambia, mtu huyu alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki kuliko yule mwingine, kwa sababu kila ajikwezaye atashushwa, lakini kila mtu anayejinyenyekeza atainuliwa.”
\p
\v 15 Watu walimletea watoto wao wachanga, ili aweze kuwagusa, lakini wanafunzi wake walipoona hayo, wakawazuia.
\v 16 Lakini Yesu akawaita kwake akisema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie. Maana ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao.
\v 17 Amini, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto ni dhahiri hatauingia.”
\p
\v 18 Mtawala mmoja akamwuliza, akisema, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
\p
\v 19 Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema, ila Mungu peke yake.
\p
\v 20 Unazijua amri- usizini, usiue, Usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.”
\p
\v 21 Yule mtawala akasema, “Mambo haya yote nimeyashika tangu nilipokuwa kijana.”
\p
\v 22 Yesu alipoyasikia hayo akamwambia, “Umepungukiwa jambo moja. Lazima uuze vyote ulivyonavyo na uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni -kisha njoo, unifuate.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Lakini tajiri aliposikia hayo, alihuzunika sana, kwa sababu alikuwa tajiri sana.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 24 Kisha Yesu, akamwona alivyohuzunika sana akasema, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
\v 25 Maana ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
\p
\v 26 Wale waliosikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeweza kuokolewa?”
\p
\v 27 Yesu akajibu, “Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.”
\p
\v 28 Petro akasema, “Naam, sisi tumeacha kila kitu na tumekufuata wewe.”
\p
\v 29 Kisha Yesu akawaambia, “Amini, nawaambia kwamba hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto, kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
\v 30 ambaye hatapokea mengi zaidi katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao, uzima wa milele.”
\p
\v 31 Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawili, akawaambia, “Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa.
\v 32 Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate.
\v 33 Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 34 Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 35 Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada,
\v 36 aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza nini kinatokea.
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 37 Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 38 Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.”
\v 39 Wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, “Mwana wa Daudi, unirehemu.”
\p
\v 40 Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza,
\v 41 “Unataka nikufanyie nini.” Akasema, “Bwana, nataka kuona.”
\p
\v 42 Yesu akamwambia, “Upate kuona. Imani yako imekuponya.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.
\c 19
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 19
\p
\v 1 Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 3 Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 4 Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 5 Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.”
\v 6 Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha.
\v 7 Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, “Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.”
\p
\v 8 Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”
\p
\v 9 Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.
\v 10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea.”
\p
\v 11 Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.
\v 12 Hivyo akawaambia, “Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.
\v 13 Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, Fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.
\p
\v 14 Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, Hatutaki mtu huyu atutawale.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 16 Wa kwanza akaja, akasema, Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi.
\p
\v 17 Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi.
\p
\v 18 Wa pili akaja, akasema, Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.
\p
\v 19 Huyo Afisa akamwambia, Chukua mamlaka juu ya miji mitano.
\p
\v 20 Na mwingine akaja, akasema, Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,
\v 21 kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda.
\p
\v 22 Huyo Ofisa akamwambia, Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
\v 23 Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
\v 24 Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.
\p
\v 25 Wakamwambia, Bwana, yeye ana mafungu kumi.
\p
\v 26 Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
\v 27 Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu.’”
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 28 Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 29 Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
\v 30 akisema: “Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
\v 31 Kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni, Bwana anamhitaji.’”
\v 32 Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
\p
\v 33 Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, “Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?”
\p
\v 34 Wakasema, “Bwana anamhitaji.”
\v 35 Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 36 Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 37 Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,
\v 38 wakisema, “Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!”
\p
\v 39 Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.”
\p
\v 40 Yesu akajibu, akasema, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti.”
\p
\v 41 Yesu alipoukaribia mji aliulilia,
\v 42 akisema, “Laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
\v 43 Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande.
\v 44 Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa.”
\p
\v 45 Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,
\v 46 akiwaambia, “Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”
\p
\v 47 Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 48 lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.
\c 20
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 20
\p
\v 1 Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa sheria walimwendea pamoja na wazee.
\v 2 Walizungumza, wakimwambia, “Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya?”
\p
\v 3 Naye akajibu, akawaambia, “Nami pia nitawauliza swali. Niambieni
\v 4 ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu?”
\p
\v 5 Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Tukisema ilitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumwamini?
\p
\v 6 Na tukisema; Ilitoka kwa wanadamu; watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.”
\v 7 Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka.
\p
\v 8 Yesu akawaambia, “Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
\p
\v 9 Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 12 Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 13 Hivyo bwana wa shamba akasema, Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu.
\p
\v 14 Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu.
\v 15 Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?
\v 16 Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine.” Nao waliposikia hayo, wakasema, “Mungu amekataa.”
\p
\v 17 Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni?
\p
\v 18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda.’”
\p
\v 19 Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 20 Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 21 Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
\v 22 Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
\p
\v 23 Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
\v 24 “Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, “Ya Kaisari.”
\p
\v 25 Naye akawaambia, “Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 26 Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 27 Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
\v 28 wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
\v 29 Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
\v 30 na wa pili pia.
\v 31 Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
\v 32 Baadaye yule mwanamke pia akafa.
\v 33 Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.”
\p
\v 34 Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.
\v 35 Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 36 Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 37 Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
\v 38 Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake.”
\p
\v 39 Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, “Mwalimu, umejibu vema.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 40 Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 41 Yesu akawaambia, “Kivipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
\v 42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
\q
\v 43 mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.
\p
\v 44 Daudi anamwita Kristo Bwana, basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
\p
\v 45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,
\v 46 “Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na wapenda salamu maalum sokoni na viti vya heshima katika masinagogi, na maeneo ya heshima karamuni.
\v 47 Wao pia hula nyumba za wajane, na wanajifanya wanasali sala ndefu. Hawa watapokea hukumu kubwa zaidi.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 21
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 21
\p
\v 1 Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina.
\v 2 Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili.
\v 3 Hivyo akasema, “Kweli nawaambieni, huyu mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote.
\v 4 Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake.”
\p
\v 5 Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema,
\v 6 “Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa.”
\p
\v 7 Hivyo wakamuuliza, wakasema, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?”
\p
\v 8 Yesu akajibu, “Muwe waangalifu kwamba msidanganywe. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, na Muda umekaribia. Msiwafuate.
\v 9 Mkisikia vita na vuruguvurugu msiogope, kwa sababu haya mambo lazima yatokee kwanza, lakini mwisho hautatokea upesi.”
\p
\v 10 Kisha akawaambia, “Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 11 Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 12 Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 13 Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 14 Kwa hiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 15 kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 16 Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.
\v 17 Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu.
\v 18 Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 19 Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 20 Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.
\v 21 Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 22 Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 23 Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 24 Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 25 Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 26 Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 27 Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.
\v 28 Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.”
\p
\v 29 Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote.
\v 30 Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 31 Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 32 Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 34 Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla
\v 35 kama mtego. Kwa sababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima.
\v 36 Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
\p
\v 37 Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.
\v 38 Watu wote walimjia asubuhi na mapema ili kumsikiliza ndani ya hekalu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 22
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 22
\p
\v 1 Basi sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu ilikuwa imekaribia, ambayo inaitwa pasaka.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 2 Makuhani wakuu na waandishi wakajadiliana namna ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 3 Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na mbili.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 4 Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 5 Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 6 Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 7 Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe.
\v 8 Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile.”
\p
\v 9 Wakamuuliza, “Wapi unataka tuyafanyie hayo maandalizi?”
\p
\v 10 Akawajibu, “Sikilizeni, mtakapokuwa mmeingia mjini, mwanamume ambaye amebeba mtungi wa maji atakutana na ninyi. Mfuateni kwenye nyumba ambayo ataingia.
\v 11 Kisha mwambieni bwana wa nyumba, “Mwalimu anakwambia, Kiko wapi chumba cha wageni, mahali ambapo nitakula Pasaka na wanafunzi wangu?’”
\v 12 Atawaonyesha chumba cha ghorofani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi humo.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 13 Hivyo wakaenda, na wakakuta kila kitu kama alivyowaambia. Kisha wakaandaa chakula cha Pasaka.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 14 Muda ulipofika alikaa na wale mitume.
\v 15 Kisha akawaambia, “Nina shauku kubwa ya kula sikukuu hii ya Pasaka na ninyi kabla ya kuteswa kwangu.
\v 16 Kwa maana nawaambieni, sitakula tena mpaka itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.”
\v 17 Kisha Yesu akachukua kikombe, na alipokwisha kushukuru, akasema, “Chukueni hiki, na mgawane ninyi kwa ninyi.
\v 18 Kwa maana nawaambia, sitakunywa tena mzao wa mzabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.”
\v 19 Kisha akachukua mkate, na alipokwisha kushukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.”
\v 20 Akachukua kikombe vivyo hivyo baada ya chakula cha usiku akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, ambayo imemwagika kwa ajili yenu.”
\v 21 Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.
\v 22 Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!”
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 24 Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote.
\p
\v 25 Akawaambia, “Wafalme wa watu wa mataifa wana ubwana juu yao, na wale mwenye mamlaka juu yao wanaitwa waheshimiwa watawala.
\v 26 Lakini haitakiwi kabisa kuwa hivi kwenu ninyi. Badala yake, acha yule ambaye ni mkubwa kati yenu awe kama mdogo. Na yule ambaye ni wa muhimu sana awe kama atumikaye.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 27 Kwa sababu yupi mkubwa, yule akaaye mezani au yule anayetumika? Je si yule aketie mezani? Na mimi bado ni kati yenu kama atumikaye.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 28 Lakini ninyi ndio ambao mmeendelea kuwa nami katika majaribu yangu.
\v 29 Nawapa ninyi ufalme, kama vile Baba alivyonipa mimi ufalme,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 30 kwamba mpate kula na kunywa mezani kwangu kwenye ufalme wangu. Na mtakaa kwenye viti vya enzi mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israel.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 31 Simoni, Simoni, fahamu kwamba, Shetani ameomba awapate ili awapepete kama ngano.
\v 32 Lakini nimekuombea, kwamba imani yako isishindwe. Baada ya kuwa umerudi tena, waimarishe ndugu zako.”
\p
\v 33 Petro akamwambia, “Bwana, niko tayari kwenda na wewe gerezani na hata katika mauti.”
\p
\v 34 Yesu akajibu, “Nakwambia, Petro, Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua.”
\p
\v 35 Kisha Yesu akawaambia, “Nilipowapeleka ninyi bila mfuko, kikapu cha vyakula, ua viatu, je mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu “Hakuna.”
\p
\v 36 Kisha akawaambia, “Lakini sasa, kila mwenye mfuko, na auchukue pamoja na kikapu cha vyakula. Yule ambaye hana upanga imempasa auze joho lake anunue mmoja.
\v 37 Kwa sababu nawaambia, yote ambayo yameandikwa kwa ajili yangu lazima yatimilike, Na alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati. Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu kinatimizwa.”
\p
\v 38 Kisha wakasema, “Bwana, tazama! Hizi hapa panga mbili.” Na akawaambia, “Yatosha.”
\p
\v 39 Baada ya chakula cha usiku, Yesu aliondoka, kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara, akaenda mlima wa Mzeituni, na wanafunzi wakamfuata.
\v 40 Walipofika, aliwaambia, “Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”
\v 41 Akaenda mbali na wao kama mrusho wa jiwe, akapiga magoti akaomba,
\v 42 akisema, “Baba, kama unataka, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nitakavyo mimi, lakini mapenzi yako yafanyike.”
\v 43 Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 44 Akiwa katika kuugua, akaomba kwa dhati zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yakidondoka chini.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 45 Wakati alipoamka kutoka katika maombi yake, alikuja kwa wanafunzi, na akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni yao,
\v 46 na akawauliza, “Kwa nini mnalala? Amkeni muombe, kwamba msiingie majaribuni.”
\p
\v 47 Wakati alipokuwa bado akiongea, tazama, kundi kubwa la watu likatokea, na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili akiwaongoza. Akaja karibu na Yesu ili ambusu,
\v 48 lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”
\p
\v 49 Wakati wale waliokuwa karibu na Yesu walipoona hayo yanayotokea, wakasema, “Bwana, je tuwapige kwa upanga?”
\v 50 Kisha mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
\p
\v 51 Yesu akasema, “Hii inatosha.” Na akagusa sikio lake, akamponya.
\v 52 Yesu akasema kwa kuhani mkuu, na kwa wakuu wa hekalu, na kwa wazee waliokuja kinyume chake, “Je mnakuja kana kwamba mnakuja kupambana na mnyang'anyi, na marungu na mapanga?
\v 53 Nilipokuwa pamoja nanyi siku zote kwenye hekalu, hamkuweka mikono yenu juu yangu. Lakini hii ni saa yako, na mamlaka ya giza.”
\p
\v 54 Wakamkamata, wakamuongoza, wakamleta nyumbani mwa kuhani mkuu. Lakini Petro akamfuatilia kwa mbali.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 55 Baada ya kuwa wamewasha moto katika ule uwanda wa ndani na walipokwisha kukaa chini pamoja, Petro akakaa katikati yao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 56 Mtumishi mmoja wa kike akamuona Petro alipokuwa amekaa katika mwanga utokanao na moto, akamtazama akamwambia, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja naye.”
\p
\v 57 Lakini Petro akakana, akasema, “Mwanamke, mimi simjui.”
\p
\v 58 Baada ya muda kidogo, mtu mwingine akamuona akasema “Wewe pia ni mmoja wao.” Lakini Petro akajibu, “Mwanaume, mimi siyo.”
\p
\v 59 Baada ya kama saa moja hivi, mwanaume mmoja akasisitiza akasema, “Kweli kabisa huyu mtu pia alikuwa pamoja naye, maana ni Mgalilaya.”
\p
\v 60 Lakini Petro akasema, “Mwanaume, sijui usemalo.” Na mara, wakati akiongea, jogoo akawika.
\p
\v 61 Akageuka, Bwana akamtazama Petro. Na Petro akalikumbuka neno la Bwana, pale alipomwambia, “Kabla ya jogoo kuwika leo, utanikana mimi mara tatu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 62 Akienda nje, Petro akalia kwa uchungu mwingi.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 63 Kisha wale wanaume waliokuwa wakimlinda Yesu, wakamdhihaki na kumpiga.
\v 64 Baada ya kumfunika macho, wakamuuliza, wakisema, “Tabiri! Ni nani aliyekupiga?”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 65 Wakaongea mambo mengine mengi kinyume cha Yesu na kumkufuru yeye.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 66 Mara ilipokuwa asubuhi, wazee wa watu walikusanyika pamoja, wakuu wa makuhani na waandishi. Wakampeleka kwenye Baraza,
\v 67 wakisema, “Kama wewe ni Kristo, tuambie.” Lakini yeye akawaambia, “Kama nikiwaambia, hamtaniamini,
\v 68 na kama nikiwauliza hamtanijibu.”
\v 69 Lakini kuanzia sasa na kuendelea, Mwana wa Adamu atakuwa amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu.”
\p
\v 70 Wote wakasema, “Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?” Na Yesu akawaambia, “Ninyi mmesema mimi ndiye.”
\v 71 Wakasema, “Kwa nini bado tunahitaji tena ushahidi? Kwa sababu sisi wenyewe tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\c 23
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 23
\p
\v 1 Mkutano wote wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.
\v 2 Wakaanza kumshutumu, wakisema, “Tumemkuta mtu huyu akipotosha taifa letu, kwa kukataza tusitoe kodi kwa Kaisari, na akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, Mfalme.”
\p
\v 3 Pilato akamuuliza, akisema, “Je wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Na Yesu akamjibu akisema, “Wewe wasema hivyo.”
\p
\v 4 Pilato akamuambia kuhani mkuu na makutano, “Sioni kosa kwa mtu huyu.”
\p
\v 5 Lakini wao wakasisitiza, wakisema, “Amekuwa akiwachochea watu, akifundisha katika Uyahudi yote, kuanzia Galilaya na sasa yuko hapa.”
\p
\v 6 Pilato aliposikia haya, akaulizia kama mtu huyo ni wa Galilaya?
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 7 Alipotambua kuwa alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka Yesu kwa Herode, ambaye naye alikuwa Yerusalemu kwa siku hizo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 8 Herode alipomuona Yesu, alifurahi sana kwa sababu alitaka kumuona kwa siku nyingi. Alisikia habari zake na alitamani kuona moja ya miujiza ikifanywa na yeye.
\v 9 Herode alimhoji Yesu kwa maneno mengi, lakini Yesu hakumjibu chochote.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Makuhani wakuu pamoja na waandishi walisimama kwa ukali wakimshitaki.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Herode pamoja na maaskari wake, walimtukana na kumdhihaki, na kumvika mavazi mazuri, kisha akamrudisha Yesu kwa Pilato.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 12 Herode na Pilato wakawa marafiki kuanzia siku hiyo, (kabla ya hapo walikuwa maadui).
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 13 Pilato akawaita pomoja makuhani wakuu na watawala na umati wa watu,
\v 14 Akawaambia, “Mmeniletea mtu huyu kama mtu anaye waongoza watu wafanye mabaya, na tazama, baada ya kuwa nimemhoji mbele yenu, sikuona kosa kwa mtu huyu kuhusu mambo yote ambayo ninyi mnamshitaki yeye.
\v 15 Hapana, wala Herode, kwa maana amemrudisha kwetu, na tazama hakuna chochote alichokifanya kinachostahili adhabu ya kifo.
\v 16 Kwa hiyo basi nitamuadhibu na kumuachilia.
\v 17 [Sasa, Pilato anawajibika kumuachilia mfungwa mmoja kwa wayahudi wakati wa sikukuu.]
\p
\v 18 Lakini wote wakapiga kelele pamoja, wakisema, “Mwondoe huyo, na tufungulie Baraba!”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 19 Baraba alikuwa ni mtu ambaye amewekwa gerezani kwa sababu ya uasi fulani katika jiji na kwa kuua.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 20 Pilato akawaambia tena, akitamani kumwachilia Yesu.
\p
\v 21 Lakini wao wakapiga kelele, wakisema, “Msulibishe, msulibishe.”
\v 22 Akawauliza kwa mara ya tatu, “Kwa nini, huyu mtu amefanya maovu gani? Sikupata kosa linalostahili adhabu ya kifo kwake. Kwa hiyo nitakapo maliza kumuadhibu nitamuachilia.”
\v 23 Lakini wakasisitiza kwa sauti ya juu, wakitaka asulubiwe. Na sauti zao zikamshawishi Pilato.
\v 24 Hivyo Pilato akaamua kuwapatia matakwa yao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 25 Akamuachilia yule waliyemtaka ambaye alifungwa kwa kusababisha ghasia na kuua. Lakini akamtoa Yesu kwa matakwa yao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 26 Walipokuwa wakimpeleka, walimkamata mtu mmoja aitwaye Simoni wa Ukirene, akitokea katika nchi, wakamtwika msalaba ili abebe, akimfuata Yesu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 27 Umati mkubwa wa watu, na wanawake ambao walihuzunika na kuomboleza kwa ajili yake, walikuwa wakimfuata.
\v 28 Lakini akawageukia, Yesu akawaambia, Mabinti wa Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe na kwa ya ajili watoto wenu.
\v 29 Tazama, siku zinakuja ambazo watasema, “Wamebarikiwa walio tasa na matumbo yasiyozaa, na matiti ambayo hayakunyonyesha.
\v 30 Ndipo watakapo anza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Mtufunike.
\v 31 Maana kama wakifanya mambo haya ikiwa mti mbichi, itakuwaje ukiwa mkavu?”
\p
\v 32 Wanaume wengine, wahalifu wawili, walipelekwa pamoja naye ili wauwawe.
\v 33 Walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo wakamsulubisha pamoja na wale wahalifu, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
\v 34 Yesu alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. “Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.
\v 35 Watu walikuwa wamesimama wakiangalia huku watawala wakimdhihaki, wakisema, “Aliwaokoa wengine. Sasa ajiokoe mwenyewe, kama yeye ni Kristo wa Mungu, mteule,”
\p
\v 36 Askari pia walimdharau, walimkaribia yeye na wakumpa siki,
\v 37 wakisema, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi jiokoe mwenyewe”
\v 38 Kulikuwa pia na alama juu yake iliyoandikwa “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.”
\p
\v 39 Mmoja wa wahalifu aliyesulubishwa alimtukana akisema, “Wewe si Kristo? Jiokoe mwenyewe na sisi”
\p
\v 40 Lakini yule mwingine akajibu, akimkemea na akisema, “Je wewe humuogopi Mungu, nawe uko katika hukumu hiyo hiyo?
\v 41 Sisi tupo hapa kwa haki, kwa maana sisi tunapokea kile tunachostahili kwa matendo yetu. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”
\v 42 Na aliongeza, “Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”
\p
\v 43 Yesu akamwambia, “Amini nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”
\p
\v 44 Hapo ilikuwa karibu saa ya sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa ya tisa,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 45 Mwanga wa jua ulizimika. Kisha pazia la hekalu likagawanyika katikati kuanzia juu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 46 Akilia kwa sauti kuu, Yesu alisema, “Baba mikononi mwako naiweka roho yangu,” baada ya kusema haya, akafa.
\p
\v 47 Wakati Akida alipoona yaliyotendeka alimtukuza Mungu akisema, “Hakika huyu alikuwa mtu mwenye haki.”
\v 48 Wakati umati wa watu waliokuja pamoja kushuhudia walipoona mambo yaliyofanyika, walirudi huku wakipiga vifua vyao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 49 Lakini marafiki zake, na wanawake waliomfuata toka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiangalia hayo mambo.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 50 Tazama, palikuwepo na mtu aitwaye Yusufu, ambaye ni mmoja wa baraza, mtu mzuri na mwenye haki,
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 51 (alikuwa hajakubaliana na maamuzi au matendo yao), kutoka Armathaya, mji wa Kiyahudi, ambao ulikua ukisubiria ufalme wa Mungu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 52 Mtu huyu, alimkaribia Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 53 Alimshusha, na akauzungushia sanda, na akaumweka katika kaburi lililokuwa limechongwa katika jiwe, ambalo hakuna aliyewahi kuzikwa.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 54 Ilikuwa ni siku ya maandalizi, na Sabato inakaribia.
\v 55 Wanawake, waliokuja nao kutoka Galilaya, walimfuata, na wakaona kaburi na jinsi mwili wake ulivyolazwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 56 Walirudi na kuanza kuandaa manukato na marashi. Kisha siku ya sabato walipumzika kwa mujibu wa sheria.
\c 24
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\cl Sura 24
\p
\v 1 Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa.
\v 2 Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 3 Wakaingia ndani, lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 4 Ilitokea kwamba, wakati wamechanganyikiwa kuhusu hili, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi ya kung'aa.
\v 5 Wanawake wakiwa wamejaa hofu na wakiinamisha nyuso zao chini, wakawaambia wanawake, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu?
\v 6 Hayupo hapa, ila amefufuka! Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa angali Galilaya,
\v 7 akisema kwamba Mwana wa Adamu lazima atolewe kwenye mikono ya watu wenye dhambi na asulubishwe, na siku ya tatu, afufuke tena.”
\v 8 Wale wanawake wakakumbuka maneno yake,
\v 9 na wakarudi kutoka kaburini na wakawaambia mambo haya yote wale kumi na moja na wengine wote.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 10 Basi Maria Magdalena, Joana, Maria mama wa Yakobo, na wanawake wengine pamoja nao wakatoa taarifa hizi kwa mitume.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 11 Lakini ujumbe huu ukaonekana kama mzaha tu kwa mitume, na hawakuwaamini wale wanawake.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 12 Hata hivyo Petro aliamka, na akakimbia kuelekea kaburini, na akichungulia na kuangalia ndani, aliona sanda peke yake. Petro kisha akaondoka akaenda nyumbani kwake, akistaajabu nini ambacho kimetokea.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 13 Na tazama, wawili miongoni mwao walikuwa wakienda siku hiyo hiyo katika kijiji kimoja kiitwacho Emmau, ambacho kilikuwa maili sitini kutoka Yerusalemu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 14 Wakajadiliana wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotokea.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 15 Ikatokea kwamba, wakati walipokuwa wakijadiliana na kuulizana maswali, Yesu akasogea karibu akaambatana nao.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 16 Lakini macho yao yalizuiliwa katika kumtambua yeye.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 17 Yesu akawaambia, “Nini ambacho ninyi wawili mnakiongelea wakati mnatembea?” Wakasimama pale wakionekana na huzuni.
\p
\v 18 Mmoja wao, jina lake Cleopa, akamjibu, “Je wewe ni mtu pekee hapa Yerusalemu ambaye hajui mambo yaliyotokea huko siku hizi?”
\p
\v 19 Yesu akawaambia, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo kuhusu Yesu Mnazareti, ambaye alikuwa nabii, muweza katika matendo na maneno mbele za Mungu na watu wote.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 20 Na kwa jinsi ambayo wakuu wa makuhani na viongozi wetu walivyomtoa kuhukumiwa kifo na kumsulubisha.
\v 21 Lakini tulitumaini kwamba yeye ndiye atakaye waweka huru Israeli. Ndiyo, mbali na haya yote, sasa ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 22 Lakini pia, baadhi ya wanawake kutoka katika kundi letu walitushangaza, baada ya kuwapo kaburini asubuhi na mapema.
\v 23 Walipoukosa mwili wake, wakaja, wakisema kwamba waliona pia maono ya malaika waliosema kwamba yu hai.
\v 24 Baadhi ya wanaume ambao walikuwa pamoja nasi walienda kaburini, na kukuta ni kama vile wanawake walivyosema. Lakini hawakumuona yeye.”
\p
\v 25 Yesu akawaambia, “Ninyi watu wajinga na wenye mioyo mizito ya kuamini yote ambayo manabii wamesema!
\v 26 Je haikuwa lazima Yesu kuteseka kwa mambo haya, na kuingia katika utukufu wake?”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 27 Kisha kuanzia kutoka kwa Musa na manabii wote, Yesu akawatafsiria mambo yanayomuhusu yeye katika maandiko yote.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 28 Walipokaribia kile kijiji, huko walikokuwa wakienda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea mbele.
\v 29 Lakini walimlazimisha, wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana inaelekea jioni na siku ni kama imeisha.” Hivyo Yesu akaingia kwenda kukaa nao.
\v 30 Ilitokea kwamba, wakati amekaa nao kula, alichukua mkate, akaubariki, na kuuvunja, akawapa.
\v 31 Kisha macho yao yakafunguliwa, wakamjua, na akatoweka ghafla mbele ya macho yao.
\v 32 Wakasemezana wao kwa wao, “Hivi mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, wakati alipoongea nasi njiani, wakati alipotufungulia maandiko?”
\v 33 Wakanyanyuka saa hiyo hiyo, na kurudi Yerusalemu. Wakawakuta wale kumi na mmoja wamekusanyika pamoja, na wale waliokuwa pamoja nao,
\v 34 wakisema, “Bwana amefufuka kwelikweli, na amemtokea Simoni.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 35 Hivyo wakawaambia mambo yaliyotokea njiani, na namna Yesu alivyodhihirishwa kwao katika kuumega mkate.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 36 Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, “Amani iwe kwenu.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 37 Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 38 Yesu akawaambia, Kwa nini mnafadhaika? Kwa nini maswali yanainuka mioyoni mwenu?
\v 39 Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo.”
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 40 Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 41 Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, “Je mna kitu chochote cha kula?”
\v 42 Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 43 Yesu akakichukua, na kukila mbele yao.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 44 Akawaambia, “Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike.”
\v 45 Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko.
\v 46 Akawaambia, “Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 47 Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 49 Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\p
\v 50 Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki.
2017-11-08 21:23:27 +00:00
\v 51 Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni.
2023-10-13 17:25:12 +00:00
\v 52 Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu.
\v 53 Waliendelea kuwepo hekaluni, wakimsifu Mungu.